Bunge la Katiba: CHADEMA imekosea sana katika hili

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
6,557
Reaction score
25,717
Binafsi ninaamini kuwa wapo watu wengi sana ndani ya Chama cha Chadema ambao ni 'smart' zaidi yangu lakini mara nyingi huwa nashangaa sana juu ya maamuzi wanayoyafanya na huwa na-question kama wamefanya mashauri ya kina.!
Katika 'movie' inayoendelea dodoma kuhusu utungaji wa katiba mpya, umeibuka mjadala hivi karibuni kuwa nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo. Makundi mbalimbali yametoa misimamo mbalimbali kuonyesha wanamtaka nani hasa kwa kuzingatia maslahi yao.! Katika mazingira haya ya 'kampeni' na 'kufagilia' nani awe Mwenyekiti wa kudumu nimeshangazwa sana kuona chama cha Chadema kikimuunga mkono wazi wazi Mhe. S. Sitta!! Watu wengi wameupigia debe uamuzi huu wa chadema lakini binafsi nimeshangazwa mno.. Kwanini??
Kwanza nianze kwa kukiri kuwa ni kweli tunatunga katiba ya watanzania wote, lakini pia ni lazima na ni wajibu wa kila kundi/kikundi kuwa makini kulinda maslahi yake ya kitaasisi na kisekta/nyanja katika ujumla wake.! Ninachomaanisha hapa ni nini? Ni dhahiri kuwa kila taasisi/nyanja/sekta iliyopo pale dodoma Bungeni ina maslahi inayojitahidi kuyapigania, hivyo inajitahidi kuangalia njia na mbinu mbalimbali ili kufanikisha hilo. Katika mbinu hizo ndipo chama cha Chadema kikaamua kuweka wazi msimamo wake wa kumpigia debe Mhe. S. Sitta ikidhani kuwa ni hatua ya kimkakati kufanikisha 'kupush' agenda wanazozipigania. Watu wengi sana wameipigia chapuo hatua hii, binafsi naamini Chadema wamepigwa goli dakika ya kwanza alafu wanashangilia! Ntafafanua;

i) CHADEMA HAIJAANGALIA MBALI
- katika siasa kuna mbinu huwa napenda kuiita 'acha wafu wazikane', naomba nielezee kidogo. Ndani ya CCM kulikuwa na makundi yanayosigana ambapo kila kundi lilikuwa na nia ya kusimamisha mtu wao, nikiyaorodhesha machache, kuna kundi lilitaka kumsimamisha chenge, wengine walitaka asimame Mama Migiro na kuna kundi na lingine lilimtaka Sitta! Huu mkanganyiko ndani ya CCM ulikuwa na uwezo wa ku-work on Chadema's favor kama wangeutumia vizuri. Kulikuwa na kila dalili ya kundi moja kulikwamisha kundi lingine ndani ya CCM wenyewe hili mtu wa kundi lingineisichukue nafasi ya uenyekiti. Kitendo cha Chadema kuonyesha upande waliopo uliwafanya CCM waungane na kuamua kumpitisha kwa makubalino maalum. (Kulinda maslahi ya chama) hivyo Chadema wasahau kuhusu Sitta kuwafanyia 'favor' zozote zile ndani ya bunge..
Chdema walipaswa wakae kimya katika ili, walitakiwa "kuwaacha wafu wazikane" ili wagawanyike na iwe rahisi kuwadhibiti

ii) CHADEMA wamekiri ni Dhaifu
Binafsi nimetafsiri kitendo cha Chadema kumpigia debe mtu wa CCM kama ni kitendo dhaifu na kuwa hawana ushawishi wowote ndani ya bunge. Hata kama wana idadi ndogo lakini walipaswa kujikakamua na kumuunga mkono mtu sahihi hata kama hatoshinda, hii ingetufanya tuwe na imani kuwa wako pale wanajua wanachokifanya..

iii) CHADEMA haijifunzi
Mwaka 2010, Chadema walimfuata Mhe. Sitta na kumuomba agombee urais kupitia chama chao!! Baada ya mazungumzo marefu Sitta 'akawachomolea' na wengi hata hawakulijua hili suala.
Jambo la kusikitisha mwaka Jana Mhe. Sitta akatokea hadharani na kusema kuwa chadema hakuna kiongozi ndio maana hata walidiriki kumfuata na kumpigia magoti agombee uraisi kupitia chama chao. Binafsi sielewi chadema inawezaje kumuamini mtu wa namna hii.

iv) CHADEMA imejitia pingu
Kama Sitta ataharibu (and am sure he will) sitegemei kusikia malalamiko kutoka chadema kwasababu wametumia nguvu nyingi sana kumpigia debe...
 
