Bunge lajadili malori kukwama bandarini

Mkuu unamlaumu JPM bure. JPM alifanya mambo yaende kwasababu anajua kusimamia mambo. JPM aliisafisha sana Bandari. Kuongoza watu wa nchi hii si kazi ndogo. Hata uje na sheria nzuri kama huna msimamizi nchi hii kazi bure. Kipindi cha JPM urasimu ulipungua mno. Namkumbuka JK siku moja alisema msibani kwa JPM, " Watu wale wa Ardhi ni wagumu balaa". Kama Rais mstaafu anajua. Mzee Mwinyi (Mheshimiwa) alishawahi sema ilivyo ngumu kuleta nidhamu serikalini. Hata Mheshimiwa Mbowe angekuwa Rais angekumbana na hayo. Nadhani Mindset zetu au tamaduni zimetuathiri kimtindo na pia hatuna institution kali za kuwajibishana. Mimi Hayati JPM bila kumumunya Maneno alijitahidi sana na hili la Malori ungesikia mziki wake. Watu wengi hufanya kazi kwa kuogopa kupoteza kazi, wakiachwa wanazoea na kubweteka. Makampuni Private hasa ya nje huwa hayana woga kumtimua mtu akiwa mzembe ndiyo maana watu huwa wana nidhamu. PM akazane pia katika hili.
 
Waziri Mkuu anatakiwa asaidiwe maana kila mara anatembelea bandari lakini hakuna mabadiliko ya utendaji yanayoonekana
 
Hilo tukio hilo lilikuwa maigizo tu. Badala ya kupoteza dk 20 'kujadili' Jenista angeambiwa atoe taarifa yake yaishe. Kwani Tulia alikuwa hajui PM amekwenda Dar?
Hapo ujue huenda kuna jambo lilikuwa linafunikwa kwa kuzua mjadala mpya wa "maroli!!"
 
Hapo ujue huenda kuna jambo lilikuwa linafunikwa kwa kuzua mjadala mpya wa "maroli!!"
Ewaaah! Haiingii akilini PM aondoke eti Spika na naibu, hawajui.
Spin hiyo, kipo wanatufanyia hawa hujuma. TRA kila mara imekuwa kawaida SANA, system down, leo iimekuwa dharura izungumzwe bungeni.

Wanataka kumhujumu mama Rais.
Mizigo kukwama kisa system, ni kawaida SANA hapo bandarini, hata enzi za mwendazake.
Washaanza KOMEDI SHOO

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hakuna bunge hapo, ni Halmashauri Kuu ya ccm in disguise.
 
Cosato Chumi unatuwakilisha vizuri sana wana Mkwawa High School wenzio.

Wewe ni product nzuri ya Makanyagio Casino kabla haijawa University.
Kwenye siasa kila kitu huwa na motive.. Ukifuatilia sana utakutana na figisu za kina Kakoko humo!
 
Naam huu ndio unaweza kuwa ukweli wenyewe...
Na tusubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…