Bunge la Kenya lapitisha mkataba wa EPA

Bunge la Kenya lapitisha mkataba wa EPA

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,440
Reaction score
8,149
Wakati nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zikiwa zimejipa muda kutafakari Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Jumuiya ya Ulaya, Bunge la Kenya limepitisha uamuzi wa kusaini mkataba huo.

Katika kikao cha dharura kilichofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 9, wakuu wa nchi zinazounda EAC waliamua kujipa muda wa miezi mitatu kutafakari kwa kina makubaliano hayo, yanayoitwa EAC-EU Economic Partnership Agreements(Epa), kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.

Gazeti la Daily Nation limeripoti kuwa makubaliano hayo yamepitishwa na Bunge.

Kenya, inayozisukuma nchi nyingine za jumuiya kusaini makubaliano hayo ambayo, miongoni mwa vipengele vyake yanaruhusu bidhaa kutoka nchi wanachama wa EU kuingia bila ya ushuru, iliitisha kikao cha dharura cha Bunge kwa ajili ya kujadili suala hilo jana.
 
Kenya wamejipima wameona ina maslahi kwao wameipitisha.

ngoja wao waendelee, sisi wazee wa kudesa tutadesa huko mbele kama kwao italipa.
 
Kenya wamejipima wameona ina maslahi kwao wameipitisha.

ngoja wao waendelee, sisi wazee wa kudesa tutadesa huko mbele kama kwao italipa.

Tanzania ijitoe kwenye yale makubaliano ya ushuru wa forodha ya Afrika mashariki tuendelee na mambo yetu.Vitu vikiingia nchini toka Kenya vichajiwe ushuru kama vimetoka ulaya.Sababu kenya yaweza tumika kama uchochoro wa bidhaa za ulaya kupenya nchini kwetu kupitia makubaliano ya ushuru wa forodha vikaingia kuja kuua bidhaa na viwanda vyetu.
 
EPA inaonekana ni mkataba wa kizimwi kwa sababu hatuna cha kuuza EU! Kutokuwa na cha kuuza huku si kwamba ni kilema tulichopewa na Mwenyezi Mungu na hivyo hatuna namna bali kunatokana na kilema cha kushindwa kutumia akili tuliyonayo!! Kutokuwa na cha kuuza huku si kwa sababu tumeambiwa nyie Waafrika Manyani hamna cha kutuuzia bali ni kwa sababu sisi wenyewe tumekosa kutumia raslimali tulizonazo na kuwa na cha kuuza!!! Ni ajabu, aibu na inachukiza kusikia nchi yenye ardhi yenye rutuba kila mahali; nchi yenye virgin land lakini bado haina cha kuuza kwenye eneo la kiuchumi ambalo halina ardhi ya kutosha! Inakera na kuchukiza, hata baada ya miaka 50 ya uhuru wapo watu watakuja hapa na kudai hakuna ushindani huru kv nchi za Ulaya zinatokuwa ruzuku kwa wakulima wao!!

Go Kenya go cuz' you don't wanna hide yourself in these stupid African justifications! You need EU to sell your horticultural products; sisi hatuna haraka... nyie tangualieni tu kwa hao manyan'gau wenzenu...!!!
 
Tanzania ijitoe kwenye yale makubaliano ya ushuru wa forodha ya Afrika mashariki tuendelee na mambo yetu.Vitu vikiingia nchini toka Kenya vichajiwe ushuru kama vimetoka ulaya.Sababu kenya yaweza tumika kama uchochoro wa bidhaa za ulaya kupenya nchini kwetu kupitia makubaliano ya ushuru wa forodha vikaingia kuja kuua bidhaa na viwanda vyetu.

tusign tu make bakhesa atakuwa anauza juisi zake ulaya kiulaini
 
Wakenya lazima wapitishe maana wana bidhaa nyingi sana za kuziuza EU
 
Kama zipi hizo zamaana zaidi ya maua ndio yanayokwenda kule.kama maziwa ulaya EU wanamaziwa yakutosha tu na high quality
 
Kenya wamejipima wameona ina maslahi kwao wameipitisha.

ngoja wao waendelee, sisi wazee wa kudesa tutadesa huko mbele kama kwao italipa.
Kenya wana monopoly kubwa sana ktk soko la maua na tanzanite (zetu)! kwa hiyo kwao EPA ni fursa kubwa sana, sisi hapa hatuna cha kuuza ulaya, tuwaache wajitafutie riziki sisi tupige siasa! Kuwafanya wasubiri mpaka januari, watakuwa time barred, hawawezi kukubali hususani tukizingatia kwamba Rais Uhuru mwenyewe ana interest kubwa sana kwenye soko la maua
 
nilikua naangalia bunge jana.... mbunge mmoja alisema asilimia 40 ya bidhaa zote ambayo kenya inauza nje inaenda EU.... hio 40% ni wafanyikazi millioni nne ambao wameajirika kutokana na hio 40%....

kwahivyo tukishindwa kuingia kwa huo mkataba kama eac, bidhaa za kenya zitalipishwa kodi, jambo ambalo litafanya ziwe bei ghali na zishindwe kushindana na bidhaa za nchi nyengine....kufanya kampuni zi filisike....kwahivyo hio ni guarantee watu millioni 4 watakosa kazi.....
 
This agreement will allow EU ships docking at the port to receive service promoting our ship building industry

Istoshe itapea KQ more revenue

Boost our flower exports

And clothes to the EU

it will reduce costs ya farm equipment and more herbicides and pesticides

Allow EU agents to open shop in kenya for uptake and export of our products and vice versa

Nk...kuna vitu vingi

Fyi kenya is classified as a middle income country the rest of EA ni least developed country so this deal is God sent ......
 
So the deal is viable for kenya only,
What is Tz & ug going to get out of it??
 
Tanzania hatuwezi sign hilo deal kwa kuwa bado tuna dosa dosa kiuchumi wa viwanda hatutaki kuwa jalala la bidhaa za wengine
 
So the deal is viable for kenya only,
What is Tz & ug going to get out of it??
growing at a avg rate of 7%, you wont stay LCD for ever.... also the other deal which exists is not liberalised as the EPA, they say you can export stuff to them, but in reality, you can never meet their hidden restrictions.... in the EPA, we can export anything we can affored to export and compete with their own products hata kama tutakua na market share ya 0.6% bado tutauza hata vijiti vya kupigia meno ile watu wa mashambani hutumia kama toothbrush (it cleans better than an average brush).....
 
This agreement will allow EU ships docking at the port to receive service promoting our ship building industry

Istoshe itapea KQ more revenue

Boost our flower exports

And clothes to the EU

it will reduce costs ya farm equipment and more herbicides and pesticides

Allow EU agents to open shop in kenya for uptake and export of our products and vice versa

Nk...kuna vitu vingi

Fyi kenya is classified as a middle income country the rest of EA ni least developed country so this deal is God sent ......
Thats Kenya. How about Tanzania?
 
Hizi ni sarakasi za siasa tu, Kenya tayari walikuwa wameshatia saini huo mkataba kwa hiyo kuupeleka bungeni kwa sasa bila ya kupata saini za nchi nyingine za EAC ni kupoteza tu kodi ya wananchi wa Kenya.
 
Mkuu,
Kweli kabisa manake Kenya hujiona kama ndiyo ''Afrika Mashariki yote'' kama ilivyo Mareakani wakisema ''The world'' wanamaanisha Marekani, angalau Marekani ana ubavu wa kulazimisha mambo duniani lakini siyo Kenya hata kikanda ubavu huo hawana.
 
Back
Top Bottom