winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 379
- 603
Mh. Spika napenda kutoa hoja kama ifuatavyo:
Kwanza kabisa Mh. tumeona na kushuhudia ni kwa namna gani mtandao (internet) umeleta mageuzi makubwa kibiashara na kijamii na hivyo kufanya ubadili uti wa mgongo wetu wa Taifa kutoka "kilimo" na kuwa "biashara-mtandaoni".
Vijana wengi sasa wamejiajiri na biashara ndogondogo na kubwa na wanapotumia mitandao ya kijamii kama vile Whatsapp, Instagram, youtube na facebook wanawafikia wateja wengi na kusababisha faida kuwa kubwa mara dufu ya ile ambavyo wangepata kwa kuuza kwenye eneo dogo walilopo. Tumeona pia wengi wamevumbua mitandoa mizuri kama vile www.jamiiforums.live na mingine ambapo ingepata baraka za serikali ingesababisha ujira mwingi na kuifanya Tanzania kuwa matajiri zaidi ya maskini.
Serikali imeweka zaidi laana katika mitandao "interent products" kuliko baraka hivyo kufifisha nia ya wengi wenye ndoto za kuibuka kitaifa na kimataifa kukata tamaa na kuishia kutafuta ajira ilimradi aweze kudumu mahitaji yake ya siku huku ndoto zao zikifa kabisa. Vijana wengi wanasomea "computer science" lakini wakija mtaani hawana ajira na hawapati urahisi wa kufanya yaliyo katika ndoto zao.
Waheshimiwa wabunge la jamuhuri ya mtandaoni mimi mwenyewe ni mfaidika wa mitandano mbalimbali ikiwa bidhaa zangu nyingi nimeagiza sehemu mbalimbali yaani ndani ya nchi na nje ya nchi, hivyo nimeonja utamu wa biashara mtandaoni kwani unapata bidhaa zenye ubora na chaguo lako linakuwa pana zaidi " wide option"
Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi. Je, serikali haioni umuhimu wa kupitia upia sheria za mtandaoni na kuzifanya ziwe nafuu na zenye kumuezesha kijana mjasiriamali, ambae hana mtaji wa kifedha bali mwenye mtaji wa NIA na NDOTO kuweza kufanya makubwa na hatimae kupata matajiri wenye uwezo wa kuajiri wengine? Tumeona sheria nyingi za mtandao zilivyokandamizi na zenye makali dhidi ya vijana wenye ndoto zao za kuwa mabilionea kama ilivyo kwa akina: -
Watawala wetu wameamua kuweka sheria ngumu za mtandaoni kwasababu ya matusi ya vijana wawili watatu lakini hawakufikiria kwamba kuna vijana mamilioni kwa mamilioni wenye uchu na uwezo mkubwa wa kutimiza ndoto zao kwenye mitandano mbalimbali ikiwemo ya kuanzisha wao wenyewe na ile ambayo tayari imekwisha anzishwa. Ni kweli katika mtandao wapo wanautukuna wakubwa lakini haikufanyika tathmini yakinifu kujua ni kwa idadi gani ukilinganisha na wale wenye faida katika taifa letu. Watawala wametishwa na kivuli chao wenyewe na hivyo wakaboa nyumba nzima kwa kuhoghofia mambo yasiyokuwepo.
Ukijumlisha sheria za mtandaoni, vile vile kuna sheria nyingi mno ambazo zimetungwa kimuhemko na kwa kuzingatia utashi na hisia za mtu au kundi la watu wachache na hijazingatia maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla. Nichukue nafasi hii kuwaomba waheshimiwa wa bunge la jamuhuri ya mtandaoni kuziweka hapa wazi na kuwaomba watawala wazipitie upya ili ziweze kuwanufaisha watanzania na sio kuwarudisha miaka 100 nyuma.
PIA NIKUMBUSHIE HOJA YANGU YA SIKU ZOTE HAPA HAPA MAANA DAKIKA ZANGU HAZIJAKWISHA.
Mkopo tumepata Benki ya Mendeleo ya Afrika, Sheria na kanuni za mikataba tumezitengeneza sisi, temetangaza sisi hizo zabuni, tumezifanyia uchambuzi sisi, lakini cha kushangaza zote tumewapa wachina kuanzia makandarasi mpaka wasimizi wa miradi wametoka nje ya Taifa letu pendwa la Tanzania. Na hawa wachina wakija wanakuja na kila kitu kuanzia ndala mpaka "dawa ya meno" wakija wanakuja na vibarua wao, halafu sisi tunabaki kuwa walinzi getini na wafigizi kwenye vyumba vyao. Tafadhali naomba mliopo kwenye ngazi za maamuzi angalie hili upya na kwa usirizi wa hali ya juu.
Je, hatuna kabisa uwezo wa kujenga barabara zetu kwa kutumia wakandarasi wetu hata kwa zile pesa zinazotokana walipa kodi wetu? Je, serikali imechukua hatua gani kuwawezesha wazawa kuwa wakandarasi bora kwa tunga sheria madhubuti na kuzisimamia kikamilifu? Imeshindwa kabisa kuweka sheria na kanuni za kuwafanya watanzaia waweze kuijenga nchi yao wenyewe mpaka wachina kila uchao wao pekee ndio wanaopata tenda kubwa kubwa hadi zile zinazotokana na pesa zetu wenyewe?
Sasa swali gumu kuliko yote tunasomesha Civil Engineers wa nini? Tunasomesha Quantity saveyors wa nini? Je, tunawasomesha kuwa walinzi wa wachina? Au tunasomesha vijana wetu wa kike na kiume kuja kuwa vibarua wa wafanyabiashara wa nje? Tuach chuki chini na tuiunganishe Taifa letu tuweke nguvu moja kujengea uwez watoto wetu ambao kesho tukizekee tunawategema wao.
Siku zote kumekuwepo na kisingizio kwamba mbongo ni mwizi, mbongo ni mbabaishaji, mbongo haeleweki, mbongo hana uwezo. Hii yote ni hadithi za ALFU LELA U LELA ambaozo hazitatupeleka popote kwani tukiamua kusimamiana kikamilifu tunaweza na zaidi sana tutafanya mzunguko wa pesa kuwa mkubwa ndani ya nchi yetu. Wewe unampa mchina tenda zote zinazoifanya bajeti ya nchi kwa silimia zaidi ya 50% kisha utegemee mzunguko wa pesa uwepo ndani ya taifa lako. Hizo ni ndoto za abunuasi na uvivu wa kufikiri.
Kinaniuma sana kuona hata wabunge wakiwa bungunie wanajadili vitu "personal" badala ya kuwa wazalendo na kujadili namna bora ya kufanya Tanzani iendelee.
Najua usalama wa Taifa mpo humu pomoja na kila shushu, chukueni hizi hoja muhimu na mzifikishe kwa mabosi wenu kwa unyenyekevu maana kesho mabinti zenu watakua malaya wa wachina pamoja na "wawekezaji" hili hali vijana wenu wa kiume wakibakia walinzi wa kulinda mali za "wawekezaji" na kubakia maskini zote.

- Pierre Omidyar.
- Eric Schmidt.
- Jeff Bezos.
- Sergey Brin.
- Larry Page.
- Mark Zerkback