Bunge: Wabunge wanakatwa kodi zote stahiki ikiwemo 'PAYE''

Bunge: Wabunge wanakatwa kodi zote stahiki ikiwemo 'PAYE''

Hawa watu wana dharau sana.......
Zama zimebadilika sana watu wana taarifa zote....
Kila mtu ashinde mechi zake....
 
Wabunge wanakatwa kodi kwenye mishahara kama kawaida, hilo ni kweli.

Shida iko kwenye posho, wabunge wameweka mshahara mdogo wa 3m halafu wameweka posho nyingi karibu 9m ambazo hazikatwi kodi.

Lengo hasa la kuweka posho ama marupurupu mengine mengi ni kukwepa kodi. Posho halikatwi kodi.

Tunachotaka ni hizo posho zote ziingie kwenye mshahara ili ukatwe kodi.
Wahujumu uchumi hawa.
 
Kutoka maktaba

15 Jun 2016

Kama mnatukata kodi mkateni hadi Rais '-Mbunge Hussein Bashe

Wakati mjadala wa kuijadili bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2917 mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe amesimama bungeni kusisitiza kama serikali imeamua kuwakata kodi wabunge basi ihakikishe inatekeleza hilo kwa viongozi wote bila kubagua.

source : Millard Ayo

Kwahiyo Jerry Silaa alivyoongea juzi ni chizi? mbunge ana posho ya miliono 9 ambayo haikatwi kodi
 
3 Aug 2021

Lusinde: Awajibu wanaosema wabunge hawalipi kodi/ ataja mshahara wake hadharani

Mbunge wa Mvumi, Mh. Livingstone Lusinde amevunja ukimya na kutaja mshahara wake hadharani lakini akasema wanaotaka ubunge wasubiri 2021.

Lusinde ametoa Kauli alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma ambapo amemtaja aliyekuwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Ottouh kuwa anafanya mambo ya kukurupuka hivyo anadanganya Watanzania.

Mheshimiwa Livingstone Lusinde awasomea mapato ya kuwa mbunge mbele ya waandishi wa habari na kubainisha kilichoandikwa ktk salary slip yake:
  • Mshashara shs. 4,600,000
  • Kodi kwa mwezi shs. 1,210,500
  • Posho......?
  • Jimbo....?
  • Msaidizi ofisi .....?
  • Mafuta ya gari...?
  • Dereva...?
  • Mkopo wa gari ....?
  • Kodi ya nyumba Dodoma ....?
  • Bima ya afya ....?
Source : Mwananchi Digital

N. B

Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira?​

Faida zinazohusishwa katika kukokotoa mapato kutoka katika ajira
Mapato ya ajira yanahusisha;
a) malipo ya ujira, mshahara, malipo ya likizo, ada, kamisheni, bonasi, kiinua mgongo au posho yoyote ya safari, burudani au malipo mengine yoyote yanayohusiana na ajira au huduma inayotolewa.
b) Malipo yanayoonesha msamaha au marejesho ya matumizi ya mtu binafsi au mtu mwingine anayehusiana na mtu huyo.
c) malipo kwa mkataba wa mtu binafsi katika masharti yoyote ya ajira
d) michango na malipo ya kustaafu
e) malipo ya kupunguzwa, kupoteza au kufukuzwa kazi
f) malipo mengine yanayolipwa yanayohusiana na ajira ikiwa ni pamoja malipo yasiyokuwa ya fedha yanayopatikana kwa mujibu wa sheria
g) Malipo mengine kama itakavyoonekana yanahitaji kuhusishwa

h) malipo ya mwaka anayolipwa mkurugenzi tofauti na malipo yake ya kawaida kama mkurugenzi

