Bunge limepiga marufuku mjadala wa sakata la mechi ya Simba na Yanga

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu, amemtaka Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Mhe. Edwin Swalle, kuacha kulizungumzia sakata la mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, kwa kuwa tayari suala hilo lipo kwenye ngazi za maamuzi na linaendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu rasmi.

Mhe. Zungu amesema hayo Bungeni baada ya Mbunge Swalle kuhoji ni kwa nini mpaka sasa taarifa ya uchunguzi kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo haijatolewa hadharani. Naibu Spika amesema kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, si vyema kuendelea kujadili jambo ambalo liko katika hatua ya kushughulikiwa na mamlaka husika.

Wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Mbunge Swalle amesisitiza kuwa ni vyema soka likaongozwa kwa kufuata kanuni badala ya kuendeshwa kwa kutumia busara akitaka pia kuheshimiwa kwa hisia za mashabiki wa soka nchini.
 
Kizuguto sijui kizungumkuti yeye yupo bize maredioni kutangaza kuwa ana Mungu..!! Shetani naye tangu lini akawa na Mungu?
 
Hivi hawa walienda bungeni kuzungumzia maswala ya simba na yanga?
 
Back
Top Bottom