Bunge lakumbwa na kashfa nzito

Bunge lakumbwa na kashfa nzito

Sipingi darasa zima kuitwa kwenye interview ila kama wana MERITS au sifa husika cha ajabu creteria zilizowekwa za kuomba kazi hiyo hawana kama uzoefu wa miaka miwili.Nyegezi haiwezi kuifikia UDsm HATA iwe vipi?fuatilia UNIVERSITY LEAGUE TABLE kwa Africa utaona Udsm ina nafasi gani na Nyegezi hakuna anayeijua.
NYEGEZI haiwezi kupambana na Tumaini acha Udsm.labda ijipime na Kairuki au Bukoba University.

Wenda unatatizo ambalo halieleweki kumbe tatizo lako ni kwasababu tu udsm iko juu ya hicho chuo?
Haya mfano wapo wahitimu wa HAVARD 5 waameapply kazi na wewe mhitimu wa udsm na wakiitwa wahitimu wa udsm waachw wa havard basi inakuwa ndivyo sivyo kutokana na mtazamo wako??Pole sana
 
acheni kulalama kazi nyingine specified..kwenye hanard laazima waweke mtu wao.....hao waliokuwa shortlisted mnawafahamu vema?????????????

try next time...when one dooor is closed many more are open!
 
..st augustine ipo rwanda na kenya?..wahitimu hao ni watanzania????...sasa lazima watu wa UD ...ambako wengi tumepita mjuwe soko la ajira sasa lina ..mzumbe,dodoma,stjohn,augustine,Tumaini,kairuki,IFM, arusha,.meru,muslim...st.joseph,dar tech...etc

NIMEONGEA NA WAAJIRI WENGI ...WANASEMA WAHITIMU WA VYUO VINGINE ...WANAJIANDAA VEMA ZAIDI KWA INTERVIEWS NA MARA NYINGI HUWAZIDI WATOTO WA MUJINI UD.......nadhani watot wa UD wanakuwa na overconfidence...

Pamoja na kuwa ukweli UD inachukuwa wanafunzi wenye makzi nzuri zaidi ....lakini ujuwe mnapoingia chuo kikuuu ....mnakuwa kwenye mazingira tofauti...kuna ambao hawakupata devision one za kuingia THE PREMIUM Ud...just kwa kuwa wamesoma kwenye shule duni....lakini wanapokuwa kwenye mazingira sawa ukichanganya na akili zao za asili ...uwezo wao hukua kwa kasi ya ajabu!!

......
 
Hapa sioni tatizo kabisa.
Mimi mwenyewe nime apply kwenye kazi ambayo requirement ikisema experience miaka mitano ,tena nikiwa mwanafunzi na nimeitwa na makapuni makubwa na nikiwa short listed baadhi ya makapuni hayo ni ALCATEL-LUCENT,Atos origin n.k.

Na kiwango cha kufaulu wajili wajanja hawaangalii sana wanachoangalia je nini unakifahamu kuhusiana na kazi waliyokuitia.Pia experience mwajuwa je? hawo jamaa hawana experience?? kumaliza shule 2008 si kigezo kabisa.

Mtu iga first class yako andika CV yako shagharabala nenda kwenye interview ushindwe kuwakilisha uone jinsi utakavyopigwa bao na watu wa third class.

Hapa kwa kweli mimi sioni hoja mpaka hapo baadae mtakapotumwagia data za uhakika

Ulikuwaje mwanafunzi na ukaomba kazi? ni part time au kazi ya usiku?wewe umewahi kutuambia hapa JF kuwa unataka kuwapeleka ulaya wachezaji wa ila huna contact zao viongozi wa club na timu ya Taifa wanakufanyia hiyana.tukakupa contact zao wote nini kiliendelea? natilia mashaka kuwa umefanya kazi ALCATEL ukiwa na status ya uanafunzi.

Hao wa UDSM ,Tumaini na vyuo vingene hawakupewa nafasi ya kuitwa kwenye interview wakafanye vitu vyao.ndio maana wakajazwa Nyegezi ili wasije UDSM kuwaharibia.Kashishilah angewapa nafasi aone kama watu wake wa ST.AUGUSTINE kama wangepita.
 
