Maria space limesaidia kutoa elimu kwa jamii ya Tanzania . Nchi hii ambayo ni masikini sana kutokana na sheria mbovu na rushwa kubwa serikalini ina tatizo kubwa la mfumo. Maria Space linapigania jitihada za kuikomboa Tanzania kwa kuwa na katiba mpya. Kitu cha kushangaza salama utaifa na machawa walienda mpaka Kenya kwa kutaka kumteka huyu Mdada sasa kama hana kitu cha maana kwanini wanataka kumteka. Dr Slaa anashikiliwa kwasababu alikuwa anasema mambo ambayo serikali haikupenda Maria Space. Unatakiwa uende na kusikiza hoja kwanini Tanzania ni masikini mpaka leo. Tukiendelea na uchawa, kusifia sifia, ufisadi wa hali hii na wizi wa kura kama nchi hatutafika na hii nchi itakuwa ya kisultani. Bunge lililopo Dodoma ambalo wabunge wamepatikana kwa wizi wa kura kwa kusaidiwa na Polisi na Usalama hakuna mtu mwenye akizi zake anafikiri litatusaidia kama nchi. Vuguvugu la katiba tumshukuru sana Maria space. Lissu kuwa mwenyekiti wa Chadema tumshukuru sana Maria Space.
Kama mnaona hafanyi kitu endeleeni na machawa Dodoma lakini Watanzania wengi wasomi wanajua kinachoendelea inawezekana kabisa kwa upeo wako unafikiria kula na kunya tu sisi tunafikira Tanzania sio mtu.Tatizo kubwa ni katiba na tutaanza na mijadala ya kisomi Maria Space