Justification ya accounting practice ni sheria ya nchi kwa mujibu wa maelekezo ya TRA.
Umewekewa hii link
Mamlaka ya Mapato Tanzania - Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira? kupitia post #39
All the necessary listed employment related income is subject to taxation. Na kiasi kikubwa cha marupurupu ya wabunge kinaangua kwenye kodi.
Vitu vingi vilivyosamehewa ni ‘benefits in kind’ ambapo kwa asilimia kubwa wanapata senior civil servant. Which is absurd sheria inatakiwa ibadilishwe wachangie kiasi uwezi kutoa vitu vyote vile bure.
Mapato yasiyohusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira
Mapato yafuatayo hayatahusishwa katika kukokotoa kodi inayotokana na ajira:
(a) Kiasi kilichosamehewa na malipo ya mwisho ya zuio;
(b) Huduma za kafeteria zinazotolewa bila ubaguzi;
(c) Huduma za afya, malipo ya huduma za afya na malipo ya bima kwa huduma za afya ikizingatiwa kwamba huduma au malipo hayo:
(i) Yanapatikana ili kukidhi matibabu ya mhusika, mwenza wake na hadi watoto wao wanne; na
(ii) yanawezeshwa kupatikana na mwajiri (na mtu yeyote anayehusiana na mwajiri anayeendesha biashara kama hiyo au inayohusiana na hiyo) katika misingi isiyo ya kiubaguzi;
(d) Posho yoyote ya kujikimu, safari, burudani au posho nyingine zinazohusisha urudishaji wa gharama kwa mnufaika kwa kiwango chochote alichotumia na kisichohusiana na uzalishaji wa kipato chake katika ajira au huduma inayotolewa;
(e) Faida inayotokana na matumizi ya chombo cha moto ambapo mwajiri hadai kufanya makato yoyote au nafuu kuhusiana na umiliki, matengenezo au uendeshaji wa chombo cha moto;
(f) Faida inayotokana na matumizi ya maeneo ya makazi kwa mwajiriwa wa serikali au taasisi nyingine ambayo bajeti yake haitokani na ruzuku inayotolewa na serikali;
(g) malipo ya safari kwa mwajiriwa, mwenza wake, na hadi watoto wanne kwenda na kurudi eneo la kazi, yanayoendana na gharama halisi za usafiri ikiwa mwajiriwa anaishi zaidi ya maili 20 kutoka katika kituo chake cha kazi na ameajiriwa kutoa huduma kwa mwajiri katika eneo la kazi;
(h) Mchango na malipo ya kustaafu yanayosamehewa chini ya sheria ya Huduma za jamii za Mafao ya Kustaafu
(i) Malipo yasiyokuwa na sababu za msingi au yasiyotekelezeka kiutawala kwa mwajiri kuyajengea hoja au kuelekeza kwa wanufaika wao;
(j) Posho inayolipwa kwa mwajiriwa anayetoa huduma binafsi ndani ya taasisi kwa wagonjwa katika hospitali za umma; na
(k) Posho ya nyumba, usafiri, uwajibikaji, kazi za ziada, kazi za muda wa ziada (ajari), mazingira magumu, na honoraria inayolipwa kwa waajiriwa wa serikali au taasisi, bajeti ambayo inalipwa yote au sehemu yake na ruzuku ya bajeti ya serikali
Ukisoma kwa nia njema bila kusukumwa na CHOYO, MAONO MAFUPI NA AKILI MBOVU utagundua kuwa posho wanazolipwa wabunge hazipaswi kukatwa kodi
Mbunge anapewa 800, 000. za kulipa wafanyakazi wa ofisi yake ikikatwa kodi atawalipa nini?