Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

sio lazima ukurupuke, anataka umaarufu wa kijinga bwana, mm ni mwenyekti wangu ila namjua hana uwezo binafsi
 
Wakuu mmeniacha nje kabisa wala sielewi kinachojadiliwa hapa!
 
wewe ndio wa kupimwa akili maana hujui hata unachochangia au unatumia pc ya ofisi? hiyo bajeti unayoifagilia ni ipi hii ya mkulo au zitto kabwe..? kama ni ya mkulo itakuwa nzuri kwako kama wewe ni mtendaji wa polisi, mahakam, tra au cleaner wa white house au parliament soma alama za nyakati huitaji PHD kujua hilo bob
huyu mbowe akapimwe akili bajeti imetimiza matakwa ya wananchi.mi sioni tatizo na hii bajeti na kwa hili CCM wameonyesha kutujali sisi wananchi ambao ni mahohehahe wakutupa.
 
Kinachojadiliwa hapa ni Mh mbowe kuikubali bajeti baada ya kipindi cha bunge na hatimaye kambi rasim ya upinzani kuipinga..uko apo bob??
Ok lakini ili tujadili hoja ya Mbowe ktk kusifia kwake ni bora yawekwe maelezo yake yeye binafsi dhidi ya hotuba ya Zitto na Mnyika ambao nijuavyo wametangaza kwa niaba yaa..
 
 


Waziri alisema zipo 21, wewe umeweka 18 na tuu! Mojawapo ambayo siioni hapo ni road toll or something similar
 
MKE wa Rais, Salma Kikwete, amesifu bajeti ya serikali ya mwaka ujao wa fedha na kusema kwamba imeonesha dhamira ya dhati ya Rais Jakaya Kikwete, kuwaletea Watanzania maisha bora kwa kuboresha sekta ya elimu.

Katika hatua nyingine, Mama Kikwete amewataka walimu wanaopangiwa kwenda kufundisha katika shule za msingi zilizopo vijijini, kuitikia hatua hiyo ili kuiwezesha serikali kufanikiwa katika uboreshaji wa elimu inayotolewa kwenye shule za sekondari za kata.

Ameeleza msimamo wake pia kuhusu mtazamo wa wadau kutaka watoto wa kike kuruhusiwa kurudi shuleni na kuendelea na masomo baada ya kupewa mimba na kujifungua kwa kusema kuwa kwa maoni yake binafsi na si kama mke wa Rais, mtazamo huo si wa kukurupukia.

Ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akiwahutubia wadau wa kongamano la kujadili mikakati ya kuwawezesha na kuwaendeleza kielimu watoto wa kike wanaotoka katika mazingira hatarishi na yatima waliopo shuleni, lililoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Camfed Tanzania.

Akizungumzia uboreshaji wa sekta ya elimu, Mama Kikwete alisema serikali imedhamiria kwa dhati kuboresha sekta ya elimu na kumkomboa mtoto wa kike ili kumjengea maisha bora ya hapo baadaye.Alisema bajeti ya mwaka ujao wa fedha ni kielelezo cha jitihada hizo.

"Shule za Sekondari za Kata ni moja ya vielelezo vinavyodhihirisha azma hii ya Rais Kikwete, pamoja na kuwepo kwa changamoto zinazozikabili. Kabla ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani, watoto walikuwa wanafaulu lakini wanakosa nafasi za kuendelea na masomo kwa ukosefu wa shule, lakini sasa wote wanakwenda shule."

Amesema, kielezo kingine ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alichosema ni gumzo sasa kwa mataifa mbalimbali Duniani kutokana na kuwa na vyuo sita ndani yake kikiwemo Chuo cha Elimu ambacho kina uwezo wa kuwachukua wanafunzi 15,000 kwa pamoja wanaosomea kozi ya Ualimu.

Kuhusu walimu wanaopangiwa kufundisha shule za vijijini lakini wanakaidi agizo hilo, Mama Kikwete amelaani vikali hatua hiyo na kusema inarudisha nyuma jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu na hasa katika sekondari za kata.

"Mimi pia nilianzia ualimu vijijini wakati huo nilikuwa sijaolewa nikiitwa Salma Rashid. Nakumbuka mara ya kwanza nilipangiwa kufundisha Shule ya Msingi Chiponji iliyopo katika Wilaya ya Lindi Vijijini mkoani Lindi na nakumbuka kufika kijijini hapo wakati ule hakukuwa na usafiri wa basi na ilibidi nipande trekta. Ni vizuri walimu wakawa wazalendo kwa kukubali kufundisha vijijini," amesema.

Akizungumzia mtazamo wa wadau wa elimu kutaka wanafunzi wa kike wanaopewa mimba wakiwa shuleni kuruhusiwa kuendelea na masomo baada ya kujifungua, Mama Kikwete pamoja na kusema kuwa suala hilo linatazamwa kisheria hivi sasa, lakini alitoa msimamo wake binafsi.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Camfed Tanzania, Msaada Balula, amesema shirika hilo limepata mafanikio makubwa katika kuboresha maisha ya mtoto wa kike nchini kwa kuwajengea uwezo kielimu, kimaarifa na kiuchumi.

Source: Habari Leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…