Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tanzania Daima said:LICHA ya baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuipinga kwa kauli nzito na kejeli hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2009/2010, imepitishwa kwa kishindo na wabunge wa chama hicho tawala.
Baada ya kutishwa na spika kwamba kwa mujibu wa ibara ya 90, kifungu kidogo cha 2(b) ya katiba ya nchi, rais hataweza kulivunja Bunge isipokuwa kama wabunge watakataa kupitisha bajeti ya serikali , wabunge 221, wote wa CCM, waliipitisha kwa kuitikia ‘Ndiyo', wabunge 33 wa kambi ya upinzani waliipinga kwa kusema ‘Hapana', huku wabunge wawili kutoka Chama cha Wananchi (CUF), wakipiga kura ya kutokuwa upande wowote.
Kupitishwa kwa bajeti hiyo kwa kishindo, kunaweza kuibua maswali mengi kwani tangu kuanza kwa mjadala wa bajeti hiyo, baadhi ya wabunge wa CCM, walionyesha dhahiri kuikamia kwa kutoa kauli nzito na kuapa kwamba kama haitafanyiwa mabadiliko makubwa, hawataipitisha.
Wewe na mimi tunaweza kufanya maajabu kwa kuchagua viongozi wazuri na kutoka upinzania na sio Kelele kama za wakina Shibuda na wengine hawana jipya hawa jamaa na zaidi ya hayahaya leo inahuzunisha sana
Kama panya huuma na kupuliza na kama hukuzinduka kidole chote umepoteza. Wananchi kama hatutazinduka, tujue tumekwisha.
Wakati wa kuzinduka ni sasa.
Halafu FMES- mwanaCCM mkereketwa ansema anapigania maslahi ya taifa halafu wanaJF rrrrrrrrrrrr na thanks. Can't you people analyse mindsets za hawa wanaCCM?
Hivi hamjui yeyote anayejiita mwanaCCM ni mnafiki kwa wananchi? Niambie kama Mwakyembe aliipinga bajeti ya mwaka uliopita.
Kwa mwanaCCM maslahi ya chama mbele, wananchi (Taifa) baadae.