..st augustine ipo rwanda na kenya?..wahitimu hao ni watanzania????...sasa lazima watu wa UD ...ambako wengi tumepita mjuwe soko la ajira sasa lina ..mzumbe,dodoma,stjohn,augustine,Tumaini,kairuki,IFM, arusha,.meru,muslim...st.joseph,dar tech...etc

NIMEONGEA NA WAAJIRI WENGI ...WANASEMA WAHITIMU WA VYUO VINGINE ...WANAJIANDAA VEMA ZAIDI KWA INTERVIEWS NA MARA NYINGI HUWAZIDI WATOTO WA MUJINI UD.......nadhani watot wa UD wanakuwa na overconfidence...

Pamoja na kuwa ukweli UD inachukuwa wanafunzi wenye makzi nzuri zaidi ....lakini ujuwe mnapoingia chuo kikuuu ....mnakuwa kwenye mazingira tofauti...kuna ambao hawakupata devision one za kuingia THE PREMIUM Ud...just kwa kuwa wamesoma kwenye shule duni....lakini wanapokuwa kwenye mazingira sawa ukichanganya na akili zao za asili ...uwezo wao hukua kwa kasi ya ajabu!!

......

Wako wa Tumaini university wameachwa sio Udsm peke yake.ila kama kujiandaa kwenye interview wangewapa fursa na wa vyuo vingine ili wapate sababu za kusema kuwa unaona Nyegezi walivyo na uwezo wa kujieleza!lakini walioitwa wote ni Nyegezi kama nafasi ya Hansard wameitwa watu 15 na kumi na nne ni Nyegezi-ST-Augustine.
 
Ulikuwaje mwanafunzi na ukaomba kazi? ni part time au kazi ya usiku?wewe umewahi kutuambia hapa JF kuwa unataka kuwapeleka ulaya wachezaji wa ila huna contact zao viongozi wa club na timu ya Taifa wanakufanyia hiyana.tukakupa contact zao wote nini kiliendelea? natilia mashaka kuwa umefanya kazi ALCATEL ukiwa na status ya uanafunzi.

Hao wa UDSM ,Tumaini na vyuo vingene hawakupewa nafasi ya kuitwa kwenye interview wakafanye vitu vyao.ndio maana wakajazwa Nyegezi ili wasije UDSM kuwaharibia.Kashishilah angewapa nafasi aone kama watu wake wa ST.AUGUSTINE kama wangepita.

Tatizo lako unapenda ligi zisizo na miguu na kichwa ,lawachezaji linatokezea wapi? kifupi chansi zilitokea mimi kama mtanzania nikiwapigia debe wazangu waje wasakate kabumbu lakini ndivyo hivyo tena.

Sijakwambia nimefanya kazi alcatel ila nimeitwa kwenye interview tena nikiwa mwanafunzi na kazi yenyewe zilikuwa zinastate experience miaka mitano.
Ungekuwa wewe ungesema nimetowa rushwa teh teh teh teh kwa sababu tu udsm wamebwagwa.

Waitweje kwenye shortlist kama hao jamaa wa AUG wameshaonyesha wanatisha ktk CV.
kwa mfano.
Ngoja nikupe siri moja wale jamaa wanaofanya usaili ukishaweka tu sijui umesoma chuo gani 90% umeshamwagwa.Na ukiweka sijui ma vyeti yako nayo unaongeza 9% zinakuwa zimefika 99% za kumwagwa.

Mwezako anakuwekea tu mimi nina first digrii ktk uandishi wa habari bila kutia mbwembwe nyingi. Huyooo yupo ktk shortlist.
 
Hili Bunge la CCM ni Bunge uchwara limejaa mafisadi na siku zote hawako tayari kuweka mbele maslahi ya nchi bali yale ya chama cha mafisadi. Huu ni ushahidi mwingine tosha wa kuthibitisha kwamba Bunge hilo ni Bunge uchwara.
 
