Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanabodi,
Nimekuwa nikifuatilia kikao cha Bunge asubuhi hii live kupitia TBC, mara ghafla matangazo yakakatishwa ghafla, TBC kwanza wakaweka promos na baadaye documentary ya underwater.
Kwanza nilidhani ni technical problem ya TBC, nikahamia Star TV ili niendelee na Bunge maana na wao huwa wanarusha live, nikakuta nil.
Ndipo nilipododosa toka source fulani Bungeni akaniambia Bunge limeahirishwa ghafla for technical problem.
Vyombo vyetu vya habari lazima viwatendee haki wateja wake kwa kuwanotify something, the usual one ni ile excuse ya kawaida
" Tunawaomba radhi watazamaji wetu, hatutaweza kuendelea na matangazo haya kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, asanteni"
Hii ingetosha, hili la kukatisha tuu matangazo, no excuse ni a bit rude!
Mimi sijaelewa..................bunge limehairishwa au ma-TV yameharibika..????
Ngalikihinja, liliahirishwa kwa muda kutokana na hitilafu ya virekodi sauti vya Bunge na sio camera, likaendelea ukumbi wa Msekwa ambako hakuna camera set-up, hivyo liliendelea bila kuonekana live, lets hope saa 10 hii, litaendela salama.
Kumbe wanatosha na kuna vyombo vinavyohitajika kwenye ukumbi wa zamani? Sasa mpya ulijengwa kwa ajili gani yarabi katika nchi 'maskini' kama yetu? Kama huo si ufujaji wa mali za umma, ni nini?
Tunadumisha mila zetu bwana.
Rahisi sana kulaumu wengine lakini tujiulize kwenye kila wabongo 10 ni wangapi wana fire extinguisher kwenye makazi yao? Au kwenye wabongo wenye majumba yenye thamani ya mil. 300 kuendelea wangapi wana bima?
Ukipata haya majibu rudi uwaseme bunge na plan B, a.k.a DRP/BCP.
Hili ndio swali la hekima.. sasa najua tunaweza kuwa na Bicameral House.. tuwe na Wabunge na Maseneta.. kumbe kumbi zote mbili zinaweza kutumika... Najua wamekuwa wakiutumia huo wa Msekwa kwa semina n.k na uko updated.. now we have a reason to reduce MPS from 323 hadi 200 tu halafu tuchague maseneta 50 hivi..