Bunge la Katiba litaanza wiki ijayo Mjini Dodoma. Rasimu ya Katiba ambayo kimsingi imetokana na mawazo yetu wananchi, inaonekana kutokuwa maarufu kwa CCM na mara kadhaa Viongozi waandamizi wa Chama hicho wamejitokeza waziwazi kupinga baadhi ya mapendekezo yaliyomo kwe Rasimu hiyo.
CCM walijitahidi kwa kutumia Wajumbe wao wa Mabaraza ya Katiba, walijaribu kuhakikisha kuwa wazo la Serikali tatu linaondolewa kwa kigezo ati Serikali tatu sio Sera ya CCM [walitaka Katiba ya CCM pekee kuhusu mfumo wa Muungano!] Hilo halikufanikiwa baada ya Tume kushikilia msimamo wa waliotoa maoni nchi nzima.
Baada ya jaribio la awali kushindwa, CCM wakaja na mkakati mwovu kabisa; kumpaka matope na kumkashifu Mwenyekiti wa Tume, Mzee Warioba. Kashfa na vijembe vilitolewa hata na watu wenye heshima kwenye jamii akiwamo Mdhamini wa CCM- Mzee Peter Kisumo aliyemtuhumu Mzee Warioba kuwa miongoni wa wale Wabunge wa G55 ambao miaka ya 90 walishinikiza kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika.
Kama hilo halitoshi, uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba unatia shaka kubwa baada ya kuwajaza wanasiasa wengi kwa maslahi ya Kisiasa badala ya maslahi na mustakabali ufaao wa Taifa letu. Mfano mzuri ni uteuzi wa Mzee Kingunge kupitia Kundi la NGOs!
Ombi langu kwa Wajumbe wa Bunge la Katiba, wakumbuke kuwa yaliyomo kwenye ni mawazo yetu wananchi, wasituyatupe na kuingiza sera za Vyama vyao vya siasa. Pia, wakumbuke kuwa tunaandika Katiba ya Nchi, na siyo Katiba ya CCM. Ni vema Wabunge wa Bunge la Katiba wajue kuwa wananchi hawajaipinga Rasimu hiyo ya Katiba kwa kuwa kimsingi wamekubaliana nayo na imebeba matumaini ya Wananchi walio wengi.
Nawasilisha.