Bunge lisilo na meno na hatari ya kuuza akiba ya dhahabu

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
3,189
Reaction score
6,140
1/
Baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 uliogubikwa na damu, hofu na tuhuma nzito za kukosa haki, Tanzania imejikuta ikipoteza imani ya mataifa na mashirika mengi ya kimataifa. Matokeo yake? Misaada na ushirikiano wa kifedha kusimamishwa au kupunguzwa.

2/
Badala ya serikali kuwa wazi kwa wananchi kuhusu hali halisi ya uchumi na sababu za changamoto za kifedha, sasa tunaelezwa kuwa Benki Kuu inauza akiba ya dhahabu kwa madai kwamba “imevuka malengo ya uhifadhi.”

3/
Swali la msingi:
Je, kweli hii ni ziada ya kawaida?
Au ni hatua ya dharura kufidia pengo la fedha lililosababishwa na kusimamishwa kwa misaada ya nje?

4/
Akiba ya dhahabu ni bima ya taifa. Ni ngao ya uchumi wetu dhidi ya misukosuko ya ndani na ya kimataifa. Kuuza akiba hiyo bila mjadala wa wazi, bila uwazi wa takwimu, ni kuchezea mustakabali wa nchi.

5/
Katika nchi yenye mifumo imara ya kidemokrasia, maamuzi kama haya yangepitiwa kwa kina na BUNGE.
Lakini hapa kwetu, bunge liko kimya.

6/
Bunge ambalo lenyewe limepatikana kupitia uchaguzi unaotiliwa shaka kubwa kisheria na kimaadili, linawezaje kuwa na ujasiri wa kuisimamia serikali iliyolitengeneza?

7/
Bunge lisilo huru haliwezi:
– Kuitisha mawaziri wawajibike
– Kuhoji maamuzi hatarishi ya kiuchumi
– Kusimama upande wa maslahi ya wananchi

Hivyo linabaki kuwa muhuri wa maamuzi ya serikali, si chombo cha udhibiti.

8/
Tunapoona dhahabu ya taifa ikiuzwa, bila mjadala wa kitaifa, bila ridhaa ya wananchi, tunapaswa kujiuliza:
Je, tatizo ni dhahabu au ni uhalali wa uongozi?

9/
Uchumi hauharibiki kwa kukosa dhahabu, unaharibika kwa kukosa uaminifu, uwazi na uwajibikaji.
Na bunge lisilo na meno haliwezi kurejesha chochote kati ya hayo.
10/
Kimya cha bunge leo, ni mzigo kwa vizazi vijavyo.
Kuuza akiba ya dhahabu leo, ni kulipa gharama ya uongozi usio na ridhaa ya wananchi.

Mwisho:
Taifa linalouza akiba yake ya mwisho bila mjadala wa wazi, lina tatizo kubwa kuliko “ziada ya dhahabu.”
Lina tatizo la uhalali, uwajibikaji, na bunge lililoshindwa kuwa sauti ya wananchi.
 
Kwa mara ya kwanza Tz inauza gold reserve yake, ama kweli samuya anaupiga mwingi hadi kwenye matope!.
 
Bado haujasema mpaka useme na utasema tu yaani mpaka useme kwanini CCM mliipigia kura Milioni 32 Oktoba 29
 
ROSTAM AZIZI ANA CHUKUA DHAHABU YAKE KWENDA KUGAWANA NA RAIA FEKI WENZIE
 
Nafikiri uwekezaji kutoka nje, biashara, utalii umepungua kutokana na yale yaliyotekea 29/10.

Kuna shida kubwa serikali, nchi, watu wake wote, mihimili yake yote, vyombo vya ulinzi na usalama, rasilimali zake zote Samia kaziweka kwenye mfuko wake kwa kutumia hongo, vitisho, ubabe.

Tatizo letu ni mfumo Samia anaoutumia, ni mfumo sawa uliokuwa wa Hitler na Idd Amin. Ni mfumo unaotumiwa sana na mafia. Hakuna wa kumwambia kitu Don of dons, Boss wa maboss, hawajibiki kwa wananchi, bunge au yoyote. Yoyote anayetoa mawazo mbadala anatekwa, kuteswa, kupotezwa, kuchafuliwa.

Tatizo letu kubwa ni democratic deficit. Nchi ipo chini ya Mwanamke mwendawazimu. Tunaishi ndani ya Mafia state.

Ndio madhara ya kuwa chini ya Mafia state watu wanatekwa, kuteswa, kufichwa vituo vya polisi, mahabusu, safe houses, kupotezwa au kuuwawa mchana kweupe. Rasilimali zote ni za big don, Samia ana uwezo wa kuamua uishi au ufe, uwe uraiani au magereza.
 
Back
Top Bottom