Mzee we ni mgeni wa mateso ya nchi hiiSio Bunge tu serikali nayo haitaki kufanya maamuzi kwa jambo lolote linalowaumiza wananchi yaani ni kama vile serikali imebariki wananchi kuteseka.
Hakuna Bunge ni Vikao vyao vya ndani vya CCM Bunge gani Linashindwa kuwachukulia HATUA Wapigaji wa Fedha za Umma kama Report ya CAG ilivyowabainisha ?Wabunge wa bunge la sasa wengi ni walalamishi na washabiki badala ya kuwa viongozi. Sasa bei ya mafuta mnataka Raisi afanyaje kama bunge lenyewe haliwezi kukata kodi. Kukata kodi inabidi mkate na budget! Sasa mnataka mishahara iongezeke, kodi ipunguzwe , miradi imalizike na Mama asikope sasa inawezekana vipi!
Wabunge ni lazima wawe wawazi sio kuaminisha wananchi uongo. Wananchi wamejifunza ubaya wa kuwa na bunge fake kama hili