Bungeni: Mwenyekiti PAC amtaka Kangi Lugola kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

Bungeni: Mwenyekiti PAC amtaka Kangi Lugola kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

Alimkalia kooni mcha Mungu, CAG Professor Assad, Lugola afanye haraka akamuombe msamaha ili roho ya Assad ikunjuke, bila hivyo ataendelea kuwa na wakati mgumu sana.

Alimdhulumu Assad kwa kujihami yeye na Allah anasema, hazidishiwi mwenye kudhulumu isipokuwa hasara.
 
Alimkalia kooni mcha Mungu, CAG Professor Assad, Lugola afanye haraka akamuombe msamaha ili roho ya Assad ikunjuke, bila hivyo ataendelea kuwa na wakati mgumu sana.


Alimdhulumu Assad kwa kujihami yeye na Allah anasema, hazidishiwi mwenye kudhulumu isipokuwa hasara.
huyu hapa
 

Attachments

  • Bunge hili la CCM lina unafiki sana. Spika anatumika hovyo. Wakati Kangi Lugola ( Source ).mp4
    3.2 MB
BAADA ya Kangi Lugola, kuwekwa chini ya ulinzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa madai ya ufisadi, sasa kuwekwa kikaangoni bungeni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).



Kaboyoka ametoa hoja hiyo wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma, jana tarehe 29 Januari 2020, huku akimtuhumu Lugola kwamba alilipotosha bunge kuhusu ununuzi wa sare hizo.

“Kwa hiyo Kangi alilipotosha bunge kwa kuapa kwamba, atatoa nguo kama sare hazipo, inamaana hasomi hata taratibu,” amesema Kaboyoka.

Mwenyekiti huyo wa PAC amemkalia kooni Lugola, akimtaka aeleze sare hizo zilinunuliwa kutoa wapi pamoja na gharama zilizotumika kununua sare hizo.

“Huyo aliyepewa tenda alipatikanaje, sare zililetwa kutoka wapi, kiasi cha fedha iliyotumika ni ngapi? “ amehoji Kaboyoka.

Kaboyoka amesema Lugola akitoa maelezo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafuatilia sakata hilo, ili kujua kama idadi ya sare aliyoitoa, inaendana na idadi halisi iliyopo.

“Kuanzia hapo ndio CAG aweze kwenda stoo kujua kuna nini kutokana na zile ripoti, aone kwamba zile sare ziliagizwa mia na zimekuja mia, kinyume na hapo CAG hawezi kutoka akaenda kwenye stoo akaangalia kitu ambacho hana nyaraka zinazoonyesha kilichomo,” amesisitiza Kaboyoka.

“Nanyanyua mikono juu itakapofika jioni kama mimi nasema uongo kwamba hakuna sare hewa, najivua nguo, kamati ya mambo ya ulinzi na usalama na maofisa ya CAG twende stoo kuu tukaangalie makontena 15 na magodauni 5 yamesheheni sare za vitambaa. Nauweka uwaziri wangu rehani kama mimi nasema uongo,” Lugola aliapa bungeni.

Lugola pia alimtuhumu Profesa Mussa Assad, aliyekuwa CAG kwamba alisema uongo katika ripoti yake, juu ya ununuzi wa sare hizo.

“CAG amelihusisha Jeshi la Polisi na kashfa ya sare hewa, na kwamba sare hizi ni za bilioni 16.6. Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG,” alisisitiza Lugola.

Kwa sasa Lugola anakabiliwa na kashfa ya kuingia mkataba wa kifisadi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, ambapo anahojiwa na TAKUKURU.

Lugola anahojiwa na TAKUKURU baada ya Rais John Magufuli kuiagizataasisi hiyo kuchunguza mkataba huo, kwa ajili ya kujua wahusika ili wachukuliwe hatua.

Chanzo: Mwanahalisi
View attachment 1340857
Halafu Lugola huyo huyo atagombea ubunge kwa tiketi ya Chadema!
 
Alimkalia kooni mcha Mungu, CAG Professor Assad, Lugola afanye haraka akamuombe msamaha ili roho ya Assad ikunjuke, bila hivyo ataendelea kuwa na wakati mgumu sana.

Alimdhulumu Assad kwa kujihami yeye na Allah anasema, hazidishiwi mwenye kudhulumu isipokuwa hasara.
Alhaj Assad yule aliyezushiwa kutekwa na ustaadh Zitto Kabwe?
 
Ukila na kipofu Usimguse mikono sasa Lugola aka mzee wa ilani alisahau kupereka 10 pacent sasa yanamtokea puani
 
Weka link ulipotoa tukaitazame huko, vi file namna hiyo huwa najikinga navyo sana kufunguwa, nilishakumbwa na kirusi. Au ipandishe YouTube.
ukianza kuchagua video maana yake device yako ni Tecno
 
Kwani lazima alivyoishi mwalimu kika mtu afanye hivyo. Hata hueleweki.
Ukiona mtu anataka aonekane ni zaidi ya wote, halafu anaweka na mbwembwe nyingi kuonekana zaidi ya wengine, weka alama ya kuuliza.

Ile kuweka viraka vya bendera ya Taifa mpaka kwenye mashati, kama vile yeye ni mtanzania kuliko wengine. Kutembea ameshikilia ilani ya CCM kama vile yeye ni mwanaCCM kuwazidi wengine, ni dalili ya uovu anaotaka kuuficha kwa mbwembwe nyepesi nyepesi.

Mwigulu naye kuvaa skafu ya bendera ya Taifa kama vile yeye ni mtanzania zaidi kuliko wengine, ni jambo kujiuliza.

Mwalimu hakuwahi hata kuvaa kofia yenye bendera ya Taifa - ina maana akina Lugola na Mwigulu wamemzidi utaifa hata Baba yetu wa Taifa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zidumu fikra za mwalimu wangu Assad ..
 
wabunge wa CCM wanafiki wakubwa walimponda sana CAG wakiongozwa na Spika na huyo Lugola alidiriki kusema sare zilinunuliwa na zipo hakuna mtu mwongo kama CAG wakapiga makofi leo hii hiyo ripoti ya ASSAD wanaitumia kumsulubu Kangi, wanafiki wakubwa nyie
Point
 
Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG
 
Jinamizi la LUGUMI halijaibuka tena???

Ila wafuasi wa chama fulani kwa UNAFIKI wana PhD...

Tumeipenda wenyewe....


Everyday is Saturday...............😎
 
Back
Top Bottom