Uchaguzi 2020 Bungeni: Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, Bunge zima(Wabunge 350) wampigia kura za ndiyo

Yaani hakika nimefurahi mno. Majaliwa ni best PM. Ana busara nyingi, mnyenyekevu na mtendaji.

Hongera sana Mh. Rais kwa kumuamini tena Mh. Majaliwa.

Moja ya wa wasioweza kumsaidia Rais kabisa! Mambo mengi ya serikali yanayoibuliwa na kufanywa na Rais yalipaswa kufanywa na huyu jamaa lakini kila mara yeye yuko nyuma.

Unachokiita ni unyenyekevu hasa ni uoga!
 


Alifanya kazi kubwa kuzuia uhuru wa Watanzania na kuhakikisha hana mpinzani hata kwenye jimbo lake. Vilevile ameshirikiana na usalama wa taifa kuhakikisha Tanzania inatoka kwenye demokrasia na kuingia kkwenye mfumo mpya wa kisasa wa Chama kimoja kama China. Amefanikiwa kuhakikisha wapinzani wote wenye nguvu wamefungiliwa kesi na kupigwa na polisi pale ambako wamejaribu kuhoji serikali. Mpaka sasa kuna wabunge 8 tu wa upinzani na kazi kubwa na kuongeza kura kila mahali na kuweka mipango kuhakikisha CCM inashinda kila mahali hata zile sehemu ambazo wananchi hawakuchagua CCM. Ushahidi wa kura za ubunge kutokulingana ni kuonyesha wazi mipango ya majaliwa hata sehemu nyingine kuta za raisi zimezidi kura zote zilizopigwa kwa ubunge. Kuna Mbunge wa CUF wa Temeke kapata kura sifuri yaani hata yeye hajajipigia kura! Haya ni mafanikio makubwa sana. Hongera sana Majaliwa na Hongera sana CCM
 
Moja ya wa wasioweza kumsaidia Rais kabisa! Mambo mengi ya serikali yanayoibuliwa na kufanywa na Rais yalipaswa kufanywa na huyu jamaa lakini kila mara yeye yuko nyuma.

Unachokiita ni unyenyekevu hasa ni uoga!
Hakuna kitu kizuri kama kumuelewa boss wako. Ndiyo maana amemteua tena.
 
Ha
Hapo kwenye majukumu ya Waziri Mkuu, ongeza na jukumu la kusema uongo tena hadharani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…