Bunge lisijadili Mitaala ya Elimu, Wabunge wengi wana upeo mdogo

Bunge lisijadili Mitaala ya Elimu, Wabunge wengi wana upeo mdogo

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
18,585
Reaction score
16,780
Leo Bungeni wakati wa maswali na Majibu, Kuna swali lililohusu mabadiliko ya mitaala ya Elimu ili kuendana na hali ilivyo.

Naibu waziri wa elimu alikiri kuwa mfumo wetu wa Elimu uliopo haumsaidii Mhitimu kuweza kujiajiri hivyo wapo kwenye mchakato wa kubadilisha Mitaala inayotumika kukidhi soko.

Waziri alisema wanashirikiana na wadau mbalimbali kwenye kufanya mabadiliko hayo, bunge pia litashirikishwa kutoa mapendekezo yao.

Spika Ndugai akamwambia Waziri bunge lishiriki kwenye mchakato huo na siyo kuhusishwa kupitia makongamano.

Spika Ndugai anataka kila siku bungeni kutengwe muda maalumu kwa ajili ya wabunge kujadili na kupitisha marekebisho hayo ya Mtaala wa Elimu.

Ndugu Watanzania kwa aina ya Bunge hili lililopo kujadili na kupitisha mabadiliko ya Mitaala ya Elimu ni kuingiza majanga mengine makubwa kwenye Elimu ya Tanzania, Waziri wa Elimu na Wadau wengine pendeni watoto na wanafunzi wa Tanzania hii.

Kwa aina ya Bunge tulilo nalo sasa litajadili nini kuhusu Elimu?
Mfano, Mbunge anataka wafungwa na mahabusu waende na magodoro yao huko jela, huyu atachangia nini kwenye Mtaala wa Elimu?
 
Usihofu, bunge letu haliandai chochote, sio sheria wala sera. Wanapelekewa tu 'kujadili' na kupitisha. Wao ni rubber-stamp ya serikali.
Maneno ya Ndugai yamenifikirisha sasa hawa wakijadili mabadiliko ya mtaala wa Elimu ambao unahitaji mabadiliko makubwa itakuwaje?

Si lazima watoe boko tu!!
 
Wapo Wabunge Wenye uelewa Mpana wa maisha japo hawana makaratasi digrii.... Muhimu Sana washirikishwe kutoa maoni.Wasomi wengi hamnazo Wana kadiri na kukopi Mambo. Asasi za kitaifa pia Zina wadau wa kutosha, pia tupate uzoefu wenzetu waliotuacha bara Asia.
 
Hakuna bunge lolote duniani lenye uwezo wa kujadili sheria yeyote wao kama wabunge. Kinachofanyika ni watunga sheria ambao mara nyingi ni serikali ni kuwa convince wabunge kuwa sheria iliyopendekezwa ina manufaa kwa wananchi.
 
Sawa
 
Wapo Wabunge Wenye uelewa Mpana wa maisha japo hawana makaratasi digrii.... Muhimu Sana washirikishwe kutoa maoni.Wasomi wengi hamnazo Wana kadiri na kukopi Mambo. Asasi za kitaifa pia Zina wadau wa kutosha, pia tupate uzoefu wenzetu waliotuacha bara Asia.
Tunahitaji mapinduzi ya kweli kwenye mfumo wetu wa Elimu
 
Kama hili genge la wabunge likishirikishwa kwa namna yoyote ile kutengeneza mtaala wa elimu itakuwa ni janga kwa Taifa.

Bungeni kumejaa vilaza wa ajabu, elimu za kuungaunga, wale wenye elimu inayoeleweka nao ni watu wanafiki, wenye hila na waongo. Watu wa namna hiyo watatengeneza mtaala gani?

Kama tunataka kuwa na mtaala mzuri, tutafute wataalamu kutoka mataifa ya nje, hasa yale yaliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye elimu.
 
Back
Top Bottom