Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhani tuweke kipengele kwenye katiba bunge liwe live ili tumalize tatizo hili.Wito kwa TBC: Kwa vile nyinyi ndio watangazaji wa matangazo live ya Bunge, mfike mahali hayo matangazo ya Bunge Live, yawe " ring fenced", yafanywe ka ni right ya Watanzania kuangalia Bunge live na sio kama hisani, ili ili wakati wa kipindi cha Bunge, likija ombi jingine lolote la taasisi yoyote kuomba kutangaziwa live tukio lake, then waambiwe huu ni muda wa Bunge live na muda huo haupatikani kwa taasisi nyingine yoyote, na badala yake matangazo yao yaanze saa 5:00 asubuhi baada kipindi cha Bunge Live kumalizika.
Kitendo cha kupanga tukio jingine lolote litangazwe live kwa muda ule ule wa matangazo live ya Bunge, halafu matangazo ya Bunge yakakatishwa, kupisha matangazo ya tukio jingine, ni dharau kwa Bunge letu tukufu.