Bunge, Polisi na TRA ni taasisi zinazoongoza kuchukiwa na jamii nchini

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Bunge lipo pale kwa maslani yao na sio kwa maslahi ya wananchi, wabunge wanapitisha sheria nyingi zisizo wanufaisha wananchi moja kwa moja mfano Tozo na kujiongezea mishahara. Mbunge anayeonekana kuwa upande wa wananchi huundiwa kashifa za uongo na hata kusimamishwa vikao vya bunge.

Jeshi la polisi lenyewe halipo kwa ajili ya usalama wa wananchi lipo kwa usalama wa viongozi hasa wa kisiasa, linatuhumiwa kwa utekaji, kubambikia watu kesi, linatuhumiwa kwa ujambazi, linaongoza katika vitendo vya kunyanyasa wananchi mitaani na hasa vijijini polisi wanaonekana kama miungu watu, polisi inaongoza kwa rushwa nchini.

TRA ni taasisi inayolalamikiwa sana na wafanya biashara kwa kubambikia wafanyabiashara kodi na kupelekea wengi kufilisiwa. TRA inapendelea wafanyabiashara wakubwa na kuwakamua wale wadogo ambao ndio wengi.
 
Tuseme tu serikali nzima ya Samia inachukiwa sana ni basi tu...
 
Labda Bunge

Polisi na TRA wanatimiza majukumu yao kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi
Kwani bunge halipo kwa mujibu wa sheria, kila taasisi ipo pale kwa mujibu wa sheria tofauti huja pale watumishi wake wasipotimiza majukumu yao ama kwa makusudi ama shinikizo kutoka juu.
 
Ongezea mahakama, sisiem, tume ya uchaguzi
 
Wabunge posho zinawatia husda watu wanatamani posho zao
 
Kwani bunge halipo kwa mujibu wa sheria, kila taasisi ipo pale kwa mujibu wa sheria tofauti huja pale watumishi wake wasipotimiza majukumu yao ama kwa makusudi ama shinikizo kutoka juu.
Bunge linaendeshwa kwa kanuni tu

Sheria ni ya kuliasisi

Na ndio sababu hadi Leo haijulikani Kati ya Bunge na Taasisi ya urais nani mkubwa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ongeza na Task force, usalama, kikosi maalum cha utekaji. Mahakama, jela, halmashauri, wizara kama ya ardhi, katiba na sheria.
 
Bunge linaendeshwa kwa kanuni tu

Sheria ni ya kuliasisi

Na ndio sababu hadi Leo haijulikani Kati ya Bunge na Taasisi ya urais nani mkubwa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kila taasisi ina kanuni zake bwashee, polisi wana PGO, TRA ndio usiseme.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…