Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,470
kiasi ya kwamba katiba ya uganda iliandikwa kipindi cha OBOTE kuwa huwezi kuwa gavana wa benki kuu ya Uganda kama sio mkatoliki. hili hadi leo lipo.
mmmh very painful na huyu M7 naye ni Mkatoliki?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kiasi ya kwamba katiba ya uganda iliandikwa kipindi cha OBOTE kuwa huwezi kuwa gavana wa benki kuu ya Uganda kama sio mkatoliki. hili hadi leo lipo.
soma kitabu cha padri sivalon kanisa katoliki na siasa Tanzania.utajua na kuona kila kitu.Hoja nzuri lakini presenter anakosa focus. Issue ni kuwa hawana sifa au ni wakatoliki. Maana siamini kama wote waliochukuliwa ni wakatoliki kwani St. Augustine inachukua watu wa dini zote. Pia siamini kama watu wenye sifa wapo St. Augustine tu.
Inawezekana pale wakubwa walikuwa na mtu wao wakaona wachukue watu wote wa chuo kimoja ili kupoteza ushahidi lakini pia macho ya kifisadi hayaoni. Ushahidi unaonesha mafisadi mara nyingi hawajui kusoma alama za nyakati.
Ninaamini kuwa kama ofisi ya umma ilitakiwa kuchukua watu wa vyuo vingi zaidi ili kuweka diversity ya watumishi wake. Ukiweka watu wote wanatoka chuo kimoja kwa mtazamo wangu naona si sahihi.
Hoja ya kandanda kuhusu wakatoliki sikubaliani nayo hata kidogo.Kwanza mimi ni mluteri lakini sijawahi kugundua kuwa tunaonewa. Malalamiko haya nimeyasikia mara ya kwanza pale Lowassa alipojiuzuru akapokelewa kwao Monduli kwa shangwe na mmoja wa watu maarufu alikuwa Askofu Laizer wa Arusha. Baada ya hapo Lowassa alisafiri kwenda Israel kwa ziara ya kidini na mhubiri maarufu Mr Mwakasege ambaye by default nae ni mluteri. Baada ya hapo ikaonekana kuwa waluteri wanamuunga mkono Lowassa na pia wanahisi kuwa wanaonewa.
Lakini hizi ni hisia tu,sidhani kama kuna ukweli wowote. Ukiangalia kwenye nchi yetu,wakristo wa kikatoliki ndiyo wengi zaidi kuliko wakristo wengine. Kielimu pia hawako nyuma sana kwani maeneo ambayo wamisionari wa kikatoliki walifika hapo zamani walijenga mashule.
Suala la Malecela linajulikana,kama hujui leta maswali watu watakujibu. Nadhani hujui sababu kwanini Mwalimu alitishia kurudisha kadi ya CCM. Tatizo halikuwa dini(uanglikana). Kuthibitisha hilo kabla ya hapo Mwalimu alipong'atuka alimuachia madaraka Mzee Mwinyi ambaye ni muislam wakati walikuwepo wakatoliki wengi sana kipindi hicho ambao walikuwa na uwezo kama/zaidi ya mzee mwinyi.
Mwisho, naomba nitoe wito kwa watanzania,tunaposhindwa mambo tusilete chokochoko za udini kwani ukweli tunaujua. nchini kwetu waislam na wakristo wanaishi nyumba moja wanalala pamoja, wanafanya kazi ofisi bila kutengana. Utajua huyu muislam au mkristo inapofika wakati kila mtu anaenda kwenye ibada.
Asante
Yapo Mengi kaka....na ndio maana Mh. Mkapa wala hakosi Usingizi wake....Mkapa anawajua wote na madhaifu yao.....duh inasikitisha sana kumbe mama kilango naye ni mpiga mapande duh jamani huu ufanisi tutasubili sana kama ndo hivyo inauma sana na kusikitisha watoto wa maskini hatuna chetu tena.
Naomba kuuliza,
Kwani Dr Kashishila anasali kanisa gani?
.
.....NYEGEZI haiwezi kupambana na Tumaini acha Udsm.labda ijipime na Kairuki au Bukoba University.
siyo bunge tu jamani! Serikali kuu ndo kulivyo: yaani hizi interview Panels mara nyingi unakuta kila mtu ana mtu wake!
sasa sijui ni wapi angalau kuna objectivity: may be mashirika ya nje!
Hakuna sababu ya msingi. ni vitu viwili tofauti.kwa nini?
ipo sababu yoyote ya msingi?