Bungeni live: Ufafanuzi wa hoja za wajumbe kuhusiana na rasimu.

Bungeni live: Ufafanuzi wa hoja za wajumbe kuhusiana na rasimu.

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,149
Reaction score
3,825
WanaJF

Bunge linaendelea hivi sasa na limeanza kwa kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizo tolewa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba.

Kamati iliyokuwa ikiratibu uandaaji wa rasimu ya kanuni za bunge maalumu la katiba imeanza kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuhusiana na kanuni za bunge hilo.

UFAFANUZI WA AKIDI:

Moja ya hoja zilizo pendekezwa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba ni kuhusu suala la AKIDI. Awali kamati ilipendekeza walau idadi ya wajumbe kutoka bara iwe 2/3 na ile kutoka Zanzibar iwe 1/3 ili kuanza vikao. Lakini pendekezo lililo chukuliwa sasa ni kwamba wajumbe wakifika nusu ya wajumbe wote (bila kujali wa bara au visiwani) vikao vitaendelea.

Hapo hapo kwenye akidi, kamati imependekeza kuwa, katika kufanya maamuzi ya kupitisha kila ibara basi yafanyike kwa kuzingatia idadi ya wajumbe kutoka pande zote za jamhuru ya muungano (wajumbe kutoka bara na wale wa visiwani).

Hivyo pendekezo la kamati ni kuwa angalau idadi ya wajumbe kutoka bara iwe 2/3 ya wajumbe wote kutoka bara, na kwa upande wa Zanzibar, wajumbe wawe 1/3 ya wajumbe wote kutoka Zanzibar ili kuweza kupiga kura/ au kufanya maamuzi.

UFAFANUZI WA HOJA KINZANI:

Wajumbe wa bunge maalumu la katiba baadhi yao walipinga uwepo wa hoja kinzani kwamba ni kupoteza muda na itafanya iwagawe zaidi wajumbe hao, hivyo hawakuona sababu ya kuwepo kwa hoja hiyo.

Lakini wajumbe wengine waliona ni vyema hoja kinzani ikawepo kwa kuwa itatoa fursa ya wale wachache ambao kwenye mijadala ya kamati uenda hoja yao isieleweke na isipate usikivu kamili, lakini hoja hiyo hiyo ikiletwa kwenye bunge la katiba itaweza kueleweka zaidi na kupitishwa.

Hapa hoja ime-base kwenye kusikiliza hasa zile hoja za wachache zilizokosa kusikilizwa kwenye ngazi ya kamati na kukosa kupitishwa lakini uenda zikawa na tija, hivyo ni vyema hoja hizo zisipuuzwe na hivyo zipelekwe kwenye ngazi ya bunge maalumu ili kupewa mjadala zaidi.

UFAFANUZI WA KURA YA SIRI vs KURA YA WAZI:

kamati imejadili suala la upigaji wa kura kwa namna ya siri na wazi na vilevile kamati imekubali kuwa namna zote za upigaji kura zipo sawa, hivyo kamati imeona ni vyema wajumbe wenyewe waliamue suala la upigaji kura kwa kulipigia kura na kuliamua.

SUALA LA SIWA (FIMBO YA BUNGE):

Hapa kwa kweli nimefurahishwa na kamati, sikutarajia kama kamati ingefanya maamuzi mazuri kama haya kwa kuzingatia maslahi ya wananchi. Kwa ufupi ni kwamba kamati imependekeza kuwa suala la SIWA liachwe, kwa maana kwamba hakutakuwa na haja ya kutengeneza fimbo kwa ajili ya bunge maalumu la katiba.

Sababu hasa ilyopelekea kamati kusitisha suala la SIWA imeelezwa kuwa ni gharama yake kuwa kubwa sana na hivyo hawapo tayari kuliingiza taifa katika gharama hiyo isiyokuwa na tija yoyote kwa Watanzania.
 
WanaJF

Bunge linaendelea hivi sasa na limeanza kwa kutoa ufafanuzi wa hoja
mbalimbali zilizo tolewa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba.

Kamati iliyokuwa ikiratibu uandaaji wa rasimu ya kanuni za bunge maalumu
la katiba imeanza kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na
wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuhusiana na kanuni za bunge
hilo.

tupe up date za kikao
 
WanaJF

Bunge linaendelea hivi sasa na limeanza kwa kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizo tolewa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba.

Kamati iliyokuwa ikiratibu uandaaji wa rasimu ya kanuni za bunge maalumu la katiba imeanza kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuhusiana na kanuni za bunge hilo.

Mungu awaongoze kura iwe ya SIRI...
 
Ukisikiliza kwa makini majadoliano ya wajumbe wa bunge hili utagundua kuwa kuna agenda ya kuchakachua wakati wa maamzi ya mwisho ndio maana sasa wamekomaa na kura ya wazi.
 
Sasa Jussa ndio anatoa maelezo ya uwasilishaji wa kamati katika bunge maalumu.
 
Kura ya wazi ni ajenda ya kuwafanya wabunge wasiwe huru wanataka kulazimishwa kuunga mkono itikadi zao za vyama
 
Kura ya wazi ni ajenda ya kuwafanya wabunge wasiwe huru wanataka kulazimishwa kuunga mkono itikadi zao za vyama

Kama huna update usipoteze muda. Hii ni thread kwa ajili ya update. Kwa sababu hata kama una maoni hauko bungeni.
 
Kura ya wazi ni ajenda ya kuwafanya wabunge wasiwe huru wanataka kulazimishwa kuunga mkono itikadi zao za vyama

Mkuu,

Hemu tuangalie kwanza mapendekezo ya kamati kuhusu hilo, jaribu kupunguza jazba.
 
UFAFANUZI WA KURA YA SIRI vs KURA YA WAZI. kamati imejadili suala la upigaji wa kura kwa namna ya siri na wazi na vilevile kamati imekubali kuwa namna zote za upigaji kura zipo sawa, hivyo kamati imeona ni vyema wajumbe wenyewe waliamue suala la upigaji kura. Hivyo suala hili limerudishwa kwa wajumbe wenyewe.
 
Duh hii ndio Tanzania.
 
Back
Top Bottom