hivi wewe huu uwazi wa ccm umeanza lini?, uwazi huu ulitakiwa kuanzia kwenye mikataba mibovu, kashifa ya EPA na kufichwa kwa balali, kashifa ya richmond, watu wanaohusika na kukata kucha za watu, wizi wa fedha za umma n.k., usikurupuke na kufikiri wananchi hatukumbuki haya yote, tunayajua na tunajua siku moja lazima yapate majibu. harafu wewe hujui kitu kaa utulie, angalia na ujifunze. lengo la ccm ni kutaka kuwadhibiti wale wote walioteuliwa na ccm ikiwemo wabunge wake ili watekeleze matakwa ya ccm na sio matakwa ya watanzania. kama unakumbuka vizuri tuliambiwa kuwa wale wote waliokuwa wanarudisha fedha za EPA wangekamatwa baada ya kurudisha, wako wapi?. hii ndiyo serikali pekee duniani ambayo mwizi anaombwa na kubembelezwa arudishe fedha za umma na kusamehewa.