Bungeni, Dodoma: Wazalishaji/Wasambazaji waelekezwa kushusha bei za bidhaa muhimu

Bungeni, Dodoma: Wazalishaji/Wasambazaji waelekezwa kushusha bei za bidhaa muhimu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Serikali imeagiza Wazalishaji na Wasambazaji wa bidhaa muhimu kushusha mara moja bei za bidhaa zinazopandishwa pasipo kuendana na uhalisia wa Soko.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za uhaba na upandaji wa bei usioendana na uhalisia wa Soko kwenye bidhaa za Ujenzi, Vyakula, Nishati na pembejeo za Kilimo.

Amesema, hatua mbalimbali zimechukuliwa kukabiliana na hali hiyo ikiwemo Usimamiaji wa Sheria za Ushindani na kutafuta vyanzo mbadala vya upatikanaji wa bidhaa.
 
Eti maagizo ya kupunguza bei!mara ngapi mnafanya huu mchezo kuwalaghai raia?
 
Mzeee wa tamko..... Ila kufuatilia ndio mtihani
Serikali imeagiza Wazalishaji na Wasambazaji wa bidhaa muhimu kushusha mara moja bei za bidhaa zinazopandishwa pasipo kuendana na uhalisia wa Soko...
 
Kosa lilishafanyika tangu awali. Wanatakiwa kuandaa price list ya bidhaa zote ambazo zimepanda bei na kuziweka public
 
Hakuna lolote litakaloenda kutendeka...hii nchi viongozi ni ni waimba ngonjera Sana..

Bibi ushungi- tegemeeni bidhaa kupanda kutokana na Vita vya Ukraine..

PM- tunawataka wafanyabiashara kupunguza Bei za bidhaa na vifaa vya ujenzi.

Yaani hii serikari inajipiga kidole afu inanusa yenyewe...
 
Inflation ni dunia nzima kwa sasa, ondoeni tozo kama mnamaanisha sio porojo tuu
 
Majaliwa hata kama mtupu wa Uchumi angeingia au atume wasaidizi wake google apate knowledge kidogo jinsi fiscal policy and government spending zinavyoweza kupunguza inflation ndio aje atudanganye na kaspeech kake, hii ya kulaumu wafanyabiashara anaonekana mtupu zaidi
 
Hatuzalishi chochote, nishati tunaagiza almost 100%, chakula unaweza kufikiri tunazalisha kumbe tunaagiza kuliko tunachozalisha,tunaagiza mpaka chupi na viberiti acha inflation itupige tuu labda tutapata akili ya kuzalisha wenyewe
 
Back
Top Bottom