Bunge la Katiba: Waandishi watimuliwa nje ya Ukumbi

Bunge la Katiba: Waandishi watimuliwa nje ya Ukumbi

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,750
Baada ya maajabu ya jana kuwafikia wananchi moja kwa moja na haswa lilipozuka suala la kura kutofautiana na idadi ,leokuna karatasi za rasimu za kanuni ziligawiwa ,ajabu karatasi hizo hazikutosha ,zilikwisha na wengine kukosa ,waliokosa ni wengi.
 
tulia basi uandike kitu kizuri, heading yako na ulichoandika haviendani
 
Natumaini kuwa kuna wabunge katika kikao hicho wanaweza kutueleza nini kinachoendelea.
 
tulia basi uandike kitu kizuri, heading yako na ulichoandika haviendani

Net ilikatika Mb zilikwisha nikawahi kupost ,ila habari za kuaminika waandishi wametimuliwa ndani ya ukumbi na haijulikani kama wataruhusiwa kuingia au kukaribia sehemu za ukumbi au watarudi tena.
 
Watanzania tusiwe wepesi wa kuansika tusiyoyajua. Mara waandishi watimuliwa, mara karatasi hazikutosha!
 
mbona bunge harirushwi hewani jioni hii au kunanini kinaendelea mjengoni?
 
tunaposema kuwa CCM ni wezi wa kura wengi hapa huwa awaamini hata kidogo,bunge waheshimiwa kura zinazidije?hapo ndipo mimi sielewi kabisa.
hii inaonyesha kuwa huku mashinani ndio huwa vinara wa kuchakachua matokeo
 
Net ilikatika Mb zilikwisha nikawahi kupost ,ila habari za kuaminika waandishi wametimuliwa ndani ya ukumbi na haijulikani kama wataruhusiwa kuingia au kukaribia sehemu za ukumbi au watarudi tena.

Net ilikatika baada ya kubonyeza kitufe cha 'post'? Poa mkuu tumekupata.
 
Yaan majibu yakizoea kuiba linaiba tu hata haya hakuna!!
 
Net ilikatika Mb zilikwisha nikawahi kupost ,ila habari za kuaminika waandishi wametimuliwa ndani ya ukumbi na haijulikani kama wataruhusiwa kuingia au kukaribia sehemu za ukumbi au watarudi tena.
Aliyewatimua nani, Pandu Omar Ramadhan Kificho?
 
Ukandamizaji wa uhuru wa habari. Rasimu ya Katiba mpya inasemaje kuhusu hili? Media mna wawakilishi huko kwenye katiba mpya bungeni?? Nchi hii ni kiboko.
 
Hiyo net yako ni kiboko! Iliku-alert kwamba upost kwanza then ukiongeza MB ndo uendelee? Mtandao gani huo watumia yakhe!
 
Kwa mujibu wa EATV hot mix jioni hii ni kuwa waandishi wote wametimuliwa bungeni,na hiyo ni baada ya kugawa rasimu ya kanunu ambazo hazikutosha hata nusu ya wabunge wa bunge la katiba. Hivi ni kweli serikali hii ya ccm ina nia ya kuleta katibatmpya?
 
Habari ndio hio ,yaani mambo yanaendeshwa kienyeji ,sijui kama hawataunda kamati kuchunguza kwa nini makaburasha hayakutosha ,au jamaa ameshakula hela ,hivi wanakosea kulipana posho ?
 
Net ilikatika Mb zilikwisha nikawahi kupost ,ila habari za kuaminika waandishi wametimuliwa ndani ya ukumbi na haijulikani kama wataruhusiwa kuingia au kukaribia sehemu za ukumbi au watarudi tena.

Ndg mbona unaandika km unawahi Toilete vp? Sema ueleweke waandishi wamezuiliwa nn 7bu?
 
hivi wakati wanazalisha nakala za hayo makabrasha ya rasimu ya kanuni za kuendesha bunge la katiba hawakujua idadi kamili ya wajumbe wote wa bunge la katiba? we should learn how to organize things properly here in Tanzania.
 
Back
Top Bottom