PreGE2025 Bunge lirefushe madaraka ya Rais Samia ili kupisha Mageuzi ya kisheria na kikatiba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
897
Reaction score
559
Ni miaka zaidi ya 30 sasa imepita pale ambapo wanasiasa, wadau wa Demokrasia na wanaharakati walitaka kutokee kwa Mageuzi ya sheria za uchaguzi na Katiba ambayo yanahakisi mabadiliko ya kurejea kwa mfumo wa vyama vingi Nchini chini ya NCCR-Mageuzi, lengo la vuguvugu hili mpaka kinabadilishwa na kuwa chama cha siasa ilikuwa ni kuleta hayo Mageuzi ya kisheria na kikatiba ili tuweze kuwa na uwanja mpana na wa haki kati ya chama cha Mapinduzi na Upinzani.

Sasa miaka 30 imepita na NCCR-Mageuzi kabla chama hicho hakijafikia lengo hilo, na sasa vyama vingine kama CHADEMA na ACT Wazalendo vimerithi dhamana hii na sasa vyama hivi vilivyo serious na hasa hasa CHADEMA vinataka Mageuzi hayo ya kisheria na kikatiba kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 2025.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

CHADEMA iko makini na jambo hili wakiongozwa na kauli mbiu ya "No Reform no Election" sasa Watanzania wote imbeni "No Reform No Election"

Awali ACT Wazalendo iliyokuwa ikiongozwa na Ndugu Zitto Kabwe ilikubaliana kabisa na yale marekebisho ya kisheria ambayo tulipata Tume huru ya Uchaguzi INEC!, kwa sasa naona ACT Wazalendo inajaribu kubadili gia angani lakini kwa pamoja sisi Watanzania tunataka haya Mageuzi ya kisheria na kikatiba ili tuwe na haki sawa kati ya CCM na Upinzani, minzani haiko sawa wote tunalijua hilo.

CCM imekuwa ikitoa vitisho na kejeri kedekede kuhusu haya Mageuzi, huku vyombo vya dola vikijielekeza kuzima kabisa awareness ya Umma katika kudai haki zao za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kuwaonga wanaongoza Awareness hiyo, kuwatisha na hata kuwa-blackmail ili waachane na hizo harakati zao, Mfano mzuri ni NETO. CCM haitaki kwa dhati kabisa mabadiliko/Mageuzi haya kwa kudhani inajichimbia kaburi la sahau katika siasa zetu endapo uwanja wa kisiasa utakwa sawa kisheria na kikatiba.

Na hivyo sasa, kuelekea uchaguzi mkuu tumegawanyika mpaka sasa, vyama vidogo vidogo ambavyo vinakula na kuongwa na CCM na wanaCCM wenyewe wanasema twende kwenye uchaguzi kibabe na kwa vitisho kutoka CCM na vijibwa vyake, huku Upinzani ukiongozwa na CHADEMA na ACT Wazalendo wanasema bila Mageuzi ya kisheria na kikatiba hakuna uchaguzi, watauzuia na mimi nakubaliana nao kuwa tusiende kwenye uchaguzi kama hakuna Mageuzi ya dhati na ya kuaminika ya kisheria na kikatiba kama Nchi.

Na hii sasa inaleta mgogoro ambao kama siyo kutokea sasa utatokea kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, tuamini kuwa Tundu Lissu ni mwanasiasa makini ambaye anataka kuona kile anachopigania kinatokea, kwa namna hii hakuna haja ya kwenda kwenye uchaguzi kama Nchi tumegawanyika na tunalumbana lazima tukubaliane sote kwenda kwenye uchaguzi wa haki, wazi na huru.

Hivyo basi, Bunge letu lirefushe madaraka ya Rais Samia, ili kupisha Mageuzi haya ya kisheria na kikatiba kuepusha mgogoro kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, CHADEMA inasema tutazuia uchaguzi CCM na vijibwa vyake wasema hakuna wa kuzuia uchaguzi, hii si sahihi Tanzania ni yetu sote tukubaliane kama Nchi kutoka kwenye hili bila mgogoro wa kisiasa ambao unaweza kuleta mtikisiko mkubwa kwenye uchumi wetu hapo baadaye.

Rais Samia aongozewe muda wa madaraka na Bunge kwa miaka miwili ili sasa tukubaliane na tuzungumze kuhusu haya Mageuzi ya kisheria na kikatiba.