Kila kitu hufanywa kwa kificho, ingekuwa kuna uwazi haya yangekuwa hayatokei. Kuajiri kwa kujuana na kuvunja sheria yote ni ufisadi.
 
Hii issue haitoishia pazuri..watu wa damage control wanatakiwa waiseize as soon as possible iishe

Naona mmoja wa wahusika kakaa kimya sijui hajafikishiwa salamu au vipi na alivyo na mijijazba atakuja tuu humu kujibizana na hapo ndipo it will turn NASTY

by JUMAMOSI naamini mtasikia tamko la watawala kuhusu hili maana mpaka limeletwa JF inaonekana kuwa ngoma hii ni nzito na ndo kwanza bado mbichi
 
Kwa mujibu wa barua ya malalamiko kwa DR.Kashishilah Thomas majina ya waliomaliza NOV 2008 na hawana uzoefu hata wa miezi sita baadhi yao ni TUSAJINGWE,MUNGILE,CATHERINE MWIHULU,SALVATORY MKUDE,JOSEPHAT QORRO,MTAKI,EVARIST,JASMINI BABLIA,MORORO,WAMBURA,CATHELINE,IRINE,MWIHULA hao wote ni darasa moja wamehitimu NOV 2008.

UNAPOCHUKUA WATU WA DARASA MOJA KAMA WANA WEAKNESS BASI NI WOTE ILA UKIWEKA MCHANGANYIKO WANAWEZA KUJIFUNZA KWA WENZAO AU WAKAWAFUNZA WENZAO.

CHANZO CHENYEWE KUNA DADA MHITIMU WA ST.AUGUSTINE AMBAYE YUKO HR BUNGENI, AKISHIRIKIANA NA DAP NOMBO KWA BARAKA ZA DR.KASHISHILAH WAMEKUWA WAKIFANYA MAZINGAOMBWE HAYA KWA MUDA MREFU.

no wonder i keep cming back to JF

Lakini nakushangaa wale wahusika wengine wawili mbona huwataji au unaogopa?

kinachokuogopesha ni nini?

By the way mmoja kati ya hao anasema kuwa malalamiko yaliyopelekwa ni ya mwendawazimu hivyo zoezi liendelee

au habari huna?
 
ST.Augustine hawako juu kuwashinda UDSM au Tumaini University.waliochukuliwa wana kiwango kidogo cha kufaulu.nimebahatika kuona vyeti vya walioachwa na waliopita kwenye interview,wameachwa wengi wenye uzoefu na uwezo.mfano sharti la kazi lazima uwe una uzoefu wa miaka miwili hao wa ST.AUGUSTINE hata mmoja hana sifa hiyo.huwezi kuchukua watu wa darasa moja Hansard Repoter wameitwa watu 15 kwenye interview na wa ST.AUGUSTINE wako 14. nafasi zinazotakiwa ni saba.ST.Augustine hawawezi kuwa juu ya UDSM hata kwa nini.inaonekana wewe ni mmoja ya hao walioitwa kwenye Interview wakiwa wahitimu wa ST.Augustine utasema vipi majungu wakati Hard Facts zipo na unapewa.

Upenzi wa vyuo kwakua mtu fulani kasoma chuo fulani si msingi sana hapa, St. Agustin yaweza kuwa juu katika fani fulani nakuwa chini katika nyingine halikadharika UDSM. Swala kubwa hapa ni fresh graduand from school as opposed to those with 2 year experience.
 
Tatizo lako unapenda ligi zisizo na miguu na kichwa ,lawachezaji linatokezea wapi? kifupi chansi zilitokea mimi kama mtanzania nikiwapigia debe wazangu waje wasakate kabumbu lakini ndivyo hivyo tena.

Sijakwambia nimefanya kazi alcatel ila nimeitwa kwenye interview tena nikiwa mwanafunzi na kazi yenyewe zilikuwa zinastate experience miaka mitano.
Ungekuwa wewe ungesema nimetowa rushwa teh teh teh teh kwa sababu tu udsm wamebwagwa.

