Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais Madarakani, lakini ni ngumu sana


..unajua Watz kwa muda mrefu tumefundishwa kwamba sisi si lolote au chochote mbele ya watawala.

..Yaani tumeaminishwa kwamba hatuna mamlaka yoyote mbele ya viongozi tunaowachagua kwenda kuongoza serikali inayoendeshwa kwa kodi zetu.

..Wabunge, ambao ni wawakilishi wetu na watunga sheria hawatekelezi jukumu lao la kuisimamia serikali.

..Badala yake wabunge wamegeuka kuwa ombaomba wa miradi ya maendeleo kwa viongozi wa serikali. Imani ya wabunge ni kwamba bila kuwa "ombaomba" mzuri basi jimbo husika linaweza lisipate miradi ya maendeleo.
 
Mkizingua analivunja bunge .....kura za maoni anawatosa wabunge wote kabisa watakuja wapya.....mna swali lingine nani atakuwa ameshinda? Qnawakamata wote ikiwemo Ndugai nabkundi lake anawapa kesi uhaini kutaka kupindua nchi kesi miaka 10 haijaisha.....muache choko choko
 
Aah, Kamanda: ulitaka iwe rahisi? Leo Rais, kesho hakuna. The makamo,arud8she Waarabu, then ASP, fyekelea mbali. Ni lazima iwe ngumu, siyo blabla za kina tundulissu na wasaliti k8na Zitto WB. Au Mdude Chadema pia anafaa nara mojamoja.
 
Mtu akiisoma katiba yetu yote kuna mawili atapata majibu:-
La kwanza sisi wananchi ndiyo wenye matatizo au kama siyo sisi basi maRais wetu wanaotutawala ndiyo huwa mwenye shida

Hii Katiba ishapitwa na wakati kabisa, kwanza ilitakiwa iwe replaced wakati tulivyoamua kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi 1992.
Katiba hii Rais anapewa mamlaka kama ya wale Wafalme wa kale.
 
Bunge lipi ?
 
Una mshitaki vipi na wapi MTU mwenye kings kikatiba.

Spika fomu zinapita kwa Mkiti CCM

NCHI HII TUNA MFUMO WAKISHETANI SANA.

Bora kuishi na korona siyo huu mfumo
Acha Ufala wewe Yaan Corona mi Afadhali utawala?.. Fala sanaa
 
Aah, Kamanda: ulitaka iwe rahisi? Leo Rais, kesho hakuna. The makamo,arud8she Waarabu, then ASP, fyekelea mbali. Ni lazima iwe ngumu, siyo blabla za kina tundulissu na wasaliti k8na Zitto WB. Au Mdude Chadema pia anafaa nara mojamoja.
Umeandika nini hapa?
 
Na Rais anaweza kulivunja bunge!

Na kila siku wabunge wa CCM wanatishwa kwamba Rais anaweza kulivunja bunge.

Sijawahi kusikia wabunge wakiambiwa wanaweza kumuondoa Rais madarakani.
Yule ndiyo mwenyekiti wao na Rais vilevile, pia hatuna mahakama tuna mashina ya CCM tupu
 
Kwa Hilo bunge linalotokana na kura za magumashi hakuna mbuge wa kuwajibisha raisi maana hawana ushawishi kwenye sanduku la kura
 
Mbona mwendazake alifanya hovyo Kika eneo hawakuona?

..waliona ila waliamini hali siyo mbaya kiasi cha wao kushindwa kuidhibiti.

..hali ingekuwa mbaya basi ungeona wanamuondoa kwa mtindo uliotumika Zimbabwe dhidi ya Mzee Mugabe.

..Au, wangetafuta mkakati wa kuachia madaraka ya kisiasa, bila kupoteza nguvu za kiuchumi , kama ilivyotokea Afrika Kusini walivyokubali utawala wa walio wengi.
 
Kwahiyo waliidhibiti?
 
Na kwenye uchaguzi hao wabunge wanamkuta huyo rais ndo mwenyekiti wa chama hivyo majina yanakatwa LIVE.
Na wakileta chokochoko wanamkuta ndye amiri jeshi wa majeshi yote nchini[emoji23][emoji1787]
 
Watanzania wengi hatuzijui haki zetu, na hata wachache wanaozijua wanaonekana kama hawajali. Juzi hapa Chahali kaanzisha mada muhimu sana kuhusu mjadala wa katiba mpya unaoendelea.

Alichoambulia humu ni kushambuliwa na matusi kibao. Tunao ujuaji mwingi usiotusaidia.
 

..kweli kabisa.

..haki za Watz zinakanyagwa na wale wanaozijua.

..halafu kuna mashabiki ambao wanaona Watz wenzao wakionewa halafu wanashangilia uonevu na uovu huo.
 
Na wakileta chokochoko wanamkuta ndye amiri jeshi wa majeshi yote nchini[emoji23][emoji1787]
Noma kinoma. Halafu waombe taarifa za kiitelijensia zisimfikie kwamba majamaa wanataka kukupigia kura za kukung'oa. Kuvunja hilo bunge itakuwa fasta tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…