Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,717
Binafsi ninaamini kuwa wapo watu wengi sana ndani ya Chama cha Chadema ambao ni 'smart' zaidi yangu lakini mara nyingi huwa nashangaa sana juu ya maamuzi wanayoyafanya na huwa na-question kama wamefanya mashauri ya kina.!
Katika 'movie' inayoendelea dodoma kuhusu utungaji wa katiba mpya, umeibuka mjadala hivi karibuni kuwa nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo. Makundi mbalimbali yametoa misimamo mbalimbali kuonyesha wanamtaka nani hasa kwa kuzingatia maslahi yao.! Katika mazingira haya ya 'kampeni' na 'kufagilia' nani awe Mwenyekiti wa kudumu nimeshangazwa sana kuona chama cha Chadema kikimuunga mkono wazi wazi Mhe. S. Sitta!! Watu wengi wameupigia debe uamuzi huu wa chadema lakini binafsi nimeshangazwa mno.. Kwanini??
Kwanza nianze kwa kukiri kuwa ni kweli tunatunga katiba ya watanzania wote, lakini pia ni lazima na ni wajibu wa kila kundi/kikundi kuwa makini kulinda maslahi yake ya kitaasisi na kisekta/nyanja katika ujumla wake.! Ninachomaanisha hapa ni nini? Ni dhahiri kuwa kila taasisi/nyanja/sekta iliyopo pale dodoma Bungeni ina maslahi inayojitahidi kuyapigania, hivyo inajitahidi kuangalia njia na mbinu mbalimbali ili kufanikisha hilo. Katika mbinu hizo ndipo chama cha Chadema kikaamua kuweka wazi msimamo wake wa kumpigia debe Mhe. S. Sitta ikidhani kuwa ni hatua ya kimkakati kufanikisha 'kupush' agenda wanazozipigania. Watu wengi sana wameipigia chapuo hatua hii, binafsi naamini Chadema wamepigwa goli dakika ya kwanza alafu wanashangilia! Ntafafanua;
i) CHADEMA HAIJAANGALIA MBALI
- katika siasa kuna mbinu huwa napenda kuiita 'acha wafu wazikane', naomba nielezee kidogo. Ndani ya CCM kulikuwa na makundi yanayosigana ambapo kila kundi lilikuwa na nia ya kusimamisha mtu wao, nikiyaorodhesha machache, kuna kundi lilitaka kumsimamisha chenge, wengine walitaka asimame Mama Migiro na kuna kundi na lingine lilimtaka Sitta! Huu mkanganyiko ndani ya CCM ulikuwa na uwezo wa ku-work on Chadema's favor kama wangeutumia vizuri. Kulikuwa na kila dalili ya kundi moja kulikwamisha kundi lingine ndani ya CCM wenyewe hili mtu wa kundi lingineisichukue nafasi ya uenyekiti. Kitendo cha Chadema kuonyesha upande waliopo uliwafanya CCM waungane na kuamua kumpitisha kwa makubalino maalum. (Kulinda maslahi ya chama) hivyo Chadema wasahau kuhusu Sitta kuwafanyia 'favor' zozote zile ndani ya bunge..
Chdema walipaswa wakae kimya katika ili, walitakiwa "kuwaacha wafu wazikane" ili wagawanyike na iwe rahisi kuwadhibiti
ii) CHADEMA wamekiri ni Dhaifu
Binafsi nimetafsiri kitendo cha Chadema kumpigia debe mtu wa CCM kama ni kitendo dhaifu na kuwa hawana ushawishi wowote ndani ya bunge. Hata kama wana idadi ndogo lakini walipaswa kujikakamua na kumuunga mkono mtu sahihi hata kama hatoshinda, hii ingetufanya tuwe na imani kuwa wako pale wanajua wanachokifanya..
iii) CHADEMA haijifunzi
Mwaka 2010, Chadema walimfuata Mhe. Sitta na kumuomba agombee urais kupitia chama chao!! Baada ya mazungumzo marefu Sitta 'akawachomolea' na wengi hata hawakulijua hili suala.
Jambo la kusikitisha mwaka Jana Mhe. Sitta akatokea hadharani na kusema kuwa chadema hakuna kiongozi ndio maana hata walidiriki kumfuata na kumpigia magoti agombee uraisi kupitia chama chao. Binafsi sielewi chadema inawezaje kumuamini mtu wa namna hii.
iv) CHADEMA imejitia pingu
Kama Sitta ataharibu (and am sure he will) sitegemei kusikia malalamiko kutoka chadema kwasababu wametumia nguvu nyingi sana kumpigia debe...