Waitweje kwenye shortlist kama hao jamaa wa AUG wameshaonyesha wanatisha ktk CV.
kwa mfano.
Ngoja nikupe siri moja wale jamaa wanaofanya usaili ukishaweka tu sijui umesoma chuo gani 90% umeshamwagwa.Na ukiweka sijui ma vyeti yako nayo unaongeza 9% zinakuwa zimefika 99% za kumwagwa.

Mwezako anakuwekea tu mimi nina first digrii ktk uandishi wa habari bila kutia mbwembwe nyingi. Huyooo yupo ktk shortlist.

MKAMAP.

Hakuna cv unaweza kuandika bila kutaja chuo ulichosoma, mimi sijawahi kusikia labda wewe ulipoomba kazi huko ALCATEL.Obama asingetaja wapi kasoma lakini kila mtu anajua HARVARD.kutaja chuo ni jambo la wajibu kwenye CV inaonekana hata CV kwako ni mtihani.

Sema utakavyo lakini huwezi kufananisha status ya Udsm na Nyegezi.kwenye ajira HR lazima azingatie ubora wa chuo alichosoma muombaji.

Haiwezekani mtu aliyesoma Udsm akafundishwa Accounting na DR.Assad akawa sawa na mwanafunzi aliyemaliza nyegezi akafundishwa na kijana aliyehitimu hapo akapata First class akabakizwa kuwa mhadhiri.

Ubora wa chuo unatizamwa kwenye mambo mengi kama tafiti n.k na hivi vyuo vipya vina matatizo mengi kuanzia library,walimu n.k huwezi kusema mtu aliyesoma medicine KAIRUKI atakuwa sawa na mtu aliyesoma medicine MUHIMBILI university, wa muhimbili ana walimu na ana hospital ya rufaa yenye madaktari mabingwa, Muhimbili ina link na university au taasisi mbali mbali duniani.

Mhadhiri wa Kairuki atakuwa ni part time akitoka kufundisha muhimbili then aingie wodini halafu ndio aende Kairuki.kuna masomo hayafundishwi jioni kama Bio chemistry n.k
maktaba ya Udsm ina past papers toka 70s jee Nyegezi watakuwa na vitu kama hivyo?

Oxford University haiwezi kuwa sawa na Makelele university,mtu aliyesoma Oxford atakuwa na exposure kubwa kwa kusoma na watu tofauti tofauti na facilities za chuo ni advantages kwake,ubora wa wahadhiri, research zilizofanywa n.k si sawa na Makelele,

pia mtu wa Udsm atakuwa na exposure kubwa kuliko wa Nyegezi.Obama kusoma Harvard digrii ya sheria hatokuwa sawa na Mwakipesile aliyesoma law Tumaini university,Obama atakuwa amekutana na watu wa mataifa mbali mbali akiwa Harvard,Mwakipesile atakuwa na watu wanaofanana nae tu. kuna on line journals mbali mbali ambazo Harvard itakuwa inazo.ambako Tumaini hakutakuwa na facilities kama hizo.

Mkamap akija DR.slaa,DR.Nchimbi,DR,Kamala,dr.Nagu na PhD zao ambao wamesoma vyuo zisivyotambulika halafu akaja DR.Kawambwa shukuru,Dr.Mwakyembe,Professor Lipumbana DR.batilda Burian utawaweka pamoja bila kuona ubora wa vyuo walivyosoma?nikupe namba za wachezaji uwapeleke ulaya?
 
Kanda 2 hayo ulosema hapo juu ni mazito mno duh!

hebu mie nimpigie simu First Lady.....
 
Na hili ndilo tatizo la wahitimu wa Tanzania, wote wanataka kufanya kazi za kuajiriwa... ona sasa vyuo vingine vinavyonyanyapaliwa!

Elimu ya kujitegemea iko wapi?

Mnakumbulka shairi hili?

Tumeizika elimu, elimu ya kizamani
Elimu ile haramu, maana ya kikoloni
Imetuishia hamu, kuiga ya ugenini
Elimu yetu ya sasa, yawafaa wananchi

Kama ni kweli elimu yetu ya sasa yatufaa wananchi, kilio cha kuajiriwa kinatoka wapi?

