Bunge litunge Sheria ili mali ambazo hazikuandikiwa wosia zimilikiwe na Serikali inapotokea mmiliki amefariki

Asante mkuu kwa kuleta mwongozo.

Kimsingi hapa kuna mkanganyiko. Mfano mtu ambaye ni muislam lakini kaacha wosia inashughulikiwaje?

Kwenye hili pendekezo sijazingatia sana mhusika atataka mirathi ifuate utaratibu gani. Nadhani hapa kila mtu apewe uhuru wa kuchagua anaandika wosia kwa kufuata utaratibu upi aidha kimila au kidini.

Hoja yangu kwenye bandiko ni kuiweka utaratibu wa kilazima kwa kila mtu kuandika wosia kulingana na matakwa mahususi yatakayowekwa na sheria yenyewe.
 
Mtoa mada Kuna SoMo linaitwa PROBATE AND ADMINISTRATION OF ESTATE, Ukiingia humor utasoma Probate and Administration of estate ACT, PROBATE rules,Indian succession act, Local customery declaration order of 1963,
 
Haki ya nani apate kiasi gani anayo mwenye mali mwenyewe. Anatakiwa tu afuate utaratibu wa sheria utakaowekwa.

Kukiwa na sheria ya kulazimisha kila mtu aandike wosia tutakuwa tumeruka kiunzi cha kwanza muhimu pindi mtu anapofariki.
 
Hiyo itasababisha serikali kuchukua Mali za watu hata kama yatakuwa na wosia wa mirathi
Hilo halitawezekana kirahisi kwasababu kutakuwa na utaratibu wa kimahakama na wosia unakuwa umehifadhiwa kwenye mfumo wa kielektoniki.
 
Huo wizi sasa mmefika mbali, serikali ije huko mitaani kushika vijumba kisa haina wosia,
Madam, sheria ikiwepo kila mtu ataandika wosia na hivyo hapatakuwa na matukio mengi ya serikali kukamata mali.
 
Mtoa mada Kuna SoMo linaitwa PROBATE AND ADMINISTRATION OF ESTATE, Ukiingia humor utasoma Probate and Administration of estate ACT, PROBATE rules,Indian succession act, Local customery declaration order of 1963,
Asante mkuu. Ungeweza kutupa highlights maana wengine ni ma-layman kwenye sheria.
 
Asante mkuu. Ungeweza kutupa highlights maana wengine ni ma-layman kwenye sheria.
Ndg Championship, naona unaamini sana utendaji ktk serikali yetu, kama vile u mgeni nchini. Mbn ni wengi tu wanalikataa hili pendkezo lako lkn umelivalia bango! Kubali tu kuwa Tz bado fikia level hiyo unayoitaka yaishe. Ni mengi tunataka ikiwa ni pamoja na katiba mpya lkn ...dah!
 
Kwa hiyo kama mzee ana nyumba na watoto, akifa ghafla bila wosia, serikali ichukue nyumba ifanye NHC,
Kwa waislamu wana taratibu zao za miradhi.
Tunaongelea serikali, Dini ni ya kwako binafsi

Kila mtu ana imani yake na Wengine hawana

Kama hutaki kufuata sheria za nchi anzisha nchi yako binafsi na ukaishi na sheria zako na Imani yako
 
Ehhh! Kwahiyo baba na mama wakifariki serekali ichukue nyumba Mali kwasababu hakuna wosia ndio unaona suluhisho? Na hao watoto itakuaje?
However tuna Mila na desturi zetu, pia tunasheria za dini na huo unaosema wosia unaweza kuwa wa maneno pia
 
Hapana, sheria itakuwa inataka aliyefariki awe ameacha wosia. Kama hakuacha na lake halipo.

Lengo ni kuwafanya wananchi waandike wosia. Na kimsingi itakuwa very rare kukuta mtu hajaandika wosia kama sheria itakuwepo.
Kama msemaji mmoja, aliyosema - sheria za mirathi katika dini ya kiislamu, hazina utata, uwe umeandika wosia au la! Kila mtu anayestahili kupata atapata fungu lake kihalali. Kwa hiyo basi, serikali iruhusu hii sheria ya kiislamu utumike kwa Nchi nzima (kwa watu wote).
Kumbuka haya nimapendekezo pia.
 
🤣🤣 Mkuu unataka kuanzisha mpambano na sisi wa imani nyingine?
 
Ni kawaida kwa binadamu wengi kupinga changes. Hata hivyo pendekezo hili halipingi utaratibu wa kimila na kidini. Unataka utaratibu wa kuandika wosia uwe lazima kisheria.
 
Ehhh! Kwahiyo baba na mama wakifariki serekali ichukue nyumba Mali kwasababu hakuna wosia ndio unaona suluhisho? Na hao watoto itakuaje?
However tuna Mila na desturi zetu, pia tunasheria za dini na huo unaosema wosia unaweza kuwa wa maneno pia
Kukiwa na sheria kuna mtu hataandika wosia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…