Bungeni Leo: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa maelekezo mapya uendeshaji wa treni ya SGR

Bungeni Leo: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa maelekezo mapya uendeshaji wa treni ya SGR


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Uchukuzi kuendelea kulisimamia kwa karibu Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuhakikisha huduma za treni ya SGR zinaboreshwa.

Pia, Majaliwa ameagiza miundombinu ya mradi huo inaimarishwa ili uweze kudumu kwa muda mrefu. Kauli ya Majaliwa inakuja wakati baadhi ya wadau wakiwemo watumiaji wa usafiri huo wakipongeza huku wengine wakilalamikia huduma duni ndani ya usafiri huo.

Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro, ilibaini kuwepo kwa baadhi ya abiria wanaohujumu mradi huo kwa kulipa nauli pungufu na kuishauri TRC hatua za kuchukua kudhibiti hali hiyo.

Waziri Mkuu Majaliuwa amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali itaendeleza sekta ya uchukuzi ambapo pamoja na mambo mengine itasimamia sekta ya reli ikiwemo ujenzi wa SGR na uendeshaji wake kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

Pia Soma
Utendaji wa Train ya SGR uboreshwe
Acha ujinga mkuu.. hatuokoti mabundle
 
..Sgr inapaswa kuwa ya MIZIGO.

..biashara ya abiria itabidi shirika lipewe ruzuku.

..na nimeona kuna matumizi yasiyo ya lazima ikiwemo kuajiri mamia ya wahudumu
ktk treni.
We jamaa vipi aisee una mambo ya kizee sana.

Watu tunataka tuogeshwe na warembo huko kwenye treni unaleta mambo yako ya ufipa hapa.
 
We kariri tu mambo ya mabusi basi pale kuna watu wamekata kupitia mitandaoni na wakawa wamepanga foleni waiprint iwe kwenye mfumo wa ticket ya karatasi sasa kama unaona tunajitakia lipia hapo kwenye simu alafu nenda
Kwanza kajifunze maana ya kukariri,usipende kudandia maneno. Nikirudi kwenye mada nimesema hilo jambo serikali ina uwezo kabisa wa kuweka mfumo mzuri na rafiki ili kuondoa foleni na kuokoa muda,wana kila kitu kuanzia utaalamu mpaka uwezeshaji. Mfano wanaweza kutengeneza electric kadi kama za mwendo kasi na zikawa zinauzwa siyo tuu hapo stesheni bali hata kwa maajenti au Maduka yenye vigezo. Unanua kadi popote unaweka pesa then ukifika stesheni ni kuchanja tuu unaenda zako.
 
Back
Top Bottom