Kwa hali halisi ilivyo Mwenyekiti hawezi kutoka nje ya CCM hivyo kama CDM wanamkubali Sita kosa lipo wapi? Sitta aliishajijengea heshima ndani na nje ya Bunge wakati alipokuwa Spika kwa hiyo ana sifa hata mimi namkubali.labda nikuulize tu wewe ulitaka awe nani tofauti na Sitta?
 

Issue hapa si nani au nani awe mwenyekiti! Ninachokiongelea hapa ni suala la mikakakati na uwezo wa kutumia 'matukio' ndani ya bunge ku-gain influence..!
 
mchambuzi bado ni kilaza...kuna wana CCM wengi tuu CDM wanawacontrol ktk wanaowania....na support ya cdm kwa mwana CCm yeyote ni kuidhoofisha CCM kwa kuongeza tofauti za kimakundi
 
mjomba kwa vile zaidi ya 70 percent ya maoni ya rasimu yanatoka cdm , ni lazima kama chama tutafute namna ya kusimamia hili , sasa huwezi jua makubaliano ya 6 na cdm namna ya kupeleka mbele jambo hili , time will tell .
 
mchambuzi bado ni kilaza...kuna wana CCM wengi tuu CDM wanawacontrol ktk wanaowania....na support ya cdm kwa mwana CCm yeyote ni kuidhoofisha CCM kwa kuongeza tofauti za kimakundi

Asante kwa kuniita kilaza, but hata hao experts hawakuwa hivyo in one night! Thanks anyway..
 
Ninachoamini mimi, Sitta ni mwanaCCM na ni waziri ktk serikali ya CCM. Mwisho wa siku atajitahidi maslahi ya CCM yawe implemented. And I believe he will do it in a style, wait and you will see!

mjomba kwa vile zaidi ya 70 percent ya maoni ya rasimu yanatoka cdm , ni lazima kama chama tutafute namna ya kusimamia hili , sasa huwezi jua makubaliano ya 6 na cdm namna ya kupeleka mbele jambo hili , time will tell .
 
navyoona CCM pia kuna kilio, lowasa kazidiwa nguvu hapa na hili liko dhahiri baada ya mpambe wake chenge kukosa ushawishi,SITA anazo ndoto sawa na za adui yake lowasa na nina uhakika SITA atataka atumie bunge hili kujijenga kuelekea uchaguzi mkuu kwa wananchi maana ndani ya chama tayari analo kundi kama inavyojionyesha sasa,na hapo ndo naona CCM itapata shida,Sita hawezi kuacha kutaka kuongeza ushawishi na imani kwa wananchi kisa CCM wakati hata CCM tayari anaisema,ni kweli pia kuwa ilitakiwa cdm wawe na mkakati wao lakini ufanisi utakuwaje katika bunge lililojaa MACCM? CHADEMA isingeshind,lakini hofu yao ilikuwa ni kwa chenge,huyu ni mwanasheria wa CCM na anatetea CCM waziwazi na misimamo yake,kwa hiyo ukiangalia kwa makini unaweza kukubali kuwa ilikuwa sahihi kumuunga mkono SITA ili anaehofiwa zaidi asipite,na inawezekana kama bila support ya cdm kwa sita huenda chenge ndo angepita na kama hesabu zilikuwa vile basi cdm walikuwa sawa.

