Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Nimekuwa nikifuatilia mijadala katika bunge la Jamhuri ya Muungano na sasa Bunge maalumu la katiba kupitia TBC. Kitu ambacho mimi nimeona ni kasoro labda mpaka hapo nitakapoeleweshwa ni kile kitendo cha kuchelewa kuonesha picha wakati mbunge anapopewa nafasi ya kuzungumza. Utakuta mathalani mbunge kapewa nafasi ya kuzungumza sasa TBC badala ya kuanza kutuonesha mzungumzaji, wanaowanaonesha ukumbi mzima wa bunge muda mrefu kabla hawajaelekeza kamera kwa mzungumzaji. Sisi watazamaji tunapokuwa na hamu ya kumwona mzungumzaji wenyewe wanaonesha picha ya kukumbi mzima wa vunge kwa muda mrefu, halafu baadaye ndipo wanapomwonesha mzungumzaji, wakati mwingine mzungumzaji anakuwa amefika katikati ya uchangiaji wake au anapomalizia. Muda wote akizungumza tunasikia sauti lakini hatumwoni mzungumzaji badala yake tunaoneshwa watu wengine au ukumbi mzima wa bunge. Hata wakati wa kutambulisha watu au wajumbe mbali mbali TBC hawapo sharp kuelekeza kamera kule aliko mjumbe anayetambulishwa unakuta wakati mwingi mjumbe kasimama na kukaa bila kumwona. Mfano mzuri ni jana wakati wa mjadala wa bunge la katiba. Ilipofika wakati wa mwenyekiti kutambulisha viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo ambao walipendekezwa kuongoza maombi kabla ya kuanza majadiliano TBC hawakuwanesha ingawa walisimama. Tulichokiona ni picha nzima ya ukumbi mzima wa bunge lakini watambulishwa hawakuoneshwa wakati watazaji tukiwa na shauku ya kuwaona ili tuwafahamu. Mimi nadhani wangekuwa wanawahi kumwonesha mzungumzaji au mtu anayezungumziwa au kutambulishwa kisha wakazungusha kamera zao kwenye ukumbi kuchukua mapozi mbali mbali ya wasikilizaji badala ya kumwonesha mzungumzaji mwishoni au wakati amesha kaa. Au hata kama wataanza na matukio mengine isiwe muda mrefu sana kabla ya kumwonesha mzungumzaji kwani kwakweli wakati mwingine wanachosha!
Nimetafakari hili kwa muda mrefu nikahisi kuwa mojawapo ya sababu au zote inaweza kuwa labda wana kamera chache, au zinakuwa wrongly positioned, au uvivu na uelewa wa mchanganya picha na zaidi inaweza kuwa ni uvivu wa wachukua picha kuwahisha kuelekeza kamera kwa muongeaji au mahali kunapotokea tukio. Kama kuna maelezo ya kiufundi nitafurahi kuelimishwa.
Nimetafakari hili kwa muda mrefu nikahisi kuwa mojawapo ya sababu au zote inaweza kuwa labda wana kamera chache, au zinakuwa wrongly positioned, au uvivu na uelewa wa mchanganya picha na zaidi inaweza kuwa ni uvivu wa wachukua picha kuwahisha kuelekeza kamera kwa muongeaji au mahali kunapotokea tukio. Kama kuna maelezo ya kiufundi nitafurahi kuelimishwa.