Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Sheria inayotoa mamlaka kwa mtu kujipima UKIMWI

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, amesema kuwa hadi kufikia Ijumaa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaipitisha Sheria inayotoa mamlaka kwa mtu kujipima UKIMWI.

Hayo ameyabainisha leo Novemba 11, 2019 wakati wa ufunguzi wa semina elekezi kwa wasanii mbalimbali iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamin Mkapa pamoja na Baraza la watu wanaoishi na UKIMWI (NACP).

“Changamoto kubwa inayoikabili Wizara ya Afya katika suala zima la VVU na UKIMWI ni wanaume kutojitokeza kwa wingi kupima, na hapa ninavyoongea leo hadi Ijumaa sheria ya watu kujipima wenyewe Virusi vya UKIMWI majumbani kwao itapitishwa rasmi, lakini hata hivyo itampasa mtu kwenda hospitali kupima tena ili ajiridhishe hata kama atakuwa ameshajipima mwenyewe” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameongeza kuwa Wizara yake imepeleka mapendekezo ya sheria itakayoruhusu umri wa mtu kupima Virusi vya Ukimwi uanzie miaka 15.

Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wasanii wote waliohudhuria semina hiyo kutumia wafuasi wao walionao kupitia matamasha na hata mitandao ya kijamii kutoa elimu sahihi juu ya VVU na UKIMWI mwenyewe ili kutimiza lengo la Serikali la kuwa na asilimia 0 ya maambukizi mapya ifikapo mwaka 2030.
 
“Changamoto kubwa inayoikabili Wizara ya Afya katika suala zima la VVU na UKIMWI ni wanaume kutojitokeza kwa wingi kupima, na hapa ninavyoongea leo hadi Ijumaa sheria ya watu kujipima wenyewe Virusi vya UKIMWI majumbani kwao itapitishwa rasmi, lakini hata hivyo itampasa mtu kwenda hospitali kupima tena ili ajiridhishe hata kama atakuwa ameshajipima mwenyewe” amesema Waziri Ummy.

Bora kujipima majumbani, mahospitalini nyodo nyingi, masimamngo mengi, matangazo ya siri za wagonjwa ndiyo jadi,
 
Sio hivyo tu mkuu,yale mambo ya kupima na kumwambia mtu atoke nje asubirie kuitwa kwakweli yanakatisha sana tamaa,kuna jamaa wengi wanajikuta wakitoka nje hawatamani tena kusikia majibu yao na kujikuta tu wako barabarani wanarudi makwao bila ya majibu...
 
Mchawi ni majibu na ukifika mda Wa kupewa majibu kwanza ushauri unaanza unaweza hisi tayari ushaungua,kuna kipindi tuko advance level tukaenda kupima sasa kwenye kupewa majibu sasa ukaanza ushauri Mara huku kuna ngoma sana so vijana tutumie kinga,jamaa mmoja akasema yeye angekutwa na ngoma ndio hata shule asingerudi tena
 
1573582454090.png

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tayari limeipitisha rasmi sheria inayompa mamlaka, mtu kujipima mwenyewe Virusi vya Ukimwi kwa kutumia sampuli zinazotoka kwenye kinywa, pamoja na sheria inayoruhusu kijana kuanzia miaka 15, kupima Ukimwi bila ridhaa ya mzazi.

Sheria hiyo imepitishwa leo Novemba 12, 2019, na kwamba sheria hiyo itasaidia watu kujitambua hali zao mapema, hususani wanaume na kundi la vijana, ambalo kwa sasa ndilo linaloongoza kuwa na waathirika wengi wa ugonjwa huo.

Akizungumza bungeni Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile, amesema kuwa tayari Wizara imekwishajipanga juu ya upatikanaji wa vipimo hivyo na tayari imeshaanza kufanya majaribio ya mifumo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia mapokea kutoka kwa wananchi.

"Vipimo hivi havitakuwa vinatumia damu, vitakuwa vinatumia sampuli ya kinywa na hii watu watapima hata kabla ya kujamiiana na watakapobaini wamepata changamoto hizo wanakuja katika vituo vya kutoa huduma za afya ili kujiridhisha,vijana wengi wameanza kuathirika na kujamiiana wakiwa na umri mdogo, sasa tunatoa fursa kwa vijana kuanzia miaka 15 kupima Ukimwi bila ridhaa ya mzazi wake" amesema Waziri Dkt Ndugulile.
 
Nimemuuliza maswali hajajibu

Moja, amesema itachangia kufikia malengo ya 90-90-90! Kama huyajui soma UNAIDS. Nikauliza kuwa hizo takwimu tutazipataje ili tujue kuwa 90% watakua wamepima na kujua their HIV status by 2020? Maana kama MTU anajipima Mwenyewe hashurutishwi kupeleka majibu yake kwenye kituo cha Afya. Kama watakuepo basi ni wachache sana.

Pili, Disclosure bado ni tatizo kubwa sana kwenye jamii, na hii inatokakana na kuwepo kwa Stigmatization, je, hii itasaidiaje kuongeza uwazi kwa waathirika watakaokuwa wamegundulika?

Tatu, tumejiandaaje na Shock kwa wale ambao watapata majibu tofauti na matarajio yao? Kuna wengine hawawezi kustahimili, tumejiandaaje kudhibiti Suicide?

NNE, anasema wamepunguza Parental Consent ya kupima hadi 15yrs, hili ni zuri sana maana limekua changamoto sana tunapokua field! Kwa mfano, mikoa ya Kigoma hasa maeneo ya Wakimbizi, miaka 15 ni tayari ana watoto kama sio mtoto! Kwahio hili ni zuri! TATIZO linakuja hapa, tumepunguza umri wa kuhutajika kwa Parental Consent LAKINI tunakataa Wasifanye ngono katika umri huo au kuolewa hadi 18yrs! Naona kama vile kuna contradiction hapa!

Kwa sasa hii ndio nime-observe! Nashukuru wameturahisishia kuwapima ngoma hawa watoto maana ilikua ukienda pale MAKEI (panaitwa Makei kutokana na wingi wa upatikanaji wa Nyuchi) kule Mafinga unavikuta vitoto vinajiuza hadi unaogopa!
 
View attachment 1261625

Vifaa vinapatikana wapi!?
 
Mimi nnazo SD Bioline huwa nampima mpenzi wangu kila nikikutana naye. Mara flani nilikutana na binti nikawa sina nikapiga dry,niliwaza sana ile miezi
 
Kuna watu wengi sana warajiua

MAKEI inapatikana maeneo gani hapo Mafinga Mkuu wa Kikosi? Nataka nikafanye utafiti kidogo.
 
Back
Top Bottom