Research Solutions TZ
Member
- Jul 11, 2020
- 66
- 145
Wabunge wni wawakilishi wa wananchi ambao wapo kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi. Hii ni tafsiri ya kikatiba lakini kiuhalisia hali ni tofauti.
Niwakumbushe ndugu zangu kulikuwa na ongezeko la bei za vifurushi ambapo ni kelele za wananchi katika mitandao zilizofanya zile bei zishuke, aidha ni bunge ndilo lilipitisha bei zile za kuumiza.
Hivi sasa imepita tozo kwenye miamala ya simu ni wabunge wamepitisha, baada ya wananchi kupiga kelele mtandaoni, leo Julai 19 ndipo Rais amesema waangalie hilo suala.
Pia tupige kelele kabisa kuhusu tozo za kwenye muda wa hewani.
Point Yangu
Kwa kuwa wabunge wamekuwa wakitunga au kupitisha sheria kandamizi kwa wananchi badala ya kuwakilisha hali halisi ya walio mtaani ni vyema wasiwepo ili tujisimamie wenyewe kwa kuwa masuala mengi tumeweza kujisimamia
Aidha Tumeona wabunge wakililia ongezeko la mshahara ambao mshahara ghafi wao ni mara dufu ya mashahara wa mwalimu. Na ni wabunge hao hao ambao hawajui kazi yao bungeni na hubaki kuuliza chombo kipi cha kuiwajibisha serikali.
Katiba Mpya
Kwa hiyo niwape hoja mnaotaka katiba mpya kushauri bunge lisiwepo, tuwe na mawaziri ambao watapita kwa kura za wananchi kisha kuishauri serikali, hii tutaeppusha gharama kubwa inayotumika kila mwaka kulihudumia bunge
Tuungane kuwaambia bunge lisiwepo, tutajisemea wenyewe mtandaoni au kusemewa na Taasisi zisizo za kiserikali.
Nawasilisha