johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 104,319
- 183,639
haya tusubiri wamekusikiaBunge la sasa ndio linamaliza muda wake na linategemewa kuvunjwa rasmi mwezi June panapo majaliwa.
Tumeshuhudia bunge hili likipoteza wabunge wengi kwa kufukuzwa na huenda likawa limeweka historia ya nahodha kuwatosa mabaharia baharini.
Yote kwa yote maisha bado yanaendelea baada ya siasa.
Leo natoa tu angalizo kwa bunge lijalo bila kujali Spika atakuwa Zungu, Chenge au Tulia, kwamba chonde chonde bunge ni mali ya wananchi.
Uongozi ni dhamana tu sisi wananchi tunataka wabunge wote wapate haki kwa usawa, tena walindwe na kuongozwa vyema mbunge kufukuzwa liwe ni swala la mchakato na siyo uamuzi wa mtu mmoja mnatutia hasara walipa kodi.
Spika siyo Nabii au mtume anayemiliki Huduma ya kichungaji ambaye yeye ni alpha na omega bali Spika ni mtumishi wa wananchi.
Mwenye enzi Mungu alibariki bunge lijalo.
Maendeleo hayana vyama!
Mtu unaweza kuwa na bonge la kichwa halafu Akiri ni ziro, ni kama mtoa mada,unapoint lakini sikuona sababu ya msingi kufananisha na walokole. sema ni vile tu walokole wako peace maana ingekua upande wa pili kungekua kunawaka moto cha msingi ni kuheshimu dini za watu
Umesahau kuwa alishapewa maagizo ya namna gani kuliendesha Bunge?? Umesahau ule msemo wa kuna Mhimili uliojichimbia chini zaidi ya mingine??Tatizo ni katiba inayompa rais madaraka makubwa, kiasi kwamba tabia binafsi za rais ndio zinaamua mienendo na utendaji wa taasisi za umma. Huyo spika ameamua kuiga kila tabia binafsi za rais na kuzipeleka kwenye bunge, kwani anajua akijipendekeza kwa rais, atapewa tena ubunge na hatimaye uspika.
Kwani mzee Mgaya hajatoa maoni yake juu ya hilo?Bunge la sasa ndio linamaliza muda wake na linategemewa kuvunjwa rasmi mwezi June panapo majaliwa.