Kama tukienda kwenye uchaguzi kama inavyooneka sasa hakuna wa kumlaumu mwenzake katika hili, sote tutakuwa tumechangia kuleta mgogoro wa kisiasa na tutaitaji rasilimali nyingi kusuluhishana wakati uwezo wa kuamua kujitawala tunao sasa.

CCM iache kibri, ikubali twende kwenye Mageuzi makubwa ya kisheria na kikatiba ili tufanye uchaguzi wa haki, wazi na huru. Mageuzi ya kisheria na kikatiba hayatahusu mambo ya uchaguzi tu, bali mimi nimeona kuangazia tu kiasi kwenye eneo hili la Uchaguzi.

Tusogeze mbele uchaguzi.
 
Attachments

  • 20250318_211218.jpg
    20250318_211218.jpg
    140.2 KB · Views: 32
Mshasahau! Mlianza hivi hivi enzi za Jiwe, yule mbunge wa Nkasi pua kubwa, hata bungeni hakurudi kurefusha muda wa "JIWE".
 
Rais Samia aongozewe muda wa madaraka na Bunge kwa miaka miwili ili sasa tukubaliane na tuzungumze kuhusu haya Mageuzi ya kisheria na kikatiba.

Kama tukienda kwenye uchaguzi kama inavyooneka sasa hakuna wa kumlaumu mwenzake katika hili, sote tutakuwa tumechangia kuleta mgogoro wa kisiasa na tutaitaji rasilimali nyingi kusuluhishana wakati uwezo wa kuamua kujitawala tunao sasa.

Mkuu STOP this, huu ushauri wako ndio utakaoleta mgogoro, hata hio miaka miwili ikiisha bado Rais atataka aongezewe mingine kwa ajili ya kujipanga na jambo lingine tena na baadae atang'ang'ania madarakani.

Watanzania tuna desturi ya kufanya mazoea, ukishaweka sababu ambayo itafanya Rais aongezewe muda, basi kila muda utakapomalizika itatafutwa sababu nyingine.

Tanzania ni failed state, kichwa cha mwendawazimu kila mwanasisiemu anaona anaweza kujifunzia kunyoa.
 
Mshasahau! Mlianza hivi hivi enzi za Jiwe, yule mbunge wa Nkasi pua kubwa, hata bungeni hakurudi kurefusha muda wa "JIWE".
Jaribu kutofautisha.

Hoja ya wajinga wale kipindi cha Magufuli ilikuwa Katiba inadilishwe ili magufuli atawale milele.

Hoja ya sasa ni Bunge liahirishe uchaguzi kwa kipindi cha miaka 2 kupisha mabadiliko ya Katiba na Sheria za Uchaguzi. Hakuna shida yeyote kwenye hili.
 
Aongezewe miaka mitano ili upatikane muda mzuri wa kuandaa katiba mpya
 
Bunge letu lirefushe madaraka ya Rais Samia, il

Kumtegemea mtu ni hatari sana.

Hili suala halihitaji mtu bali watanzania wote wenye utashi na nia ya kweli kukamilisha reforms, wakae mezani kwa uwazi bila hila ya kubaki madaralani yeye binafsi au chama chake.

Ili akitokea mtu awe rais n.k akikengeuka akaenda kinyume na maagano ya kundi kubwa lenye nia njema bila kujali vyama tutaweza kumfokea kuwa amevunja maagano yetu na siyo maagano yake mtu mmoja.
 
Ni miaka zaidi ya 30 sasa imepita pale ambapo wanasiasa, wadau wa Demokrasia na wanaharakati walitaka kutokee kwa Mageuzi ya sheria za uchaguzi na Katiba ambayo yanahakisi mabadiliko ya kurejea kwa mfumo wa vyama vingi Nchini chini ya NCCR-Mageuzi, lengo la vuguvugu hili mpaka kinabadilishwa na kuwa chama cha siasa ilikuwa ni kuleta hayo Mageuzi ya kisheria na kikatiba ili tuweze kuwa na uwanja mpana na wa haki kati ya chama cha Mapinduzi na Upinzani.

Sasa miaka 30 imepita na NCCR-Mageuzi kabla chama hicho hakijafikia lengo hilo, na sasa vyama vingine kama CHADEMA na ACT Wazalendo vimerithi dhamana hii na sasa vyama hivi vilivyo serious na hasa hasa CHADEMA vinataka Mageuzi hayo ya kisheria na kikatiba kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 2025.

CHADEMA iko makini na jambo hili wakiongozwa na kauli mbiu ya "No Reform no Election" sasa Watanzania wote imbeni "No Reform No Election"

Awali ACT Wazalendo iliyokuwa ikiongozwa na Ndugu Zitto Kabwe ilikubaliana kabisa na yale marekebisho ya kisheria ambayo tulipata Tume huru ya Uchaguzi INEC!, kwa sasa naona ACT Wazalendo inajaribu kubadili gia angani lakini kwa pamoja sisi Watanzania tunataka haya Mageuzi ya kisheria na kikatiba ili tuwe na haki sawa kati ya CCM na Upinzani, minzani haiko sawa wote tunalijua hilo.

CCM imekuwa ikitoa vitisho na kejeri kedekede kuhusu haya Mageuzi, huku vyombo vya dola vikijielekeza kuzima kabisa awareness ya Umma katika kudai haki zao za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kuwaonga wanaongoza Awareness hiyo, kuwatisha na hata kuwa-blackmail ili waachane na hizo harakati zao, Mfano mzuri ni NETO. CCM haitaki kwa dhati kabisa mabadiliko/Mageuzi haya kwa kudhani inajichimbia kaburi la sahau katika siasa zetu endapo uwanja wa kisiasa utakwa sawa kisheria na kikatiba.

Na hivyo sasa, kuelekea uchaguzi mkuu tumegawanyika mpaka sasa, vyama vidogo vidogo ambavyo vinakula na kuongwa na CCM na wanaCCM wenyewe wanasema twende kwenye uchaguzi kibabe na kwa vitisho kutoka CCM na vijibwa vyake, huku Upinzani ukiongozwa na CHADEMA na ACT Wazalendo wanasema bila Mageuzi ya kisheria na kikatiba hakuna uchaguzi, watauzuia na mimi nakubaliana nao kuwa tusiende kwenye uchaguzi kama hakuna Mageuzi ya dhati na ya kuaminika ya kisheria na kikatiba kama Nchi.

Na hii sasa inaleta mgogoro ambao kama siyo kutokea sasa utatokea kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, tuamini kuwa Tundu Lissu ni mwanasiasa makini ambaye anataka kuona kile anachopigania kinatokea, kwa namna hii hakuna haja ya kwenda kwenye uchaguzi kama Nchi tumegawanyika na tunalumbana lazima tukubaliane sote kwenda kwenye uchaguzi wa haki, wazi na huru.

Hivyo basi, Bunge letu lirefushe madaraka ya Rais Samia, ili kupisha Mageuzi haya ya kisheria na kikatiba kuepusha mgogoro kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, CHADEMA inasema tutazuia uchaguzi CCM na vijibwa vyake wasema hakuna wa kuzuia uchaguzi, hii si sahihi Tanzania ni yetu sote tukubaliane kama Nchi kutoka kwenye hili bila mgogoro wa kisiasa ambao unaweza kuleta mtikisiko mkubwa kwenye uchumi wetu hapo baadaye.

Rais Samia aongozewe muda wa madaraka na Bunge kwa miaka miwili ili sasa tukubaliane na tuzungumze kuhusu haya Mageuzi ya kisheria na kikatiba.

Kama tukienda kwenye uchaguzi kama inavyooneka sasa hakuna wa kumlaumu mwenzake katika hili, sote tutakuwa tumechangia kuleta mgogoro wa kisiasa na tutaitaji rasilimali nyingi kusuluhishana wakati uwezo wa kuamua kujitawala tunao sasa.

CCM iache kibri, ikubali twende kwenye Mageuzi makubwa ya kisheria na kikatiba ili tufanye uchaguzi wa haki, wazi na huru. Mageuzi ya kisheria na kikatiba hayatahusu mambo ya uchaguzi tu, bali mimi nimeona kuangazia tu kiasi kwenye eneo hili la Uchaguzi.

Tusogeze mbele uchaguzi.
Iwapo ikiwa sii janja janja ya ccm ya wakati wote hata mimi nitaunga hilo mkono.
 
Kwa CCM hii hii tunayoijua? Rais na Bunge linaweza kubaki hata miaka 50 na kusitokee mabadiliko yo yote!
 
Mimi mwana-CCM kindakindaki; naunga mkono mageuzi. "No Reform No Election"
 
Kwani walio kuzaa wanasemaje na wewe kuendelea kuwa mtoto ukivaa pampasi mpaka sasa
 
Back
Top Bottom