Bunge lakanusha tuhuma za Paul Makonda kuhusika na wizi wa simu bungeni

Jabirimakame

Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
71
Reaction score
37
Kitengo cha ulinzi na usalama cha Bunge kimetoa taarifa ya kukanusha, tuhuma zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zikimhusisha Mbunge wa Bunge maalumu la Katiba ndugu Paul Makonda kuhusika na wizi wa simu ya Mjumbe wa Bunge la Katiba. Akitoa taarifa hiyo mbele ya Bunge maalumu la katiba, Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalumu, Mh. Pandu Amiri Kificho alisema;

 
Vijana wa bavicha akili zao ni za viroba na gongo. Ndio walileta huo umbea hapa JF.
 
leo ndio wanatoa taarifa ya kukanusha wakati watu walishambiwa vinginevyo
 
je simu iliibiwa au la? na kama iliibiwa je tufikiri kuwa kuna kibaka kutoka kinondoni au unga limited ndiye aliyekwenda kuikwapua huko ndani ya bunge?? na hii ni taarifa ya pili ya wizi ndani ya ukumbi huo wa bunge maalum la katiba!! ila taarifa ya kwanza haikutolewa ufafanuzi wowote,, basi tunaomba tu mtwambie kuwa huyo kibaka wenu (wa ndani ya bunge) kesha kanywa na kudhibitiwa ili asifanye vitendo kama hivyo tena,au tusubirie katiba ya vibaka.
 
Tumeelewa.Lakini,simu imeshapatikana? Mwizi aliyetoka nje ya Bunge amejulikana?
 
Vijana wa bavicha akili zao ni za viroba na gongo. Ndio walileta huo umbea hapa JF.

wewe akiri zako ni za nini za kupumuliwa siyo? Msalani alisapoti habari hiyo wewe unakuja kudandia Bavicha ndo mlivo kalilishwa et eee!
 
Upuuzi mtupu, nilitegemea agesema kuwa simu imepatikana. Na kama imepatikana ni kwa njia ipi? Why hakutangaza hilo?

Aliposema simu imepotea alitegema nini? Vipi imepatikana?

Nani alikuwa karibu na mpoteza simu? Zaidi ya Makonda?

Mwizi ni mwizi tu mnampoza ki utu uzima, vipi na kashfa zake za kipindi cha nyuma?

OK cctv za ukumbini, zinaonyesha nini?

Wazee wengine wa hovyo sana!
 
Vijana wa bavicha akili zao ni za viroba na gongo. Ndio walileta huo umbea hapa JF.

Kama ni umbea Simu imepatikana? Je ni kwa nini wamechelewa kukanusha wakati habari hii ipo tangu jana asubuhi.
 
Vijana wa bavicha akili zao ni za viroba na gongo. Ndio walileta huo umbea hapa JF.
Vipi imepatikana? Cctv za bungeni zimeonyesha ni nani?

Chenge wakati anawanga bungeni kwa kumwaga unga alionekana, why not Paul Makonda?

Namsubiri akanushe yeye kwa mdomo wake... tumwage ushahidi hapa!

Simu ipo wapi Makonda!?
 
Kama ni umbea Simu imepatikana? Je ni kwa nini wamechelewa kukanusha wakati habari hii ipo tangu jana asubuhi.

Hebu soma taarifa vizuri wewe, acha kukurupuka na kupayuka hovyo.
 
watoto wa bavicha punguzeni umbea,.hili ni jukwaa la elimu katika siasa na sio umbea.
 
Mwambie kwa mwanahabari makini, kupotea kwa simu bungeni kwa mazingira tata, hiyo ni habari?

Kwa nini alitangaza?
 
Magamba hivi walishayavua au walisafishwa na tuhuma ili wawe safi ilihali wachafu?
 
Lisemwalo lipo na kama halipo linakuja. Kwanini asingiziwe yeye wakati wajumbe wapo wengi?
 
Wazee wengine hovyo sana,hivi yeye si ndio alileta umbea kwanza simu imeibwa?jirani ni makonda sasa kairudisha au ndio tuamini ukoo wa panya unalindana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…