Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais Madarakani, lakini ni ngumu sana

Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais Madarakani, lakini ni ngumu sana

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
KATIBA INARUHUSU LAKINI NI NGUMU SANA BUNGE KUMWONDOA RAIS MADARAKANI

Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi,

Leo nimeona nije na hili jambo la kusisimua lililopo kwenye katiba yetu lakini lisilotekelezeka. Halitekelezeki kwa sababu CCM haijawahi teua mgombea mwenye matatizo yasiyo ya kawaida kufikia hatua ya kufikiria kumwondoa madarakani. Lakini kwa upande mwingine tuchangamshe akili zetu na kuona jinsi gani hili suala lilivyo gumu kutekelezeka hasa nyakati hizi CCM ikiwa inaongoza.

Katiba kupitia ibara ya 46A imeweka wazi taratibu za kufuatwa. Imeandikwa hivi;
Ibara ya 46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais.

(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au

(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

Baada ya hili azimio la bunge kuna taratibu zimeelezwa hadi kufikia hatua ya Rais kuondolewa. Ugumu uko wapi? Ni kwenye kofia ya pili ya Rais kama mwenyekiti wa CCM. Hapa namaanisha baada ya rais kuondolewa madarakani atabaki na uenyekiti wa chama. Kama aliondolewa kwa fitna basi hao wabunge ambao pia ni wanachama wa CCM watakuwa katika wakati mgumu sana kulikwepa rungu la mwenyekiti.... uwezekano mkubwa ni wengi wao kufukuzwa uanachama. Ikumbukwe mojawapo ya hatua kwenye utekelezaji wa azimio hilo ni uwepo wa taarifa ya maandishi yenye sahihi za wabunge wanaounga mkono. Hakuna kujificha kwa waliohusika. Ila Tukumbuke ibara hii;

67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-

(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

Kwahiyo hakuna mbunge atapenda kujiingiza kwenye matatizo ya kuhatarisha ubunge wake kwa kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wake wa chama. Mwisho wa siku hiyo ibara itaendelea kutotumika. Binafsi nawapongeza sana viongozi wa CCM walioamua rais pia awe mwenyekiti wa CCM. Kuvaa hizi kofia mbili kwa mpigo imezuia hatari nyingi sana.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Na Rais anaweza kulivunja bunge!!

Na kila siku wabunge wa CCM wanatishwa kwamba Rais anaweza kulivunja bunge.

Sijawahi kusikia wabunge wakiambiwa wanaweza kumuondoa Rais madarakani.
Ulitaka waambiwe na nani wakati wanaweza kufanya impeachment.
 
Nimeelezea kwenye post

..Nimekusoma.

..Uenyekiti wa chama sio kinga.

..Wabunge wakiamua wanaweza kubana kwenye chama na bungeni.

..Na kama HOJA yao inaungwa mkono na WANANCHI itakuwa vigumu kuwazuia.
 
..Nimekusoma.

..Uenyekiti wa chama sio kinga.

..Wabunge wakiamua wanaweza kubana kwenye chama na bungeni.

..Na kama HOJA yao inaungwa mkono na WANANCHI itakuwa vigumu kuwazuia.
Tatizo pia rais ana intelijensia kali. Hadi ifike hatua hiyo kuna watu watakuwa wameshashughulikiwa
 
Una mshitaki vipi na wapi MTU mwenye kings kikatiba.
Spika fomu zinapita kwa Mkiti CCM

NCHI HII TUNA MFUMO WAKISHETANI SANA.
Bora kuishi na korona siyo huu mfumo
Hoja kama hizi ni A1 fupi na directly to the point,kudos mtoa hoja hii,kunywa wine ya Rubbicon (red)lete bill inbox
 
..Nimekusoma.

..Uenyekiti wa chama sio kinga.

..Wabunge wakiamua wanaweza kubana kwenye chama na bungeni.

..Na kama HOJA yao inaungwa mkono na WANANCHI itakuwa vigumu kuwazuia.
Wanasema, ni lazima bunge limueleze raisi nia yake ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, hapo sasa kabla wao hawajapiga hiyi kura, raisi anaweza kuamua kulivunja bunge na hivyo kivitendo kwa kutumia sheria hiyo, Bunge haliwezi kumuondoa raisi madarakani.
 
Wanasema, ni lazima bunge limueleze raisi nia yake ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, hapo sasa kabla wao hawajapiga hiyi kura, raisi anaweza kuamua kulivunja bunge na hivyo kivitendo kwa kutumia sheria hiyo, Bunge haliwezi kumuondoa raisi madarakani.
Hilo balaa zito.... 🤣🤣🤣
 
..mbona kila wakati wanakumbushwa kuwa rais anaweza kulivunja bunge?

..nadhani hiyo ni namna ya kuwanyong'onyeza ili wajione hawana uwezo wa kumuwajibisha raisi.

Safi sana JokaKuu. Hili ni jambo linaloonesha kabisa kuwa hakuna check-and-balance na hivo katika ngapi za juu hakuna aliye na maamuzi juu ya matendo ya mwingine. Mara Rais anaweza kuvunja Bunge, Bunge linaweza kumwondoa Rais, lakini Rais ndiye anayechagua hata Jaji Mkuu. Na kama haitoshi, hata maRais na waziri wakuu waliopita bado wanaweza kushiriki katika mchakato rasmi wa kuteua Rais wa siku za usoni. Maana yake makosa yao madarakani yanaweza kulindwa na maRais wa siku za usoni!!

Madaraka ya Rais ni mengi na makubwa kuliko inavohitajika. Wananchi hawana mamlaka mara baada ya kufanya uchaguzi! Pathetic!!
 
Kabla ya wabunge kulipitisha hilo azimio la kumtoa Rais madarakani na kupiga kura, asubuhi yake tu Rais anawahi kulivunja bunge kwa kutumia Katiba ili hao wabunge wakapitishe azimio na wake/waume zao majumbani.

Ndio upuuzi wa Katiba yetu.[emoji1534]
 
Kabla ya wabunge kulipitisha hilo azimio la kumtoa Rais madarakani na kupiga kura, asubuhi yake tu Rais anawahi kulivunja bunge kwa kutumia Katiba.

Ndio upuuzi wa Katiba yetu.[emoji1534]
Na kwenye uchaguzi hao wabunge wanamkuta huyo rais ndo mwenyekiti wa chama hivyo majina yanakatwa LIVE.
 
Una mshitaki vipi na wapi MTU mwenye kings kikatiba.
Spika fomu zinapita kwa Mkiti CCM

NCHI HII TUNA MFUMO WAKISHETANI SANA.
Bora kuishi na korona siyo huu mfumo
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Back
Top Bottom