Bunge la chini la Zimbabwe lapitisha muswada wa kuongeza muda wa Rais kukaa madarakani kutoka miaka 5 hadi 7

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Bunge la chini la Zimbabwe limepitisha mswada unaolenga kuongeza muda wa rais kukaa madarakani kutoka miaka mitano hadi saba. Hatua hii inampa mwanya Rais Emmerson Mnangagwa kusalia madarakani hadi mwaka 2030. Mswada huo ulipata uungwaji mkono wa wabunge 216 na kuvuka theluthi mbili zinazohitajika, na sasa unatarajiwa kupita kiulaini katika bunge la juu ambako chama tawala cha ZANU-PF kina ushawishi na udhibiti mkubwa.​

​

Dalili za Rais Mnangagwa, ambaye sasa ana umri wa miaka 83, kutaka kuongezewa muda zilianza kuonekana miaka miwili iliyopita pale wafuasi wake walipoanza kumpigia chapuo wakidai anahitaji muda zaidi kukamilisha mipango yake. Wakati wafuasi wakitetea hatua hii, wakosoaji wanasema huu ni ujanja tu wa kung'ang'ania madaraka. Aidha, baadhi ya wanaharakati walijaribu kupinga mpango huu mahakamani, lakini kesi zao zilitupiliwa mbali kutokana na kasoro za kisheria.

Mnangagwa, anayejulikana sana kwa jina la utani kama "Mamba", aliingia madarakani mwaka 2017 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa mtangulizi wake Robert Mugabe, ambaye alikuwa mshirika wake wa karibu kwa miaka mingi. Hatua hii ya kubadili sheria ili kusalia madarakani inafuata mkumbo uliopo katika baadhi ya nchi za Afrika kama Uganda na Cameroon, ambapo viongozi wakongwe wanaendelea kujikita madarakani licha ya kuongoza idadi kubwa ya raia vijana.​

=========== For English Audience ===========
​
Zimbabwe lawmakers back legislation extending president's time in power

HARARE, June 18 (Reuters) - Zimbabwe's lower house of parliament passed a bill to extend presidential terms from five to seven years on Thursday, which would allow President Emmerson Mnangagwa to remain in power until 2030.
Some 216 lawmakers voted in favour of the draft legislation, passing the 187 mark needed for a two-thirds majority.

The bill now moves to the upper house of ⁠parliament, where it is also expected to sail through as Mnangagwa's governing ZANU-PF party controls it through traditional leaders and other proxies who generally vote with the party.

Signs that Mnangagwa, 83, wanted to stay in power beyond the end of his second term in 2028 emerged about two years ago, when his supporters started chanting slogans at ZANU-PF rallies that he needed more time to complete his agenda. The party last year resolved to change the constitution to lengthen presidential terms, and the plan received cabinet backing in February.
Critics say the bill is a ruse for Mnangagwa to ‌stay ⁠in power for longer, though its backers say it will strengthen accountability and foster political stability.

ZIMBABWE'S 'CROCODILE' PRESIDENT
Mnangagwa is nicknamed "the crocodile," an animal portrayed in Zimbabwean lore as stealthy and ruthless. He came to power after a 2017 military coup ousted longtime leader Robert Mugabe, who had been in power since independence in 1980. Until ⁠they fell out in the months leading up to the coup, Mnangagwa was one of Mugabe's closest lieutenants, serving in top government positions including vice president.

Some activists and veterans of the country's liberation war launched court ⁠challenges against the plan to extend Mnangagwa's time as head of state, but they were struck off the court roll this week for technical reasons. Other African countries whose leaders have changed ⁠the law to stay in power for longer include Cameroon and Uganda, entrenching a trend on the continent where some of the world's oldest leaders govern its youngest populations.

SOURCE: REUTERS
 
Zimbabwe wanapata faida gani kumng'ang'ania mganga wa kienyeji Mnangagwa!
Hawawezi kumpata dikteta mzuri?
 
Huyu ndiye wapigania ukombozi yeye na Mugabe wakiwa mstuni Bulawayo North Rhodesia, walifukuza wazungu si kwa sababu ya uzalendo Bali uroho na uchu wa kupata madaraka
 
Bunge letu pia litafanya kitu kumuongeze Mama Dr Samia muda ili atuongoze hadi 2037 kwa sababu ndo hitaji la wananchi wengi kwa sasa.
 
Namsihi Rais Samia naye afuate huu mpango wa chama rafiki wa ccm. Naye aongeze muda hadi 2035 maana ndiyo kaanza awamu yake. Ile ya 2021 to 2025 alikuwa anamalizia ngwe ya Magufuli
Aishi Milele Mtukufu Rais wetu Samia🫱🏽‍🫲🏾
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…