Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Uchukuzi kuendelea kulisimamia kwa karibu Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuhakikisha huduma za treni ya SGR zinaboreshwa.
Pia, Majaliwa ameagiza miundombinu ya mradi huo inaimarishwa ili uweze kudumu kwa muda mrefu. Kauli ya Majaliwa inakuja wakati baadhi ya wadau wakiwemo watumiaji wa usafiri huo wakipongeza huku wengine wakilalamikia huduma duni ndani ya usafiri huo.
Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro, ilibaini kuwepo kwa baadhi ya abiria wanaohujumu mradi huo kwa kulipa nauli pungufu na kuishauri TRC hatua za kuchukua kudhibiti hali hiyo.
Waziri Mkuu Majaliuwa amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali itaendeleza sekta ya uchukuzi ambapo pamoja na mambo mengine itasimamia sekta ya reli ikiwemo ujenzi wa SGR na uendeshaji wake kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.
Pia Soma
Utendaji wa Train ya SGR uboreshwe