Tatizo lako unapenda ligi zisizo na miguu na kichwa ,lawachezaji linatokezea wapi? kifupi chansi zilitokea mimi kama mtanzania nikiwapigia debe wazangu waje wasakate kabumbu lakini ndivyo hivyo tena.
Sijakwambia nimefanya kazi alcatel ila nimeitwa kwenye interview tena nikiwa mwanafunzi na kazi yenyewe zilikuwa zinastate experience miaka mitano.
Ungekuwa wewe ungesema nimetowa rushwa teh teh teh teh kwa sababu tu udsm wamebwagwa.
Waitweje kwenye shortlist kama hao jamaa wa AUG wameshaonyesha wanatisha ktk CV.
kwa mfano.
Ngoja nikupe siri moja wale jamaa wanaofanya usaili ukishaweka tu sijui umesoma chuo gani 90% umeshamwagwa.Na ukiweka sijui ma vyeti yako nayo unaongeza 9% zinakuwa zimefika 99% za kumwagwa.
Mwezako anakuwekea tu mimi nina first digrii ktk uandishi wa habari bila kutia mbwembwe nyingi. Huyooo yupo ktk shortlist.
MKAMAP.
Hakuna cv unaweza kuandika bila kutaja chuo ulichosoma, mimi sijawahi kusikia labda wewe ulipoomba kazi huko ALCATEL.Obama asingetaja wapi kasoma lakini kila mtu anajua HARVARD.kutaja chuo ni jambo la wajibu kwenye CV inaonekana hata CV kwako ni mtihani.
Sema utakavyo lakini huwezi kufananisha status ya Udsm na Nyegezi.kwenye ajira HR lazima azingatie ubora wa chuo alichosoma muombaji.
Haiwezekani mtu aliyesoma Udsm akafundishwa Accounting na DR.Assad akawa sawa na mwanafunzi aliyemaliza nyegezi akafundishwa na kijana aliyehitimu hapo akapata First class akabakizwa kuwa mhadhiri.
Ubora wa chuo unatizamwa kwenye mambo mengi kama tafiti n.k na hivi vyuo vipya vina matatizo mengi kuanzia library,walimu n.k huwezi kusema mtu aliyesoma medicine KAIRUKI atakuwa sawa na mtu aliyesoma medicine MUHIMBILI university, wa muhimbili ana walimu na ana hospital ya rufaa yenye madaktari mabingwa, Muhimbili ina link na university au taasisi mbali mbali duniani.
Mhadhiri wa Kairuki atakuwa ni part time akitoka kufundisha muhimbili then aingie wodini halafu ndio aende Kairuki.kuna masomo hayafundishwi jioni kama Bio chemistry n.k
maktaba ya Udsm ina past papers toka 70s jee Nyegezi watakuwa na vitu kama hivyo?
Oxford University haiwezi kuwa sawa na Makelele university,mtu aliyesoma Oxford atakuwa na exposure kubwa kwa kusoma na watu tofauti tofauti na facilities za chuo ni advantages kwake,ubora wa wahadhiri, research zilizofanywa n.k si sawa na Makelele,
pia mtu wa Udsm atakuwa na exposure kubwa kuliko wa Nyegezi.Obama kusoma Harvard digrii ya sheria hatokuwa sawa na Mwakipesile aliyesoma law Tumaini university,Obama atakuwa amekutana na watu wa mataifa mbali mbali akiwa Harvard,Mwakipesile atakuwa na watu wanaofanana nae tu. kuna on line journals mbali mbali ambazo Harvard itakuwa inazo.ambako Tumaini hakutakuwa na facilities kama hizo.
Mkamap akija DR.slaa,DR.Nchimbi,DR,Kamala,dr.Nagu na PhD zao ambao wamesoma vyuo zisivyotambulika halafu akaja DR.Kawambwa shukuru,Dr.Mwakyembe,Professor Lipumbana DR.batilda Burian utawaweka pamoja bila kuona ubora wa vyuo walivyosoma?nikupe namba za wachezaji uwapeleke ulaya?