Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?

Pascal Mayalla, uwe makini na statements zako. Unasema kuwa 'bumge letu', bunge lenu, wewe na nani? Tupo ambao tunaamini kuwa kwa sasa nchi yetu haina bunge. Na hilo limethibitishwa mpaka na hukumu ya mahakama kuu kwamba kuna watu wamejipa ubunge. Hawakuchaguliwa na mtu yeyote, hao wewe unawaita ni wabunge wako?

Kuna wahuni wamejazana bungeni waliopora haki za wananchi kuwachagua wabunge. Wakuna mwananchi anayewakilishwa na wahuni waliopokonya haki ya wananchi.

Kwa maswali yako:

1) Hatuna bunge, kuna wahuni waliopokonya haki za wananchi wakajitawaza kuwa ni wabunge.

2) Bunge huwa halina wahuni, na itabakia hivyo. Kilichotokea ni wahuni kujiita wabunge.

3) Wahuni lazima waongozwe na mhuni mwenzao. Wanaweza kumwita jina lolote lile. Mhuni hana haki ya kumwita yeyote kumhoji kwa nini ameitwa mhuni. Sasa kama kuna syndicate ya wahuni bungeni, iitwe kwa jina gani zaidi ya kuitwa kwa jina lake halisia?

4) Dr. Slaa ametumia lugha ya staha sana kuiita Serikali ya sasa ni yenye uhalali wa mashaka. Katiba inasema kuwa kiongozi mkuu wa Serikali ni Waziri Mkuu. Mkuu wa nchi ni Rais wa JMT. Katiba inasema kuwa Waziri mkuu atateuliwa na Rais kutoka chama chenye wabunge wengi na kuidhinishwa na Bunge, na lazima awe ni mbunge wa kuchaguliwa. Mwulize Majaliwa alichaguliwa na nani, alipata kura ngapi? Majaluwa kutoitwa mhuni, ni staha tu ya Watanzania, lakini alistahili kuitwa hivyo.
 
Aah! Kumbe na suti zote zile hakuchaguliwa na wanatandahimba! Sikulijua hilo.
 
Asante ndugu Muandishi kwa shabaaha mujarabu.
Kwanza kabisa alichokisema Dr, Padre W.P.Slaa sio utashi mwema, na kwakweli sio ungwana kwa kiongozi makini, mzoefu aliewahi kufikiriwa nafasi ya juu nchini kama huyu kuukosea ustahimilivu na hatimae kuushushia heshima muhimili huu muhimu wa bunge. Angeweza kutumia lugha nyingine kulingana na heshima yake nchini hata kama ameghadhabishwa na kilichofanywa na Bunge. Binafsi naona ni sahihi sana na kwakweli naunga mkono pendekezo la kua, aitwe kwenye kamati ya Bunge, na Ungwana ni vitendo namshauri aitikie wito na aliombe radhi bunge na waTanzania ambao nao wameghadhabishwa na kauli yake isiyokua na nidhamu ndani yake. Vinginevyo mjadala wa hoja zake muhimu utashift badala ya wananchi na makundi mbalimbali kujadili hoja zake, mjadala na vita za maneno kuhusu kauli zake za dharau kwa Bunge na zilizokosa matashi mema ya kiuongozi. Aidha akikaza shingo atadhalilika zaidi na waliojipanga kimdalilisha kisiasa.
 
Njaa itakuuwa wewe mayalla!..... lini utaacha ukuwadi!? Hata ubunge wa kuteuliwa tu wamekunyima! Achilia mbali ubunge wa afrika mashariki....

Sijapata kuona mwaandishi mnafiki! Na mzandiki kama wewe!

Ndio maana hata Mwenda zake alikuita NJAA!.....LIVE IKULU!

Kilichofanywa na Bunge wewe unaiona kiko sawa!? Kuharakisha tusipate muda wa kuhoji!?

Njaa na uoga vitakumaliza!....

Shamba unalopalilia kila siku kukicha.....
Lakini wanavunaniwa wengine.....hushtuki tu!
 
Mhuni au mshenzi hana jina jingine zaidi ya alivyo. Kama unafanya uhuni, sasa uitwe nani?
 
Ni bunge takataka sio la hovyo tu
Lile siyo bunge ni genge la wahuni tupu
 
La hovyo, waoga kwa kulinda maslahi yao, hawajali raia, nchi wala vizazi vyao. Hawana upeo, waroho wa mali na anasa.
Latakiwa kuvunjwa na tuwachuguwe SISI RAIA BILA KUJALI CHAMA!😡😠🤬
 
Ulishaaga humu JF, umesahau nini tena hadi umerudi na nyuzi zako hizi?
 
Mkuu
Hata sisi wananchi tunaamini Bunge letu uhalali wake ni wa mashaka.

Siungi mkono uchaguzi 2020 ulivyofanyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…