Mapato yasiyohusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira

Mapato yafuatayo hayatahusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira:
(a) Kiasi kilichosamehewa na malipo ya mwisho ya zuio;
(b) Huduma za kafeteria zinazotolewa bila ubaguzi;
(c) Huduma za afya, malipo ya huduma za afya na malipo ya bima kwa huduma za afya ikizingatiwa kwamba huduma au malipo hayo:
(i) Yanapatikana ili kukidhi matibabu ya mhusika, mwenza wake na hadi watoto wao wanne; na
(ii) yanawezeshwa kupatikana na mwajiri (na mtu yeyote anayehusiana na mwajiri anayeendesha biashara kama hiyo au inayohusiana na hiyo) katika misingi isiyo ya kiubaguzi;
(d) Posho yoyote ya kujikimu, safari, burudani au posho nyingine zinazohusisha urudishaji wa gharama kwa mnufaika kwa kiwango chochote alichotumia na kisichohusiana na uzalishaji wa kipato chake katika ajira au huduma inayotolewa;
(e) Faida inayotokana na matumizi ya chombo cha moto ambapo mwajiri hadai kufanya makato yoyote au nafuu kuhusiana na umiliki, matengenezo au uendeshaji wa chombo cha moto;
(f) Faida inayotokana na matumizi ya maeneo ya makazi kwa mwajiriwa wa serikali au taasisi nyingine ambayo bajeti yake haitokani na ruzuku inayotolewa na serikali;
(g) malipo ya safari kwa mwajiriwa, mwenza wake, na hadi watoto wanne kwenda na kurudi eneo la kazi, yanayoendana na gharama halisi za usafiri ikiwa mwajiriwa anaishi zaidi ya maili 20 kutoka katika kituo chake cha kazi na ameajiriwa kutoa huduma kwa mwajiri katika eneo la kazi;
(h) Mchango na malipo ya kustaafu yanayosamehewa chini ya sheria ya Huduma za jamii za Mafao ya Kustaafu
(i) Malipo yasiyokuwa na sababu za msingi au yasiyotekelezeka kiutawala kwa mwajiri kuyajengea hoja au kuelekeza kwa wanufaika wao;
(j) Posho inayolipwa kwa mwajiriwa anayetoa huduma binafsi ndani ya taasisi kwa wagonjwa katika hospitali za umma; na
(k) Posho ya nyumba, usafiri, uwajibikaji, kazi za ziada, kazi za muda wa ziada (ajari), mazingira magumu, na honoraria inayolipwa kwa waajiriwa wa serikali au taasisi, bajeti ambayo inalipwa yote au sehemu yake na ruzuku ya bajeti ya serikali
Source : Mamlaka ya Mapato Tanzania - Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa ‘ itokanayo na Ajira?

Halafu wanatuambia hawana vyanzo vya mapato wakati ‘benefits in kind’ zote hizo nchi wenzetu unalipa income tax.

Nyumba kama unakaa bure utalipa 10% ya market value kwa mwaka kutoka kwenye mshahara wako.

Thamani ya gari unalotumia utalipa 3-5% kwa mwaka kutoka kwenye mishahara wako.

Mafuta kwa mwaka utalipa percent kadhaa kwa kutoka kwenye mshahara wako.

Posho zote zitajumlishwa na mapato yako mengine utalipa income tax kwa mwaka.

Mwigulu unavyanzo vingi vya mapato acha kukamua maskini na boresha makusanyo kama ilivyokuwa awamu iliyopita.

Kuna waajiriwa wengi awalipi kodi stahiki nchi kulingana na nchi nyingine duniani.
 
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (PAYE) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.

Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Mimi ninadhani kuwapigia kelele hawa jamaa kuhusu ulipaji kodi yaweza isiwe dawa. Kodi huuma pale ambapo una mshahara kiduchu au kazi yako haina namna yoyote ya kuongeza kipato zaidi ya mshahara.

Sasa hawa jamaa wanaweza kulipishwa kodi, je, posho na marupurupu watakazojipa tutazijua? Wanaweza kupaisha huko kwenye maslahi mengine ikawa balaa zaidi.

Kinachotakiwa ni uungwana tu. Kulipwa kulingana na kipato cha nchi ili kupunguza imbalances
 
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (PAYE) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.

Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Kama wabunge wenyewe wanakili hawalipi Kodi tena wabunge wasomi wa sheria kama Jerry silaa alafu Leo mnataka kutuaminisha kua mnalipa Kodi. Lipeni Kodi kwa hizo 9m ambazo ni posho kama wazalendo
 
Hawa wanatumia ujanja wa kujificha kwenye mujibu wa sheria

Hela zote wanazopata kwa mwezi ni karibu 12milion.

Hapo iliyoandikwa mshahara ni milion 3 tu

Zingine zote wanaziita posho ili zikwepe kodi.

Milion 9 yote posho tu
Hata posho kwa mujibu wa sheria zinapaswa zikatwe kodi.
 
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (PAYE) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.

Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Nani amini matamko ya hii serikali haramu
 
Kwani hiki kikaratasi walichoprint ndio kinatosha kuwa ushahidi wanakatwa Kodi?

Waache maigizo!
 
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (PAYE) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.

Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Mbona ni PAYE tu muheshimiwa jobo? Vipi mifuko ya Jamii!! Bima ya afya na pspf mnakatwa au ni PAYE tu?? Nyoosha maelezo vizuri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabunge wanaficha kipato chao na kutuonesha mshahara tu, pengine hawaelewi maana ya neno kipato?

Kama ni hivyo basi wasome hapa TRA wanazungumzia nini kuhusu mapato yatokanayo na ajira:

Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira?

Faida zinazohusishwa katika kukokotoa mapato kutoka katika ajira
Mapato ya ajira yanahusisha;
a) malipo ya ujira, mshahara, malipo ya likizo, ada, kamisheni, bonasi, kiinua mgongo au posho yoyote ya safari, burudani au malipo mengine yoyote yanayohusiana na ajira au huduma inayotolewa.
b) Malipo yanayoonesha msamaha au marejesho ya matumizi ya mtu binafsi au mtu mwingine anayehusiana na mtu huyo.
c) malipo kwa mkataba wa mtu binafsi katika masharti yoyote ya ajira
d) michango na malipo ya kustaafu
e) malipo ya kupunguzwa, kupoteza au kufukuzwa kazi
f) malipo mengine yanayolipwa yanayohusiana na ajira ikiwa ni pamoja malipo yasiyokuwa ya fedha yanayopatikana kwa mujibu wa sheria
g) Malipo mengine kama itakavyoonekana yanahitaji kuhusishwa

h) malipo ya mwaka anayolipwa mkurugenzi tofauti na malipo yake ya kawaida kama mkurugenzi
Source :
 
Mimi ninadhani kuwapigia kelele hawa jamaa kuhusu ulipaji kodi yaweza isiwe dawa. Kodi huuma pale ambapo una mshahara kiduchu au kazi yako haina namna yoyote ya kuongeza kipato zaidi ya mshahara. Sasa hawa jamaa wanaweza kulipishwa kodi, je, posho na marupurupu watakazojipa tutazijua? Wanaweza kupaisha huko kwenye maslahi mengine ikawa balaa zaidi.

Kinachotakiwa ni uungwana tu. Kulipwa kulingana na kipato cha nchi ili kupunguza imbalances
Yani izo milioni 12 zote zikatwe kodi mkuu! Mimi nimeona salary slip ya mtu wangu wa karibu yani basic inajumlishwa na posho nyingine ndo inakatwa kodi mkuu... Imagine na uyu ni mtumishi wa kawaida kabisa kwann wao basic tu ndo inakatwa kodi hii si sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa kuhusu Waheshimiwa Wabunge kukatwa Kodi .

Ofisi ya Bunge la Tanzania imesema kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa Umma pamoja na Viongozi wa Kisiasa, Wabunge wanakatwa Kodi ikiwemo ya Mapato (PAYE) inayokatwa kwenye Mishahara yao kwa mujibu wa Sheria.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa zinazodai Wabunge hawalipi Kodi kwenye Mishahara kusambaa Mitandaoni.

Zaidi, soma: Jerry Silaa: Wabunge tuanze kukatwa kodi kwenye Mishahara yetu
Weka pay slip
 
Back
Top Bottom