3 Aug 2021
Lusinde: Awajibu wanaosema wabunge hawalipi kodi/ ataja mshahara wake hadharani
Mbunge wa Mvumi, Mh. Livingstone Lusinde amevunja ukimya na kutaja mshahara wake hadharani lakini akasema wanaotaka ubunge wasubiri 2021.
Lusinde ametoa Kauli alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma ambapo amemtaja aliyekuwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Ottouh kuwa anafanya mambo ya kukurupuka hivyo anadanganya Watanzania.
Mheshimiwa Livingstone Lusinde awasomea mapato ya kuwa mbunge mbele ya waandishi wa habari na kubainisha kilichoandikwa ktk salary slip yake:
- Mshashara shs. 4,600,000
- Kodi kwa mwezi shs. 1,210,500
- Posho......?
- Jimbo....?
- Msaidizi ofisi .....?
- Mafuta ya gari...?
- Dereva...?
- Mkopo wa gari ....?
- Kodi ya nyumba Dodoma ....?
- Bima ya afya ....?
Source : Mwananchi Digital
N. B
https://www.tra.go.tz › swahili › paye
Mamlaka ya Mapato Tanzania - Kodi ya Mapato yatokanayo na Ajira
Mwajiri anapaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika mishahara, ujira na malipo mengine yote yanayopaswa kukatwa kodi kutoka kwa waajiriwa.
Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira?
Faida zinazohusishwa katika kukokotoa mapato kutoka katika ajira
Mapato ya ajira yanahusisha;
a) malipo ya ujira, mshahara, malipo ya likizo, ada, kamisheni, bonasi, kiinua mgongo au posho yoyote ya safari, burudani au malipo mengine yoyote yanayohusiana na ajira au huduma inayotolewa.
b) Malipo yanayoonesha msamaha au marejesho ya matumizi ya mtu binafsi au mtu mwingine anayehusiana na mtu huyo.
c) malipo kwa mkataba wa mtu binafsi katika masharti yoyote ya ajira
d) michango na malipo ya kustaafu
e) malipo ya kupunguzwa, kupoteza au kufukuzwa kazi
f) malipo mengine yanayolipwa yanayohusiana na ajira ikiwa ni pamoja malipo yasiyokuwa ya fedha yanayopatikana kwa mujibu wa sheria
g) Malipo mengine kama itakavyoonekana yanahitaji kuhusishwa
h) malipo ya mwaka anayolipwa mkurugenzi tofauti na malipo yake ya kawaida kama mkurugenzi
Mapato yasiyohusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira
Mapato yafuatayo hayatahusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira:
(a) Kiasi kilichosamehewa na malipo ya mwisho ya zuio;
(b) Huduma za kafeteria zinazotolewa bila ubaguzi;
(c) Huduma za afya, malipo ya huduma za afya na malipo ya bima kwa huduma za afya ikizingatiwa kwamba huduma au malipo hayo:
(i) Yanapatikana ili kukidhi matibabu ya mhusika, mwenza wake na hadi watoto wao wanne; na
(ii) yanawezeshwa kupatikana na mwajiri (na mtu yeyote anayehusiana na mwajiri anayeendesha biashara kama hiyo au inayohusiana na hiyo) katika misingi isiyo ya kiubaguzi;
(d) Posho yoyote ya kujikimu, safari, burudani au posho nyingine zinazohusisha urudishaji wa gharama kwa mnufaika kwa kiwango chochote alichotumia na kisichohusiana na uzalishaji wa kipato chake katika ajira au huduma inayotolewa;
(e) Faida inayotokana na matumizi ya chombo cha moto ambapo mwajiri hadai kufanya makato yoyote au nafuu kuhusiana na umiliki, matengenezo au uendeshaji wa chombo cha moto;
(f) Faida inayotokana na matumizi ya maeneo ya makazi kwa mwajiriwa wa serikali au taasisi nyingine ambayo bajeti yake haitokani na ruzuku inayotolewa na serikali;
(g) malipo ya safari kwa mwajiriwa, mwenza wake, na hadi watoto wanne kwenda na kurudi eneo la kazi, yanayoendana na gharama halisi za usafiri ikiwa mwajiriwa anaishi zaidi ya maili 20 kutoka katika kituo chake cha kazi na ameajiriwa kutoa huduma kwa mwajiri katika eneo la kazi;
(h) Mchango na malipo ya kustaafu yanayosamehewa chini ya sheria ya Huduma za jamii za Mafao ya Kustaafu
(i) Malipo yasiyokuwa na sababu za msingi au yasiyotekelezeka kiutawala kwa mwajiri kuyajengea hoja au kuelekeza kwa wanufaika wao;
(j) Posho inayolipwa kwa mwajiriwa anayetoa huduma binafsi ndani ya taasisi kwa wagonjwa katika hospitali za umma; na
(k) Posho ya nyumba, usafiri, uwajibikaji, kazi za ziada, kazi za muda wa ziada (ajari), mazingira magumu, na honoraria inayolipwa kwa waajiriwa wa serikali au taasisi, bajeti ambayo inalipwa yote au sehemu yake na ruzuku ya bajeti ya serikali
Source :
Mamlaka ya Mapato Tanzania - Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira?