Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Amenishangaza mama mmoja mjumbe wa bunge la katiba aliposema kuwa nchi ambazo zimekuwa zikipiga kura ya siri kupitisha katiba zao ni nchi za mashoga. Ameyasema hayo leo alipokuwa akipinga upigaji wa kura za siri wakati wa kupitisha rasimu ya katiba kufuatia mifano iliyotolewa na mjumbe mwingine aliyekuwa akitaka kura zipigwe kwa siri na kutoa mifano ya nchi mbali mbali zilizopiga kura za siri wakati wa kupitisha katiba zao. Profesa Safari alimtaka yule mama atoe ushahidi na kama hana aombe radhi na kufuta kauli yake. Mwenyekiti wa muda Bw Pandu Kificho hakumpa nafasi yule mama kutoa ushahidi au kuomba radhi badala yake alisema wajumbe wawe makini kujadili mambo ili waepushe mjadala kwenda kwenye mambo mengine.