pia CCM watakuwa walipiga hesabu na kugungua kuwa Chenge hawezi kupenya na safari hii wameshindwa kutumi ile mbinu ya kutaka mwenyekiti kwa jinsia. na itakuwa kweli kuwa chenge singepita kwa kuwa tayari CCM imegawika,washabiki wa SITA wataendelea kuwa wa SITA na wa CHENGE PRO LOWASA WATAENDELEA KUWA WA CHENGE NA HAWAWEZI KUUNGWANISHWA NA RASIMU HII
 
mjomba kwa vile zaidi ya 70 percent ya maoni ya rasimu yanatoka cdm , ni lazima kama chama tutafute namna ya kusimamia hili , sasa huwezi jua makubaliano ya 6 na cdm namna ya kupeleka mbele jambo hili , time will tell .

Makubaliano kati ya chdm name sita yalishindikana toka 2010, this time nataka nikuhakikishie hakuna makubaliano yoyote yale! Na kama kungekuwa na makubaliano yoyote yale kati ya 6 na chadema, ccm wasingelikubali ku-'consede' kirahisi hivyo kumuacha sita achukue uenyekiti! Chadema wanahisi kuwa sita ni 'afadhali' kuliko Chenge, but they will be surprised!! Ngoja tusubiri
 
Asante kwa kuniita kilaza, but hata hao experts hawakuwa hivyo in one night! Thanks anyway..
ukiangalia vyema..CDM wana kura ya Siri nadhani unajua hofu ya CCM, wana Serikali 3 nadhani wazenj wote wa CUF na CCM wanataka hilo achilia mbali wana CCM wa bara, wana vyama vya kiraia na wanaharakati, wana wana CCM zaidi ya 50 wa 6 ambaow anaifanyia kzi CDM ndani ya CCM
 
Siku zote mahaba huwatia upofu watu. sitarajii na wala sitegemei Mh. Sitta afanye kinyume na msimamo wa chama chake ambacho kimsingi ndicho kimemteua ili asimamie kazi maalumu.

Mh. Sita ni mzuri sana kwa kuuma huku na huku, na kwa kweli atawauma sana wale wanaodhani atapinga msimamo wa chama chake.

Na sasa kama kura za wengi (CCM) zikisema hapana, Mh. Sitta ni nani hadi aseme ndiyo eti kuwafurahisha wapinzani?

Labda kwa muujiza wa Mwenyezi Mungu tutapata Katiba Mpya itakayokubalika na Watanzania wote chini ya wajumbe wengi makada wa CCM. vinginevyo kama alivyosema Mzee Mwanakijiji "tumekubali kushiriki mchakato haramu, tuwe tayari kukubali na matokeo yake"
 
wana wana CCM zaidi ya 50 wa 6 ambaow anaifanyia kzi CDM ndani ya CCM

Am not so sure about that mkuu.! Mara nyingine huwa tunapenda kujiaminisha hiyo..
Turudi kwa topic, kama hizi 'facts' zita-work out kama ulivyoeleza, chadema wanapaswa wakae chini na kukuna kichwa hasa ili waelewe game plan ya ccm, kwasababu siamini kama ccm ni mazezeta kiasi cha kukubali ku-consede kirahisi hivyo..
 
chenge hata kkunganisha setsi hawezi tena, achilia mbali kujieleza kwa lugha yoyote
 
wala uiswe sure ili CDM Mpigwe bao...huo ndio ukweli.Km 6 alifika mbali mwanzoni nini kinamshinda sasa?na si yeye pekee wapo wengine..kwa ujumla Bunge hili lipo infected with CDMism
 
Nadhani kicho kidogo atakachouma CCM kinaitosha CDM..kwani serikali 3 nayo inawapa CDM marafiki Zenj na bara ktk CCM..km 6 atauma kidogo basi kibaba kitajaa.....
 
,washabiki wa SITA wataendelea kuwa wa SITA na wa CHENGE PRO LOWASA WATAENDELEA KUWA WA CHENGE NA HAWAWEZI KUUNGWANISHWA NA RASIMU HII

Niliposema ccm wameunganika sikuwa na maana kuwa zile kambi zao za urais zimeunganika, la hasha! Wameunganika katika mchakato wa kumpata mwenyekiti, kuweka tofauti zao za ki-kambi pembeni na kujaribu kufanya kazi pamoja kutetea maslahi yao yanayofanana, tukumbuke kuwa kuna maeneo mengi sana kwenye rasimu ambayo Team El na Team Sitta wana maslahi yanayo fanana.!

