Bunge laulizwa alipo Job Ndugai, lasema halina taarifa alipo, inawezekana yupo jimboni kwake

hv kuna kosa akifukuzwa ubunge kama alivyomfukuza joshua nasari
 
Kijifungia ndani hakutakusaidia mzee wangu. Unaweza jiletea magonjwa mengi kutokana na msongo wa mawazo. Tunajua fika hukutafajia hili lililotokea lakini binadamu wote hatujui kesho yetu.
Yaliyokutokea yamekua funzo kwetu kwamba vyeo na dhamana tulizopewa si za milele. Zinaweza kukoma muda wowote tena pale tusipotarajia. Jipige moyo konde utoke hadhari maisha yaendelee.
Uliyotukosea watanzania ukiwa spika wa bunge ni makubwa kuliko kosa lililokuondoa kwenye kiti. Utafanya vizuri kama utatoka hadharani pia utuombe radhi. Ukifanya hivyo nakuhakikishia mzee wangu utaishi kwa amani zaidi kuliko hata ulipokua na cheo. Toka hadharani acha kujificha. Tumejiandaa kukupokea kwa upendo tulojaliwa.
 

Ndugai aweza kuwa mateka mahali.

Yuko wapi Moses Lijenje?
 
huyu Ndugai alimfuta ubunge Lissu kwa kile anachodai ni mtoro na hajulikani alipo sasa tulia amfute na na yeye ubunge na kunyimwa stahiki zake zote kwa utoro bungeni bila taarifa
Wala siyo yeye aliyempora Lissu ubunge bali serikali hii ambayo imempora yeye Uspika. Katiba mpya siyo kipaumbele chetu.
 
Ameenda kumtembelea mkuu wake aliyetaka kumlazimisha kuendelea na utawala lakini Bwana akafanya yake!!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Jinga tu , mtu mzima na akili zako unadanganywa na mkwere wa msoga?
Mkuu, siasa za bongo ni calculation kali sana plus figisu nyingi, ghiriba, shirki, ngebe, unafiki etc..kama unafikiri ni rahisi kiasi cha Job kuingizwa mkenge jaribu kugombea jimbo lolote 2025.
 
leta hoja ya maana sio kila siku lissu. umeanza vizuri ungeandika hivi kama bunge halina taarifa ya ndugai alipo na yenyewe ndio mhimili katika mhimili mitatu je nani atajua?kila siku lissu , mara mbowe , mara sijui nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…