Wito kwa TBC: Kwa vile nyinyi ndio watangazaji wa matangazo live ya Bunge, mfike mahali hayo matangazo ya Bunge Live, yawe " ring fenced", yafanywe ka ni right ya Watanzania kuangalia Bunge live na sio kama hisani, ili ili wakati wa kipindi cha Bunge, likija ombi jingine lolote la taasisi yoyote kuomba kutangaziwa live tukio lake, then waambiwe huu ni muda wa Bunge live na muda huo haupatikani kwa taasisi nyingine yoyote, na badala yake matangazo yao yaanze saa 5:00 asubuhi baada kipindi cha Bunge Live kumalizika.