Katibu wa Bunge ana PhD lakini elimu yake imeshindwa hata kuzuia uchafu huu licha ya kupewa taarifa za hila zake akishirikiana na NOMBO.
 
Mkamap, hio CV isiyokuwa n Jina la Chuo...duh mara ya kwanza kusikia...!! au ndio CV za kupika!!!

na Hao wanaofanya shortlist nao magumashi au wamegumikwa wimbi la UFISADI....

Katibu wa Bunge elewa sasa Tanzania inajitajidi kuwa Macho, mambo ya Ajira ni mambo sensitive sana. unapofanya ukiritimba huu usione kuwa utaachwa,pia elewa ufisadi wa style hii unaweza fananishwa na ule unaofanywa na Vibaka barabarani ambao at the end huishia Kuchomwa MOTO...
......usijeingizwa ktk hilo kwani wale waliokosa hizo nafasi wasije kukufanya sivyo wakielewa kuwa Hukutumia Strong Vigezo kufanya selection yako....
 
mimi sio expert wa HR ila kwenye hii issie nadhani hawa jamaa wamechemka maana its imposible watu wa darasa moja kuwa na same grades, experience and level of expertise.

Ila kuhusu chuo gani bora naona watu wameenda out off topic. UDSM au St Augustine vyote bora na pia inadepend na course gani ufanyayo.

Kuhusu working experience na pia kuwa mwanafunzi that is so possible, i know alot of people who study and work part-time that means waimaliza university employaility yao inakuwa kubwa taking into account they are fresh from university with new ideas as well as they have working experience.

Few years ago nilisikia st augustine inafundishwa na jesuit fathers, na kama that is still the case then possible hii university is far more advanced on teaching quality than UDSM. maana jesuit fathers wako dedicated in education and teaching na veti vyao sio vya kuforge lol...

watu wanaojua zaidi watupe habari nini kinaendelea st augustine maana tusije tukawa tunaongea with no fact. alafu pia st augustine hawana redio na television? kama wanayo then possible hawa wanafunzi wanapata experience from there?
 
MKAMAP.

Hakuna cv unaweza kuandika bila kutaja chuo ulichosoma, mimi sijawahi kusikia labda wewe ulipoomba kazi huko ALCATEL.Obama asingetaja wapi kasoma lakini kila mtu anajua HARVARD.kutaja chuo ni jambo la wajibu kwenye CV inaonekana hata CV kwako ni mtihani.

Sema utakavyo lakini huwezi kufananisha status ya Udsm na Nyegezi.kwenye ajira HR lazima azingatie ubora wa chuo alichosoma muombaji.

Haiwezekani mtu aliyesoma Udsm akafundishwa Accounting na DR.Assad akawa sawa na mwanafunzi aliyemaliza nyegezi akafundishwa na kijana aliyehitimu hapo akapata First class akabakizwa kuwa mhadhiri.

Ubora wa chuo unatizamwa kwenye mambo mengi kama tafiti n.k na hivi vyuo vipya vina matatizo mengi kuanzia library,walimu n.k huwezi kusema mtu aliyesoma medicine KAIRUKI atakuwa sawa na mtu aliyesoma medicine MUHIMBILI university, wa muhimbili ana walimu na ana hospital ya rufaa yenye madaktari mabingwa, Muhimbili ina link na university au taasisi mbali mbali duniani.

Mhadhiri wa Kairuki atakuwa ni part time akitoka kufundisha muhimbili then aingie wodini halafu ndio aende Kairuki.kuna masomo hayafundishwi jioni kama Bio chemistry n.k
maktaba ya Udsm ina past papers toka 70s jee Nyegezi watakuwa na vitu kama hivyo?

