But I'm sure the issue beteween Raila, Ruto and Ongeri will emerge somewhere on the move.
That issue mkuu is a done deal. Raila na Ruto hawapatani hata kwa suluhu ya
upanga maana their paths are totally different. Raila ashaonyesha kua hana time
na mafisadi ambao wamejaa katika hii seriklai ya Kibaki. Kibaki naye anajulikana
wazi kua ni mfisadi papa na anaonyesha live ndo maana aliwarudishia hawa
mawaziri nyadhifa zao licha ya kwamba kuna shuku na jinsi hela ilivyopotea
katika ofisi zao.
Kwa sasa Ruto amejiunga na wabunge wa kambi ya Kibaki ambao wanataka
kumpiga Raila vita ndani ya Bunge. Kuna mswada f'lani walitaka kuuleta bungeni
kuhusu kutokua na imani na Waziri Mkuu. Kisha kuna ile nafasi ya leader of
Government Business ndani ya Bunge ambapo kuna stalemate kati ya Raila na
Kalonzo Musyoka (muwakilishi wa PNU). Kulingana na vyanzo vyangu, miswada
yote miwili itapigwa chini. Tusubiri tuone.
Kisha ishu kuu walionayo hawa wabunge hata hivyo ni kuwapatia wakenya katiba
mpya ambayo ukiniuliza mimi nitakwambia hamna upya wowote ni ile ya zamani.
Siasa za Kenya zitakua za kusisimua katika miezi ijayo mitatu maana kuna viti viwili
vya wabunge ambavyo vitapigiwa kura.
Bw. Omino Magara (ODM) alipoteza kiti
mitaa ya Kisii baada ya petition kutokea mgombea mmja. Naye
Bw. Chirau Makwere (PNU)
alipoteza kiti chake baada ya malalamishi kutoka mpigia kura mmoja aliyelalamika
mahakamani kua jamaa hakushinda kihalali. Alitoa sababu zake na mahakama
ikamsikiza.Tunasubiri firimbi kutoka Spika wa Bunge.