Sihivyo rais alimchagua kuwa waziri akiwa ametoka kutuhumiwa kufanya ufisadi unafki ni janga LA taifa
huyu hapaAlimkalia kooni mcha Mungu, CAG Professor Assad, Lugola afanye haraka akamuombe msamaha ili roho ya Assad ikunjuke, bila hivyo ataendelea kuwa na wakati mgumu sana.
Alimdhulumu Assad kwa kujihami yeye na Allah anasema, hazidishiwi mwenye kudhulumu isipokuwa hasara.
Halafu Lugola huyo huyo atagombea ubunge kwa tiketi ya Chadema!BAADA ya Kangi Lugola, kuwekwa chini ya ulinzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa madai ya ufisadi, sasa kuwekwa kikaangoni bungeni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Kaboyoka ametoa hoja hiyo wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma, jana tarehe 29 Januari 2020, huku akimtuhumu Lugola kwamba alilipotosha bunge kuhusu ununuzi wa sare hizo.
“Kwa hiyo Kangi alilipotosha bunge kwa kuapa kwamba, atatoa nguo kama sare hazipo, inamaana hasomi hata taratibu,” amesema Kaboyoka.
Mwenyekiti huyo wa PAC amemkalia kooni Lugola, akimtaka aeleze sare hizo zilinunuliwa kutoa wapi pamoja na gharama zilizotumika kununua sare hizo.
“Huyo aliyepewa tenda alipatikanaje, sare zililetwa kutoka wapi, kiasi cha fedha iliyotumika ni ngapi? “ amehoji Kaboyoka.
Kaboyoka amesema Lugola akitoa maelezo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafuatilia sakata hilo, ili kujua kama idadi ya sare aliyoitoa, inaendana na idadi halisi iliyopo.
“Kuanzia hapo ndio CAG aweze kwenda stoo kujua kuna nini kutokana na zile ripoti, aone kwamba zile sare ziliagizwa mia na zimekuja mia, kinyume na hapo CAG hawezi kutoka akaenda kwenye stoo akaangalia kitu ambacho hana nyaraka zinazoonyesha kilichomo,” amesisitiza Kaboyoka.
“Nanyanyua mikono juu itakapofika jioni kama mimi nasema uongo kwamba hakuna sare hewa, najivua nguo, kamati ya mambo ya ulinzi na usalama na maofisa ya CAG twende stoo kuu tukaangalie makontena 15 na magodauni 5 yamesheheni sare za vitambaa. Nauweka uwaziri wangu rehani kama mimi nasema uongo,” Lugola aliapa bungeni.
Lugola pia alimtuhumu Profesa Mussa Assad, aliyekuwa CAG kwamba alisema uongo katika ripoti yake, juu ya ununuzi wa sare hizo.
“CAG amelihusisha Jeshi la Polisi na kashfa ya sare hewa, na kwamba sare hizi ni za bilioni 16.6. Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG,” alisisitiza Lugola.
Kwa sasa Lugola anakabiliwa na kashfa ya kuingia mkataba wa kifisadi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, ambapo anahojiwa na TAKUKURU.
Lugola anahojiwa na TAKUKURU baada ya Rais John Magufuli kuiagizataasisi hiyo kuchunguza mkataba huo, kwa ajili ya kujua wahusika ili wachukuliwe hatua.
Chanzo: Mwanahalisi
View attachment 1340857
Alhaj Assad yule aliyezushiwa kutekwa na ustaadh Zitto Kabwe?Alimkalia kooni mcha Mungu, CAG Professor Assad, Lugola afanye haraka akamuombe msamaha ili roho ya Assad ikunjuke, bila hivyo ataendelea kuwa na wakati mgumu sana.
Alimdhulumu Assad kwa kujihami yeye na Allah anasema, hazidishiwi mwenye kudhulumu isipokuwa hasara.
Weka link ulipotoa tukaitazame huko, vi file namna hiyo huwa najikinga navyo sana kufunguwa, nilishakumbwa na kirusi. Au ipandishe YouTube.huyu hapa
Itakuwa siyo huyo, ninaomuongelea ni former CAG Professor Assad aliyepikiwa majungu na mpishi mmojawapo ni Lugola.Alhaj Assad yule aliyezushiwa kutekwa na ustaadh Zitto Kabwe?
ukianza kuchagua video maana yake device yako ni TecnoWeka link ulipotoa tukaitazame huko, vi file namna hiyo huwa najikinga navyo sana kufunguwa, nilishakumbwa na kirusi. Au ipandishe YouTube.
Does it matter?ukianza kuchagua video maana yake device yako ni Tecno
Ukiona mtu anataka aonekane ni zaidi ya wote, halafu anaweka na mbwembwe nyingi kuonekana zaidi ya wengine, weka alama ya kuuliza.
Ile kuweka viraka vya bendera ya Taifa mpaka kwenye mashati, kama vile yeye ni mtanzania kuliko wengine. Kutembea ameshikilia ilani ya CCM kama vile yeye ni mwanaCCM kuwazidi wengine, ni dalili ya uovu anaotaka kuuficha kwa mbwembwe nyepesi nyepesi.
Mwigulu naye kuvaa skafu ya bendera ya Taifa kama vile yeye ni mtanzania zaidi kuliko wengine, ni jambo kujiuliza.
Mwalimu hakuwahi hata kuvaa kofia yenye bendera ya Taifa - ina maana akina Lugola na Mwigulu wamemzidi utaifa hata Baba yetu wa Taifa!!!
CCM wote ni WAKANGIHata John wa chatto nae ni kangi ?
Pointwabunge wa CCM wanafiki wakubwa walimponda sana CAG wakiongozwa na Spika na huyo Lugola alidiriki kusema sare zilinunuliwa na zipo hakuna mtu mwongo kama CAG wakapiga makofi leo hii hiyo ripoti ya ASSAD wanaitumia kumsulubu Kangi, wanafiki wakubwa nyie
Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG