Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Bunge limepitisha nyongeza ya mapato na matumizi ya jumla ya shilingi bilioni 945.7 kwa ajili ya kuongeza kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2024/25 kutoka shilingi trilioni 49.346 iliyoidhinishwa awali hadi shilingi trilioni 50.291.
Nyongeza hiyo imewasilishwa na Waziri wa Fedha, Mwigulu (Mb), ambaye ameeleza kuwa fedha hizo zitakazotekeleza shughuli za sekta za elimu, afya utalii na program mbalimbali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, zimepatikana kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Pia soma: Waziri wa Fedha apendekeza nyongeza ya Tsh. bilioni 945.7 kwenye bajeti ya serikali ya 2024/25. Pesa za Kampeni zinatafutwa?
Alisema shilingi bilioni 325.9 zimetengewa Wizara ya Fedha, kwa ajili ya matumizi ya kitaifa, kugharamia malipo ya madeni ya watumishi, wakandarasi na wazabuni wa ndani pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba.
Nchemba aliongeza kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetengewa shilingi bilioni 131.4 kwa ajili ya kugharamia mahitaji ya Mtaala mpya wa sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule za sekondari za amali, upatikanaji wa vifaa na walimu.
“Fedha hizo zitagharamia ukamilishaji wa ujenzi wa vyuo vya VETA, ujenzi wa maktaba ya Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), ujenzi wa miundombinu ya Chuo cha Nelson Mandela-Arusha, ujenzi wa majengo ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima pamoja na ujenzi wa Jengo la Maktaba Mwanza,” alibainisha Mwigulu.