Bunge lazima kumhoji mkuu wa JWTZ au waziri wa ulinzi. Usalama wa taifa. Lt.Col. Seromba

Bunge lazima kumhoji mkuu wa JWTZ au waziri wa ulinzi. Usalama wa taifa. Lt.Col. Seromba

Je, unataka hiyo kikao maalum ?

  • Ndio nataka.

    Votes: 22 88.0%
  • Hapana sitaki.

    Votes: 3 12.0%

  • Total voters
    25
siku hizi masuala muhimu hatuyapendi tunapenda vitu rahisi kusikia.Kama nchi hii ikiendelea na jinsi ya tunavyofikiri sijui tutaishia wapi miaka 20 ijayo.Watu tunapenda vyama kuliko nchi,tunapenda misaada kuliko kutumia mbongo zetu kutatua matatizo yetu

natafuta antvirus ya huyu kirusi siasa katika ubongo wa watz......msaada kwa mwenye nayo tafadhali
 
hiyo ni kamati ya ulinzi na mambo ya nje ndugu,jaani bunge lote likae kumhoji mtu 1 si itakuwa uonevu?

ww ndo shughuli za bunge uyo mtu mmoja unayemzarau unajua impact yake ktk taifa? kuna watu ni muhumu kuliko hta idadi yote ya mkoa refer pengo la nyerere kuanzia TAIFA mpka CCM
 
bunge la sasa halina meno hayo... kuna ushabiki na siasa za bendera
 
Habari za mchana,

Naomba Bunge letu ifanye kikao maalum ya kumhoji mkuu wa JWTZ au waziri wa ulinzi kuhusu Lt. Col. Seromba.
Watanzania wanataka kujua ukweli. Watanzania, lazima tujue huyo Lt. Col. Seromba:
- alikuwa anafanya nini ?
- anatoka wapi ?
- cheo chake inamruhusu kuona/kupata/kusoma nini Jeshini ?
- pahali anaweza kukimbilia ?
- mafunzo gani ilipata ?

Je, Jeshi wamekagua wanajeshi wote ( uwezekano wa askari wapelelezi) ?
Hatua gani JWTZ imechukua ?
Je, Jeshi wamekagua computer zote ( uwezekano wa virus ) ?

Watanzania, tusisahau kama tuko katika kipindi cha misukosuko:
- Iran inatumia bendera ya Tz (labda ni USA, UK au Israel inapeleleza);
- uhusiano wa kijeshi kati yetu na China au na North Korea ;
- NSA ya USA na upelelezi wao duniani kote ;
- madawa ya kulevya ( isije ikawa story ya Guinea ) ;
- uhusiano mbaya na EAC (Rwanda na Kenya);
- uranium na uhusiano na makampuni ya Russia (nakupa uranium, unanipa silaha);
- gas na uhusiano na makampuni ya China (nakupa gas, unanipa silaha) ;
- etc .

Mungu Ibariki Tanzania.

- Anonym poll
- Leta idea yako

maoni yako ni mazuri sana ila ni ya kitoto mno....majeshi ya nchi zote huwa hayapo perfect,na ndo maana mtu mmoja hawe kiuwa na taarifa zote za jeshi labda mkuu wa majeshi na Rais kwa hiyo mi sioni unachoogopa kuhusiana na huyu mtoro...utapoteza muda wako mwingi lakini haitasaidia chochote...watoro ni wengi...kwa mawazo yako wanajeshi hawapaswi kuacha,kukaa na watu,kustaaf nk......hatwendi hivo kama taarifa za jeshi unataka kuzijua zipo nje nje tu ...muulize julius asange wa wikileaks uone kama hatakupa data za kutosha....
usiogope saaana jua jeshi linaundwa na binadamu....waongo wamo,wanaopenda pesa/sifa wamo,wambea wamo nk....
 
Ndugu yangu tumeliwa, kwa mujibu wa JW wenyewe walisema huyu alikuw aMtaalamu wa mifumo ya Komputa, na wakubwa wote piengine hata Mwamunyange mwenyewe alikuwa anategemea kufundihswa na huyu mtu, Kwa watu wanofanya kazi za ICT na hasa za Support watakubaliana na mimi tukiwa maofisini humu almost siri zote za wakubwa na ofisi huwa tunazijua na tukizitaka ni mwendo wa kubofya tu na kila kitu kipo wazi.

Kumbuka tena walisema huyu alikuwa mkufunzi wa ICT na alikuwa nafundisha hao wakubwa.

Uko sahihi asilimia 100% kabisa.
 
maoni yako ni mazuri sana ila ni ya kitoto mno....majeshi ya nchi zote huwa hayapo perfect,na ndo maana mtu mmoja hawe kiuwa na taarifa zote za jeshi labda mkuu wa majeshi na Rais kwa hiyo mi sioni unachoogopa kuhusiana na huyu mtoro...utapoteza muda wako mwingi lakini haitasaidia chochote...watoro ni wengi...kwa mawazo yako wanajeshi hawapaswi kuacha,kukaa na watu,kustaaf nk......hatwendi hivo kama taarifa za jeshi unataka kuzijua zipo nje nje tu ...muulize julius asange wa wikileaks uone kama hatakupa data za kutosha....
usiogope saaana jua jeshi linaundwa na binadamu....waongo wamo,wanaopenda pesa/sifa wamo,wambea wamo nk....
labda maoni yangu ni ya kitoto lakini kusema kama jeshi si perfect kwajila ni binadamu so tuendelee hivyo hivyo, hiyo ndio maoni ya kitoto ! of course there is imperfection and it's our duty to try to correct those imperfection so that in the future, we are protected!
 
Uko sahihi asilimia 100% kabisa.

pongezi kwa kuwaza zaidi ya kikomo cha upeo wako. Jeshini hakuna anayejua zaidi ya yaliyopo katika kambi yake, aghalabu ata asiyajue kwa 100% pia.
 
Haya yote yangewezekana kama:

Sisi waTz tungekuwa serious na nchi yetu. Tatizo ni sisi waTz. Cha kushangaza ni kwamba, hata kwa mambo ya kipuuzi tunayofanyiwa na serikali hii, lkn tunaishia kuwaangalia tu. Inatupasa tubadilike ili tuweze kuiwajibisha hii serikali.
 
Back
Top Bottom