Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Ubaya ni kwamba bila aibu Spika anakuwa PRO wa CCM.
Sijui hiyo kazi kapewa na ni yarabi?
Anapangiwa kazi Polepole siku hizi.
Boss wa Bunge jitambue basi linda kiti chako!!
atajitambuaje kama kuingia mjengoni alimdunda ntu live na ikawa pouwa. sasa kwanini asiwashwe washwe kutetea kiti chake!!
 
Sasa itabidi tuanze kuangalia muda ama saa ya barua kuandikwa
Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.

Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.

Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Ndugu Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotamka kwamba:

“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.”

Hivyo, Ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.

Screen-Shot-2017-11-01-at-3.19.21-PM-950x704.png
Screen-Shot-2017-11-01-at-3.20.17-PM-950x559.png
 
View attachment 621961

Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.

Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.

Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapo juu..

Hii hapa Barua ya Nyalandu aliyomuandikia Spika
View attachment 622471
Hizi ni siasa za kisanii na ni maelezo yayokanayo na maagizo toka nje ya mhimili....ama kweli wanazidi kujivua nguo hadhani.
 
Haya ni maajabu ya dunia....yaani spika ndo amekuwa msemaji wa chama?....barua ya kufukuzwa inatangazwa na spika shame..!!!

Chama ndo kilitakiwa kuutangazia uma kwamba wamemvua uanachama na kikao kilikaa lini...hii ni aibuuuu ptuuuu
......Albadiri haijawahi kumuacha mtu salama.
 
Hawa wameshanganyikiwa kabisa bora wangekaa kimya waulizeni hiyo barua kutoka kwa katibu mkuu ikimueleza spika kumvua Ubunge na kwa kikao kipi PolePole asiropoke wakati wa press yake juzi?
Akili ya kawaida nilitegemea kuona barua kutoka ofisi ya katibu mkuu CCM ikieleza kufukuzwa kwa Nyalandu ndipo ifuate ya Spika wamechemka
Picha Lazaro Nyalandu leo akiwa na Tundu Lissu hospital Nairobi leo.View attachment 621953
Seeking for political asylum....he's not Gina escape the judgement cup Of his leadership.
 
Back
Top Bottom