Pia umesema Sitta hawezi kuwaangusha wananchi ili kuitetea ccm, hii inaweza kuwa kweli au si kweli! Kwanini? Sitta anafahamu kuwa bado hana ushawishi wa kutosha ndani ya chama ukilinganisha na EL, hivyo anaweza kutumia karata hii ili aweze kupata confidence ya chama kwa kuhakikisha analinda maslahi ya chama.! Kwasababu anafahamu kuwa hata kama wananchi wakimpenda ila kama chama akitamchagua kama mgombea wao wa urais haita kuwa na manufaa yoyote! Naamini tunakumbuka fitna alizofanyiwa Salim mwaka 2005 licha ya kupendwa na wengi..!
 
labda mimi sielewi maana ya kuunganika,lakini hata nikifa sasa nasema ccm hawajaunganika kumpata mwenyekiti wao,kuunganika maana yake mnakuwa kitu kimoja na kuondoa tofauti zenu,unataka kuniaminisha LOWASA ameondoa tofauti zake kwa SITA? CHENGE nae?na wale washabiki wakubwa wa lowasa wanaomchukia SITA,sitaki kuamini na sitakuja kuamini.

kilichofanyika siyo ccm wameungana bali CCM wameamua kuondoa mgombea mmoja abaki mmoja,haya mambo si ndio yale ya kipindi cha mwinyi na nyerere,unaletewa kuchagua MWINYI na BOX TUPU ama NYERERE na BOX TUPU, hiyo haikumaanisha CCM walikuwa wamoja na ndio maana wengine hawakutaka ila hawakuwa na chaguo lingine.

wewe subiri wakati wa kura,zingine zitaharibika ama wengine hawataenda kabisa kupiga kura,kura zote zitakuwa chini ya 600 maana najua wasiomuunga mkono kwa itikadi za makundi hwwezi kirahisi kumpigia kura.

kwanza nikusahihishe,sikusema hawezi kuwaangusha wananchi,nimesema atataka kujiimrisha kwa kujikusanyia wafuasi wengi kwenye jamii n hiyo ndio silaha kubwa kwake.

nikikuuliza leo nini sababu ya CCM kumpitisha SITTA utaniambia ni ushawishi ndani ya CCM? SITTA hana ushawishi mkubwa sana ndani ya CCM ila ana wafuasi wengi sana ambao ni wananchi,NA KAMA HUJUI SIASA NAKUELEZA WAZI KUWA HAKUNA NGUVU KUBWA KAMA KUKUBALIKA NA WATU HATA CHAMA HAKIFUI DAFU,leo ccm wamelazimika kumwanchia sita baada ya kubaini nguvu kubwa anayopewa na wananchi hasa walioteuliwa na raisi na hao ndio wamemuokoa na wasingekuwa hao CCM wangemtosa LIVE,na hata 2015 kama SITA akijijengea umahiri mkubwa na imani kubwa CCM itapata shida sana,maana wakichagua kumtosa wanachagua kushindwa uchaguzi endapo ataamua kuhama chama ama kugombea kama mgombea binafisi.

NAAMINI SITA ANAJUA KUWA HAKUNA NGUVU KUBWA KUSHINDA YA WANANCHI NA HATATAKA KUIPOTEZA,NA HIYO NGUVU YA NJE YA SITA NDIO IMEWAFANYA CCM WAAMUE BILA KUPENDA,WEWE UNADHANI KAMA MAKINDA ANGETAKIWA KWENDA KUPIGIWA KURA NA WANANCHI CCM WANGEMUACHA SITTA?WASINGEJARIBU MAANA WANGEANGUKA VIBAYA NA HATA MWAKANI NGUVU YA NJE NDO ITAWATISHA KULIKO YA NDANI,MBONA ALIPOKUWA SPIKA ALIKUWA HAOGOPI KULALAMIKIWA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…