Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Watanzania wa leo si wale wa Nyerere msitulishe matango pori nyalandu kajiuzuru kwa anachokiamini katika siasa sio ccm wamemwandikia barua ya kumfukuza mmechelewa na propaganda zenu
 
  • Thanks
Reactions: AWM
Kwa upuuzi huu kweli hii nchi imewashinda. Endeleeni kuwapa 5 wapinzani.
 
Hiyo ni barua uchwara. Kwa sababu hauwezi kumvua uachama mwanachama aliye kihama chama kwa mapenzi yake mwenyewe.
 
Ni aibu kwa ofisi ya bunge na CCM kufanya vitu kama hivi. Mheshimiwa Nyalandu alitangaza rasmi kuhama CCM sasa inakuwaje tena hii barua ya kufukuzwa CCM. Kuhama CCM ni dhambi?
Ni katika kujaribu kumdhalilisha tu.
Kwa ninavyojua Ndugai apokee barua toka tarehe 30 (Jumatatu) kisha apige kimya mpaka leo kweli??
Hata Mkulu mwenyewe alisema kua Majizi yamekimbia CCM, hakusema Yamekimbizwa CCM akimaanisha jamaa aliondoka mwenyewe na hakuondolewa.

Sasa hizi story za barua kutoka kwa Katibu Mkuu kweli haziingii akilini
 
Huko CCM ni mnara wa Babeli, na wote tunajua kilichotokea. Kama katibu mkuu anadai kufukuza mtu, wakati mwenezi hana taarifa, maana yake kila mtu na lwake.

so katiba yao katibu mkuu anamamlaka ya kufukuza mtu uanachama tena mbunge ?
 
Watu wakisema Bunge ni kitengo cha Ikulu wanakataa, sasa kama Bunge linatumika kwenye propaganda chafu kama hizi nani atakaa amuamini mtu anayejiita spika na wenzake wa aina yake?

Hebu fikiria CCM inayopenda sifa iache kuitisha mkutano na waandishi wa habar kutangaza kumvua uanachama Nyalandu ndio watume hiyo taarifa kwa spika eti watume barua tu hivihivi?

Saa nyingine hawaCCM wakumbushwe kuacha utoto, kwani mkuu wao pia hata hili la leo atakuwa anaona aibu kwani ingekuwa kweli basi ike juzi kule Mwanza angeifanya topic.
 
Mi binafsi hiyo barua ya binge hainisumbui kichwa na hata ya ccm isingenipa kiwewe! Kikao hicho cha kumfukuza Nyalandu kilikaa link na wapi? Maana, kilichokaa mara ya mwisho wengi wetu tulifikiri nape, bashe navwengieo wangebaraswa lakini wakaja na taarifa ya 'chama kiko imara'!

Ccm wajue watanzania si 'wadanganyika' katika zama hizi za tehama!
Ulitaka wawe watangaza vikao Kukujulisha?
 
Hatudanganyiki tunachojua ni Nyalandu kajiuzulu na si vinginenyo
 
Juzi Polepole alisema "....kuhama kwa Nyalandu sio jambo geni.....ni afya ya siasa..." Polepole says Nyalandu is insignificant

...na kisha akasema tena "....namshangaa Nyalandu kuhama CCM chenye itikadi ya Ujamaa na kwenda CHADEMA kisicho na itikadi...."

Spika Ndugai anadhalilisha Bunge na kiti cha u-Spika, Ofisi ya Bunge imekuwa kama Tawi la Wakereketwa wa CCM Kizota. Wabunge mwajibisheni huyo ili msizidi kudhalilika.
Haraka haraka hakuwa na taarifa kama ofisi ya bosi wake na ilishamjadili na imeshaandika barua ya kumfukuza uanachama
 
Kuna mijitu na heshima ya nafasi zao inatia aibu.Kwel hii begging generation is unchangable.
 
Hakuna kikao chochote CCM imekaa tangu Nyalandu atangaze kukihama Chama.CCM huwa ina utaratibu wake wa vikao na si vinginevyo.
 
Polepole alisema Nyalandu amejiuzulu sababu kashindwa kasi Ya rais, spika anasema Nyalandu kavuliwa uanachama.
Nomaaaaa
34044878abe6d7fc4a9fb49daf41e2cb.jpg
 
Back
Top Bottom