Oxford University haiwezi kuwa sawa na Makelele university,mtu aliyesoma Oxford atakuwa na exposure kubwa kwa kusoma na watu tofauti tofauti na facilities za chuo ni advantages kwake,ubora wa wahadhiri, research zilizofanywa n.k si sawa na Makelele,

pia mtu wa Udsm atakuwa na exposure kubwa kuliko wa Nyegezi.Obama kusoma Harvard digrii ya sheria hatokuwa sawa na Mwakipesile aliyesoma law Tumaini university,Obama atakuwa amekutana na watu wa mataifa mbali mbali akiwa Harvard,Mwakipesile atakuwa na watu wanaofanana nae tu. kuna on line journals mbali mbali ambazo Harvard itakuwa inazo.ambako Tumaini hakutakuwa na facilities kama hizo.

Mkamap akija DR.slaa,DR.Nchimbi,DR,Kamala,dr.Nagu na PhD zao ambao wamesoma vyuo zisivyotambulika halafu akaja DR.Kawambwa shukuru,Dr.Mwakyembe,Professor Lipumbana DR.batilda Burian utawaweka pamoja bila kuona ubora wa vyuo walivyosoma?nikupe namba za wachezaji uwapeleke ulaya?

Rafiki yangu hili ni tatizo kubwa kuelimika kunatokana na mtu na sio chuo.Haya mwakyembe ndiyo aliyasema kwa namna moja ama nyingine akija mweupe mkopo anapata akija mswahili blah blah

Hiyo ndiyo mentality na yakwako kuhusu elimu zinafanana sana na mfano wa mwakyembe.Kama chuo ndio kuelimika kwisha kazi Angalia hao viongozi wengi wa Tanzania wamesoma vyuo gani? 80% wametoka vyuo unavyovitaja yani.

UDSM - Havard - oxford .Angalia walivyo mafisadi.Mkuu mwajili mjanja anaangalia una nini kichwani na si umetoka wapi.
 
issue hapa ni jinsi watu walivyodhulumiwa na ofisi ya Bunge kwenye uajiri

au hilo nalo tatizo kwako?
 
Mkamap, hio CV isiyokuwa n Jina la Chuo...duh mara ya kwanza kusikia...!! au ndio CV za kupika!!!

na Hao wanaofanya shortlist nao magumashi au wamegumikwa wimbi la UFISADI....

Katibu wa Bunge elewa sasa Tanzania inajitajidi kuwa Macho, mambo ya Ajira ni mambo sensitive sana. unapofanya ukiritimba huu usione kuwa utaachwa,pia elewa ufisadi wa style hii unaweza fananishwa na ule unaofanywa na Vibaka barabarani ambao at the end huishia Kuchomwa MOTO...
......usijeingizwa ktk hilo kwani wale waliokosa hizo nafasi wasije kukufanya sivyo wakielewa kuwa Hukutumia Strong Vigezo kufanya selection yako....

Mkuu ndiyo hivyo sasa ukiitwa ktk interview akakupiga swali la kwanza tuambie short history ya yako na ya elimu yako utamweleza nini ? wakati vyote umeshavimwagwa ktk cv.

Kitu kingine waajili wameshaona kuanza kuweka majina ya vyuo ktk cv ni ngao fulani ambayo unaanza kujitengenezea mfano unakwenda kama Juma ki uhalisia ni mrefu harafu wewe ukaanza kumwita Juma mrefu ,hapa inamaana unataka kuonyesha kitu fulani hadhira.

Ktk Cv weka makobola unayoyafahamu ambayo yatawakovinsi waajili waamini utawezana na mikiki mikiki ya kazi yao na wakukuita ktk interview ndiyo unayadefendi vilivyo uone hata kama umetokea wapi unampiga bao wa havard.

Harafu usiweke ma photocopy yako ya vyeti wakati unatuma CV unless stated siku wakikuita ktk inteview unaenda na vyeti uriginal na wakiona upo makini sana utaona wanataka kuona vyeti vyeti vyako.
 
issue hapa ni jinsi watu walivyodhulumiwa na ofisi ya Bunge kwenye uajiri

au hilo nalo tatizo kwako?

hili naona ni tatizo mkuu mimi sioni kama kulikuwa na mkataba lazima watu fulani kutoka ktk chuo fulani lazima wawepo ktk shortlist.Labda wewe nieleze kidogo ni kivipi hao jamaa wamezulumiwa.
 
Back
Top Bottom